101-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Wakaazi Wanayomuombea Anaesafiri
Hiswnul-Muslim
101-Du’aa Ya Wakaazi Wanayomuombea Anaesafiri
[212]
أَسْتَـوْدِعُ اللَّهَ دِيـنَكَ وَأَمانَتَـكَ، وَخَـواتيـمَ عَمَـلِكَ
Astawdi’u Allaaha Diynaka, wa amaanataka, wa khawaatiyma ‘amalika
Naweka amana kwa Allaah Dini yako na uaminifu wako na mwisho wa matendo yako[1]
Mwanamke aambiwe:
أَسْتَـوْدِعُ اللَّهَ دِيـنَكِ وَأَمانَتَـكِ، وَخَـواتيـمَ عَمَـلِكِ
Astawdi’u Allaaha Diynaki, wa amaanataki, wa khawaatiyma ‘amaliki
[213]
زَوَّدَكَ اللَّهُ التقْوى، وَغَفَـرَذَنْـبَكَ، وَيَسَّـرَ لَكَ الخَـيْرَ حَيْـثُما كُنْـتَ
Zawwadaka -Allaahut-taqwa waghafara dhanbaka, wayassara lakal-khayra haythu maa kunta
Allaah Akuzidishie taqwa na Akughufurie madhambi yako, na Akufanyie wepesi katika kheri popote ulipo[2]
Mwanamke aambiwe:
زَوَّدَكِ اللَّهُ التقْوى، وَغَفَـرَذَنْـبَكِ، وَيَسَّـرَ لَكِ الخَـيْرَ حَيْـثُما كُنْـتِ
ZawwadakiLLaahut-taqwa waghafara dhanbaki, wayassara lakil-khayra haythu maa kunti
[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما)
قال سالم بن عبدالله بن عمر، أنَّ عبدالله بن عمر رضي الله عنهما كان يقول للرجلِ إذا أراد سفرًا: ادنُ مني أودِّعك كما كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يودعنا، فيقول….
Saalim bin ‘Abdullah bin ‘Umar amesema: Mtu alipotaka kusafiri, ‘Abdullaah bin Umar humwambia: Nikaribie nikuage kama alivyokuwa akituaga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) husema:
أَسْتَـوْدِعُ اللَّهَ دِيـنَكَ وَأَمانَتَـكَ، وَخَـواتيـمَ عَمَـلِكَ
Ahmad (7/2), At-Tirmidhiy (5/499) [2443], Ibn Maajah na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (2/155), Swahiyh Ibn Maajah [2296] Silsilatus-Swahiyhah (14)
[2]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه)
قال: جاء رجلٌ إلى النبي -صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله، إني أريدُ سفرًا، فزوِّدني، فقال: ((زوَّدك اللهُ التقوى))، قال: زدني، قال: ((وغفر ذنبَك))، قال: زدني،قال: ((ويسَّر لك الخيرَ حيثما كُنْتَ))
Amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, mimi nataka kusafiri, basi nipatie (mahitajio ya safari; niombee du’aa ya Baraka). Akasema: ((Allaah Akuzidishie taqwa)) Akasema: Nizidishie: Akasema: ((na Akughufurie madhambi yako)) Akasema: Nizidishie: Akasema: ((Na Akufanyie wepesi katika kheri popote ulipo)) - At-Tirmidhiy [2444] Taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/155)