104-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Msafiri Akishuka Sehemu Wakati Yuko Safarini Au Mahali Penginepo
Hiswnul-Muslim
104-Du’aa Ya Msafiri Akishuka Sehemu Wakati Yuko Safarini Au Mahali Penginepo
[216]
أَعـوذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ مِنْ شَـرِّ ما خَلَـق
A’uwdhu Bikalimati-LLaahit-ttaammati min sharii maa Khalaq
Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari alichokiumba[1]
[1]Hadiyth ya Khawlah bint Haakim (رضي الله عنهما)
((مَنْ نَزلَ مَنزِلاً ثُمَّ قال : أَعُوذُ بِكَلِمات اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ ، لَمْ يضرَّه شَيْءٌ حتَّى يرْتَحِل مِنْ منزِلِهِ ذلكَ))
((Atakayeteremka katika kituo (au makazi) kisha akasema:
أَعـوذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ مِنْ شَـرِّ ما خَلَـق
Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba - hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo (au makazi) hicho)) - Muslim (4/2080) [2708].
Tanbihi: Du’aa hii anaweza kuisoma mtu anapohamia sehemu mpya au nyumba mpya na si kufanya mambo ambayo yamezoeleka katika jamii kutendwa kama kuchinja na mialiko ya watu kukusanyika kusoma na mengineyo ambayo ni ya shirki na bid’ah.