085-Hiswnul-Muslim: Kafara Ya Kikao
Hiswnul-Muslim
085-Kafara Ya Kikao
[196]
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
Subhaanaka-Allaahumma wabihamdika, ash-hadu an laa ilaaha illaa Anta astaghfiruka wa atuwbu Ilayka
Utakasifu ni Wako ee Allaah, na Himdi ni Zako. Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Nakuomba Unigfhurie na ninarejea Kwako kutubia[1]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah na wengineo (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:
((مَنْ جَلَسَ فِي مَجْلِسٍ فَكَثُرَ فِيهِ لَغطُهُ فَقَالَ قَبْلَ أَنْ يَقُومَ: سُبْحَانَكَ اللَهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، أَشْهَدُ أَن لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ, إِلَّا غفَرَ لَهُ مَا كَانَ فِي مَجْلِسِهِ ذَلِكَ))
((Atakayekaa kikao akapiga porojo, kisha kabla ya kuondoka kikao hicho akasema:
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
Subhaanaka-Allaahumma wabihamdika, ash-hadu an laa ilaaha illaa Anta astaghfiruka wa atuwbu Ilayka. Basi Allaah Atamghufuria yaliyojiri katika kikao hicho)) – Aswaabus-Sunan; Abu Daawuwd [4859], At-Tirmidhiy (5/494) [3433], An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah’ [397], Ibn Hibbaan (2/354) [594]. na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Jaami’ [6192].
Na imethibiti kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: “Hajapatapo kukaa Rasuli wa Allaah(صلى الله عليه وسلم) kikao wala kusoma Qur-aan wala kuswali ila atamaliza na Du'aa hii’. Akasema 'Aaishah (رضي الله عنها) nikamuuliza “Ee Rasuli wa Allaah, nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur-aan wala huswali Swalaah yoyote ile ila unaimalizia kwa kusoma maneno haya kwanini hasa? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Ndio! Aayesema kheri amalize kwa kheri na anayesema shari yanakuwa maneno haya ni kafara kwake)) Ameipokea An-Nasaaiy katika Amal al-Yawm wal-Laylah [308], Ahmad (6/77), na ameisahihisha Faaruwq Hamaadah katika tahqiqi yake ya ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah ya An-Nasaaiy (Uk. 273)