098-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuingia Sokoni, Madukani
Hiswnul-Muslim
098- Du’aa Ya Kuingia Sokoni, Madukani
[209]
لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُلْـكُ ولهُ الحَمْـد، يُحْيـي وَيُميـتُ وَهُوَ حَيٌّ لا يَمُـوت، بِيَـدِهِ الْخَـيْرُ وَهوَ عَلىَ كلّ شيءٍ قَدِيرٌ.
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu, Yuhyiy wa Yumiytu wa Huwa Hayyun laa yamuwtu, Biyadihil-khayru wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme na ni Zake Himdi, Anahuisha na Anafisha, Naye ni Hai Asiyekufa, kheri iko mikononi Mwake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza[1]
[1]Hadiyth ya ‘Umar bin Khatwaab(رضي الله عنه) Kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم):
amesema: ((Atakayeingia sokoni akasema [hiyo du’aa] Allaah Atamuandikia mema milioni, Atamfutia maovu milioni, Atampandisha Daraja milioni)) na ((atajengewa nyumba katika Jannah) At-Tirmidhiy (5/291) [3429], Al-Haakim (1/538), Ibn Maajah [2235] Ad-Daarimiy na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Ibn Maajah (2/21) na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/152). Na angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (6231).
Tanbihi: ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu usahihi wake: Ibn Baaz (رحمه الله) amesema: “Ni Dhwa’iyf, ila inapasa kumdhukuru Allaah (عزّ وجلّ) kwa wingi hata anapoingia sokoni kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimdhukuru Allaah kila wakati.” Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anatuamrisha:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾
Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru.
وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
Na Msabbihini asubuhi na jioni. [Al-Ahzaab: 41-42]