097-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuingia Mjini Au Kijijini
Hiswnul-Muslim
097-Du’aa Ya Kuingia Mjini Au Kijijini
[208]
أللّـهُمَّ رَبَّ السَّـمواتِ السّـبْعِ وَما أَظْلَلَـنَ، وَرَبَّ الأَراضيـنَ السّـبْعِ وَما أقْلَلْـنَ، وَرَبَّ الشَّيـاطينِ وَما أَضْلَلْـنَ، وَرَبَّ الرِّياحِ وَما ذَرَيْـنَ، أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَ هذهِ الْقَـرْيَةِ وَخَيْـرَ أَهْلِـها، وَخَيْـرَ مَا فِيهَا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها وَشَـرِّ أَهْلِـها، وَشَـرِّ مَا فِيهَا
Allaahumma Rabbas-samaawaatis-sab’i wamaa adhw-lalna. Wa Rabbal-araadhwiynas-sab’i wamaa aqlalna. Wa Rabbash-shayaatwiyni wamaa adhw-lalna. Wa Rabbar-riyaahi wamaa dharayna. As-aluka khayra haadhihil-qaryati wakhayra ahlihaa, wakhayra maa fiyhaa. Wa a’uwdhu Bika min sharrihaa, washarri ahlihaa, washarri maa fiyhaa
Ee Allaah Rabb wa mbingu saba na kila ambacho hizo mbingu zimekipa kivuli, na Rabb wa ardhi saba na kila ambacho zimebeba, na Rabb wa mashaytwaan na walichokipoteza, na Rabb wa upepo na ulichokibeba. Nakuomba kheri ya kijiji hichi na kheri ya watu wake na kheri ya vilivyo ndani yake, Najikinga Kwako na shari ya kijiji hichi na shari ya watu wake, na shari iliyomo ndani yake[1]
[1]Hadiyth ya Swuhayb bin Sinaan Ar-Ruwmiy (رضي الله عنه) - Al-Haakim na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahabiy (2/100) na ibn As-Sunniy [524] na Al-Haafidhw ameipa daraja ya Hasan katika Takhriyj Al-Adhkaar (5/154). Ibn Baaz (رحمه الله) amesema: Na ameipokea An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah’ [547, 549] kwa Isnaad ya Hasan. angalia: Tuhfat Al-Akhyaar (Uk.370)