086-Hiswnul-Muslim: Kumuombea Du’aa Anaekuombea Maghfirah Kwa Allaah
Hiswnul-Muslim
086-Kumuombea Du’aa Anaekuombea Maghfirah Kwa Allaah
[197]
Akimuombea mtu maghfirah mwenzake akasema:
غَفَـرَ اللهُ لَكَ
Ghafara-Allaahu laka
Allaah Akughufurie
Amjibu:
وَلَكَ
Walaka
Nawe (Akughufurie)[1]
[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah Bin Sarjis (رضي الله عنه) amesema:
رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَكَلْتُ مَعَهُ خُبْزًا وَلَحْمًا أَوْ قَالَ ثَرِيدًا. قَالَ: فَقُلْتُ لَهُ: ((أَسْتَغْفَرَ لَكَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) قَالَ: ((نَعَمْ وَلَكَ)) ثُمَّ تَلَا هَذِهِ الْآيَةَ: ((وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ))
”Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) nikala pamoja naye mkate na nyama [au thariydaa – mkate katika supu ya nyama] Nikamwambia: ”Allaah Akughufurie ee Nabiy. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) Akasema: ((Ndio, nawe pia [Akufughufurie])). Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akasoma:
((وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ))
((Na omba maghfirah kwa dhambi zako na (kwa dhambi za) Waumini wa kiume na Waumini wa kike)) – Muslim [2346]. Na riwaayah nyingine kwa tamshi tofuati kidogo katika Ahmad (5/82), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (Uk. 218) [421] kwa tahqiyq ya Faaruwq Hamaadah. Aayah katika Suwrat Muhammad [19].