108-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Kueneza Na Kudhihirisha Maamkuzi Ya Kiislamu
Hiswnul-Muslim
108-Fadhila Za Kueneza Na Kudhihirisha Maamkuzi Ya Kiislamu
[224]
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: لا تَدْخُـلُوا الـجَنَّةَ حتـى تُؤمِنُوا، ولا تُؤمِنُوا حتـى تَـحابُّوا أوَلا أدُلُّكُمْ علـى شَيءٍ إذا فَعَلْتُـمُوهُ تَـحَابَبْتُـمْ؟ افْشُوا السّلامَ بَـيْنَكُمْ.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hamtoingia Jannah hadi muamini, na wala hamuwezi kuamini hadi mpendane. Je, nikujulisheni jambo ambalo mtakapolifanya mtapendana? Toleaneni Salaam baina yenu)) [1]
[225]
Na amesema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم)
ثَلاَثٌ مَنْ جَمَعَهُنَّ فَقَدْ جَمَعَ الإِيمَانَ: الإِنْصَافُ مِنْ نَفْسِكَ، وَبَذْلُ السَّلاَمِ لِلْعَالَمِ، وَالإِنْفَاقُ مِنَ الإِقْتَار
((Mambo matatu anaeyakusanya basi amekusanya imani; uadilifu wa nafsi yako na kutowa salaam kwa watu wote na kutoa swadaqah hali ya kuwa ni mchache wa mali))[2]
[226]
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الْإِسْلَامِ خَيْرٌ؟ قَالَ: تُطْعِمُ الطَّعَامَ وَتَقْرَأُ السَّلَامَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ
Imepokewatoka kwa ‘Abdullaah bin ’Amr (رضي الله عنهما) kwamba mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم): ”Ni Uislamu gani bora?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akasema: ((Kulisha chakula, na kumsalimia unayemjua na usiyemjua))[3]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) Muslim (1/74) [54] na wengineo
[2]Hadiyth ya ‘Ammaar bin Yaasir (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (1/82) - Mawquwfan Mu’allaqan (Ni Hadiyth iliyioshia kwa Swahaaba wa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) na kukatika sanad yake).
[3] Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (1/55) [12], Muslim (1/65) [39]