105-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Msafiri Akirudi Kutoka Safarini
Hiswnul-Muslim
105-Du’aa Ya Msafiri Akirudi Kutoka Safarini
[217]
اللّهُ أَكْـبَر، اللّهُ أَكْـبَر، اللّهُ أَكْـبَر
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar
Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa.
Kisha sema:
لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمْد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَـدير، آيِبـونَ تائِبـونَ عابِـدونَ لِرَبِّـنا حـامِـدون، صَدَقَ اللهُ وَعْـدَه، وَنَصَـرَ عَبْـدَه، وَهَزَمَ الأَحْـزابَ وَحْـدَه.
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku walahul-Hamd, wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Aaibuwna, taaibuwna, ’aabiduwna li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa-Allaahu Wa’dahu, wa Naswara ’Abdahu, wa Hazamal-ahzaaba Wahdahu
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ufalme ni Wake, na Himdi ni Zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Tunanarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Rabb wetu tunamsifu. Amesadikisha Allaah ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake[1]
[1] Imepokewa kutoka kwa Ibn `Umar (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akirudi vitani au kutoka Hijjah katika kila akipanda mlima akisema hivyo. Al-Bukhaariy (7/163) [1797], Muslim (2/980) [1344].