118-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unaposimama Katika Mlima Wa Swafaa Na Wa Marwah
Hiswnul-Muslim
118-Du’aa Unaposimama Katika Mlima Wa Swafaa Na Wa Marwah
[236]
Amesema Jaabir (رضي الله عنه) katika Hadiyth ndefu aliyoielezea Hijah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) kwamba alipokurubia Swafaa alisoma:
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ
Hakika Swafaa na Mar-wah ni katika alama za (Dini ya) Allaah[1]
أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اللهُ بِهِ
Abdau bimaa Badaa-Allaahu bih
Ninaanza kwa alichoanza Allaah
… Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Ka’bah kisha akaielekea na kusema:
اللهُ أكْبَرُ، اللهُ أكْبَرُ، اللهُ أكْبَرُ
Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar
Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa.
… kisha atasema yafuatayo mara tatu akiomba du’aa (yoyote apendayo) baada ya kila mara:
لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu, wa hazamal ahzaaba Wahdah
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na ni Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake.
…Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alisoma hivi mara tatu na baina yake akiomba du’aa, kisha akafanya alipokuwa Marwah kama alivyofanya alipokuwa Swafaa[2]