107-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وسلم)
Hiswnul-Muslim
107-Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وسلم)
[219]
قال رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلَاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayeniswalia mara moja basi Allaah Atamswalia mara kumi))[1]
[220]
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تجعلوا قبري عيدا، وصلوا علي فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kurejewa rejewa, na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo))[2]
[221]
وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْبَخِيلُ مَنْ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيَّ))
Pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Bakhili ni yule ambaye nikitajwa haniswalii))[3]
[222]
وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مَلائِكَةً سَيَّاحِينَ فِي الأَرْضِ يُبَلِّغُونِي مِنْ أُمَّتِي السَّلام))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Ana Malaika wanamzunguka katika ardhi, wananiletea salaam kutoka kwa Ummah wangu))[4]
[223]
وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم َ: ((مَا مِنْ أحَدٍ يُسَلِّمْ علَيَّ إلاَّ رَدَّ اللهُ رُوحِي حَتَّى أَرُدَّ عَلَيْهِ السَّلامَ))
Na pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakuna mtu yeyote anayeniswalia ila Allaah hunirudisha roho yangu ili nimrudishie salaam))[5]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (1/288) [408] Amesema Al-Bukhaariy katika Swahiyh yake: Abul Al-‘Aaaliyah amesema: “Swalah ya Allaah ni kumsifu kwake mbele ya Malaika na Swalah ya Malaika ni du’aa”
[2]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2/218) [2042], Ahmad (2/367) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (2/383)
[3]Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (5/551) p3546], na wengineo na angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (3/25) [2787] na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/177)
[4]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - An-Nasaaiy (3/43), Al-Haakim (2/421) na ameisahihisha katika Swahiyh An-Nasaaiy (1/274)
[5]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2041), na Al-Albaaniy (رحمه الله) ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/283)
Tanbihi: Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وسلم) ni kumswalia kama ilivyothibiti katika Sunnah navyo ni kama tunavyomswalia kwa Swalaatul-Ibraahimiyyah kwenye kikao cha Tashahhud kwenye Swalaah, au kumswalia kwa kifupi na kumswalia kila siku na kila mara anapotajwa na kukithirisha kumswalia siku ya Ijumaa. Lakini haijuzu mikusanyiko ya watu katika masiku wanayodai ni mawlid yake, akaswaliwa Nabiy (صلى الله عليه وسلم).