096-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Safari
Hiswnul-Muslim
096-Du’aa Ya Safari
[207]
اللهُ أكبَر، اللهُ أكبَر، اللهُ أكبَر، سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ ﴿١٣﴾ وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ ﴿١٤﴾ اللّهُـمَّ إِنّا نَسْـأَلُكَ في سَفَـرِنا هذا البِـرَّ وَالتَّـقْوى، وَمِنَ الْعَمَـلِ ما تَـرْضى، اللّهُـمَّ هَوِّنْ عَلَـينا سَفَرَنا هذا وَاطْوِ عَنّا بُعْـدَه، اللّهُـمَّ أَنْـتَ الصّـاحِبُ في السَّـفَر، وَالْخَلـيفَةُ في الأهـلِ، اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنْ وَعْـثاءِ السَّـفَر، وَكَآبَةِ الْمَنْـظَر، وَسوءِ الْمُنْـقَلَبِ في المـالِ وَالأَهْـل.
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar. Subhaanalladhiy sakkhara lanaa haadhaa wamaa kunnaa Lahu muqriniyn, wainnaa ilaa Rabbina lamunqalibuwn. Allaahumma innaa nas-aluka fiy safarina haadha al-birra wat-taqwaa, waminal ’amali maa Tardhwaa. Allaahumma hawwin ‘alaynaa safaranaa haadhaa, wa atwi ‘annaa bu’-dahu. Allaahumma Antasw-Swaahibu fis-safari, wal Khaliyfatu fil ahli. Allahumma inniy a’uwdhu Bika min wa’thaais-safari, wa kaabatil mandhwar, wa suw-il munqalabi filmaali wal ahli
Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, ((Utakasifu ni wa (Allaah) Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti. (huyu mnyama au chombo) “Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea)) Ee Allaah, hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na taqwa, na katika matendo Unayoridhia, Ee Allaah, Ifanye nyepesi safari yetu hii, na Ifupishe umbali wake, Ee Allaah, Wewe Ndiye Unayesuhubiana nami katika safari na Mchungaji wa familia yangu. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ugumu wa safari na ubaya wa mtizamo na uovu wa kubadilikiwa katika mali na familia .
Wakati wa kurudi safari atayasema hayo yalioko juu na kisha atazidisha:
آيِبُـونَ تائِبُـونَ عابِـُدونَ لِرَبِّنا حـامِـدُونَ
Aayibuwna, taaibuwna, ‘aabiduwnaa, li Rabbinaa haamiduwna
Tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Rabb wetu tunamsifu[1]