103-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Msafiri Unapoingia Usiku

Hiswnul-Muslim

103-Du’aa Ya Msafiri Unapoingia Usiku

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

[215]   

سَمِـعَ سـامِعُ بِحَمْـدِ اللهِ وَحُسْـنِ بَلائِـهِ عَلَيْـنا. رَبَّنـا صـاحِبْـنا وَأَفْـضِل عَلَيْـنا عائِذاً باللهِ مِنَ النّـار

 

Sami’a (pia Samma’a) Saami’un BihamdiLLaah, wa husni balaaihi ‘alaynaa. Rabbanaa swaahibnaa, wa Afdhwil ‘alaynaa ‘aaidhan biLLaahi minan-naari

 

Amesikia msikilizaji kwa kumhimidi Allaah, na uzuri wa mitihani Yake juu yetu.  Rabb wetu kuwa nasi na Tufadhilishe hali ya kuwa tunajikinga na Allaah kutokana na Moto[1]

 

 

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah  (رضي الله عنه) - Muslim (4/2086) Na maana ya

سَمِـعَ سـامِعُ

Yaani: “Ameshuhudia shahidi juu ya kumhimidi kwetu Allaah Ta’aalaa kwa Neema Zake na uzuri wa mitihani Yake kwetu” Ama maana ya ‘Samma’a Saami’un ni: “Amefikisha msikilizaji kauli yangu hii kwa mwengine” Na amesema tanbihi kama hiyo katika Nyiradi za sihri na Du’aa.  Na kauli yake: 

رَبَّنـا صـاحِبْـنا وَأَفْـضِل عَلَيْـنا

Yaani: Tuhifadhi na Tufadhilishe kwa wingi wa neema Zako na Tuepushe na kila yanayochukiza”  Sharh An-Nawawy (17/39)

 

 

Share