113-Hiswnul-Muslim: Anachopaswa Kusema Muislamu Akimsifu Muislamu Mwenziwe

Hiswnul-Muslim

113-Anachopaswa Kusema Muislamu Akimsifu Muislamu Mwenziwe

www.alhidaaya.com

 

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[231]

 

قال رسول اللّه صلى اللّه عليه وسلم‏:‏‏ ((إِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ مَادِحًا صَاحِبَهُ لَا مَحَالَةَ فَلْيَقُلْ: أَحْسِبُ فُلَانًا وَاللَّهُ حَسِيبُهُ وَلَا أُزَكِّي عَلَى اللَّهِ أَحَدًا أَحْسِبُهُ إِنْ كَانَ يَعْلَمُ ذَاكَ كَذَا وَكَذَا))

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Iwapo hakuna budi kwa mtu kumsifu mwenzake basi aseme: 

 

 أَحْسِبُ فُلَانًا وَاللَّهُ حَسِيبُهُ وَلَا أُزَكِّي عَلَى اللَّهِ أَحَدًا أَحْسِبُهُ ...

 

”Namdhania fulani (kwa kadhaa na kadhaa), na Allaah Ndiye Atakayemuhisabu wala simtakasi yeyote kwa Allaah.

 

Lakini namdhania (kadhaa wa kadhaa) ikiwa unajua hivyo (kwamba mtu huyo ana sifa nzuri))[1] 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Bakr (رضي الله عنه) Muslim (4/2296) [3000], Al-Bukhaariy [2662].

 

 

Share