094-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kukhofia Mkosi Nuksi

Hiswnul-Muslim

094-Du’aa Ya Kukhofia Mkosi Nuksi

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[205]

اللّهُـمَّ لا طَيْـرَ إِلاّ طَيْـرُك، وَلا خَـيْرَ إِلاّ خَـيْرُك، وَلا إِلهَ غَيْـرُك

 

Allaahumma laa twayra illaa twayruka, walaa khayra illaa khayruka, walaa ilaaha Ghayruka

 

Ee Allaah hapana mkosi ila Ulioukadiria Wewe, na hapana kheri ila kheri Yako, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako.[1]

 

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنه), Kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم):

 

((مَنْ رَدَّتْهُ الطِّيَرَةُ عَنْ حَاجَتِهِ فَقَدْ أَشْرَكَ)) قَالُوا: فَمَا كَفَّارَةُ ذَلِكَ؟ قَالَ: ((أَنْ يَقُولَ اللَّهُمَّ لاَ خَيْرَ إِلاَّ خَيْرُكَ وَلاَ طَيْرَ إِلاَّ طَيْرُكَ  وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ))

 

((Atakayerudi nyuma pasina na kuitekeleza haja yake kwa sababu ya at-twiyarah [kuogopa mkosi] amefanya shirki)) Wakuliza: Basi nini kafara yake? Akajibu: ((Aseme:

 

اللَّهُمَّ لاَ خَيْرَ إِلاَّ خَيْرُكَ وَلاَ طَيْرَ إِلاَّ طَيْرُكَ وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ

 Allaahumma laa khayra illa khayruka, wa laa twayra illa twayruka, wa laa ilaaha ghayruka – Ee Allaah, hakuna kheri ila Uiletayo Wewe, wala hakuna mkosi ila Ulioukadiria Wewe, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako))

 

Ahmad (2/220), Ibn As-Shunniy (292), na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (3/54) [1065]. Ama fali, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akipendezewa na kwa hivyo alisikia neno zuri kwa mtu akalipenda akasema: ((Tumechukua fali kutoka [mdomoni] kwako)) Abu Daawuwd [3917], Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (2/363) kutoka kwa Abu Shaykh katika ‘Akhlaaq An-Nabiyy (صلى الله عليه وسلم)’ (Uk. 270).

 

At-Twayr, Atw-Twiyara  (Ndege): Itikadi za ushirikina kutabiri jambo kama lina nuksi, mkosi, ukorofi au kama lina kheri ili walitende. Hutumia ndege; humrusha basi anaporuka kuliani huitakidi kuwa ni kheri, na anaporuka upande wa kushoto huitakidi kuwa kuna shari. Hii ni shirki kubwa kwa sababu ni kubashiria mambo ya ghayb.

 

 

Share