106-Hiswnul-Muslim: Anachopaswa Kusema Mtu Ikimfikia Khabari Ya Kufurahisha Au Ya Kusikitisha
Hiswnul-Muslim
106-Anachopaswa Kusema Mtu Ikimfikia Khabari Ya Kufurahisha Au Ya Kusikitisha
[218]
Alikuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) ikimfikia khabari ya kufurahisha akisema:
الْحَمْـدُ للهِ الَّذي بِنِـعْمَتِهِ تَتِـمُّ الصّـالِحَات
AlhamduliLLaahiL-Ladhiy Bini’matihi tattimusw-swaalihaat
Himdi Anastahiki Allaah Ambaye kwa neema Yake yanatimia mambo mema.
Na ikimjia khabari ya kusikitisha kusema:
الْحَمْـدُ للهِ على كُـلِّ حاَلٍ
Alhamdu-liLLaahi ‘alaa kulli haal
Himdi Anastahiki Allaah kwa hali zote[1]
[1]Hadiyth ya ’Aaishah (رضي الله عنها) - Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [378], Al-Haakim akaisahihisha (1/499) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Jaami’ (4/201) [4640]. Taz pia Swahiyh Ibn Maajah [3081].