109-Hiswnul-Muslim: Namna Ya Kumrudishia Salaam Kafiri Anapokusalimia
Hiswnul-Muslim
109-Namna Ya Kumrudishia Salaam Kafiri Anapokusalimia
[227]
إِذَا سَلَّم عَلَيْكُمْ أهْلُ الكِتَابِ؛ فَقُولُوا: وَعَلَيْكُمْ
Ahlul-Kitaab (Mayahudi na Manaswara) wakikuamkieni (maamkizi ya maangamizi) semeni:
وَعَلَيْكُمْ
Wa ’alaykum
Na juu yenu[1]
[1] Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/42) [6258], Muslim (4/1705) [2163].
Tanbihi: Lakini wakikusalimieni kwa maamkizi mema yaliyo bayana na sahihi yaani wakisema:
السَّلامُ عَلَيْكُم
”Assalaamu ’alaykum”
Basi jibuni vizuri kama vile Alivyomrisha Allaah (سبحانه وتعالى) yaani mjibu:
وعليكم السلام
Imethibiti hivyo kutoka kwa ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu Aayah:
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ
Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo. [An-Nisaa 4: 86] – Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad [1107]
Ama wakikuamkieni kwa matamshi yasiyokuwa bayana kama vile ”assaam ’alaykum” bila ya kutamka herufi ya laam ambayo inapeleka kuleta maana ya: ”mauti yawe juu yenu”, basi ndio mjibu hivyo: ”Wa ’alaykum”
Hadiyth ya Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:
((إِذَا سَلَّمَ عَلَيْكُمُ الْيَهُودُ فَإِنَّمَا يَقُولُ أَحَدُهُمُ السَّامُ عَلَيْكُمْ فَقُولوا: وَعَلَيْكَ))
((Akikusalimieni Myahudi, kawaida husema “Assaam ‘alaykum (mauti yakufikeni), basi semeni: “wa ‘alayka” (na kwako yakufikie)) Al-Bukhaariy [6257], Muslim [2164].