130-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl Na Takbiyr
Hiswnul-Muslim
130-Fadhila Za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl Na Takbiyr
[254]
َقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ فِي يَوْمٍ مائَةَ مَرَّةٍ، حُطَّتْ خَطَاياهُ وَلَوْ كانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Mwenye kusema:
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ
Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi ni Zake
mara mia kwa siku, atafutiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari))[1]
[255]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((مَنْ قَال: لا إِلهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْد، وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، عَشَرَ مَرَّاتْ كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إسْمَاعِيلَ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema:
لا إِلهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْد، وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr
Hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah peke Yake, hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.
… mara kumi, ni kama (thawabu za mtu) aliyewacha huru nafsi nne katika wana wa Ismaa’iyl))[2]
[256]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي الْمِيزَانِ، حَبِيبَتانِ إلى الرَّحْمنِ سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Rahmani (Mwingi wa Kurehemu) nayo ni:
سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ
Subhaana Allaahi Wabihamdihi Subhaana Allaahil-’Adhwiym
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi ni Zake, Utakasifu ni wa Allaah Aliye Mtukufu[3]
[257]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Kusema kwangu:
سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ
Subhaana Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa.
… ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua))[4]
[258]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَكْسِبَ كُلَّ يَوْمٍ أَلْفَ حَسَنَةٍ؟)) فَسَأَلَهُ سَائِلٌ مِنْ جُلَسَائِهِ: "كَيْفَ يَكْسِبُ أَحَدُنَا أَلْفَ حَسَنَةٍ؟" قَالَ: ((يُسَبِّحُ مِائَةَ تَسْبِيحَةٍ فَيُكْتَبُ لَهُ أَلْفُ حَسَنَةٍ أَوْ يُحَطُّ عَنْهُ أَلْفُ خَطِيئَةٍ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hivi anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku thawabu elfu?)) Mtu mmoja miongoni mwa waliokaa akamuuliza: ”Atachuma vipi mmoja wetu thawabu elfu?” Akamjibu: ((Aseme:
سُبْحَانَ اللهِ
Subhaana-Allaah
Utakasifu ni wa Allaah
… mara mia moja, basi ataandikiwa thawabu elfu moja, au atafutiwa madhambi elfu moja))[5]
[259]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((مَنْ قَال: سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ، غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةً فِي الْجَنَّةِ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakaesema:
سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وبِحَمْدِهِ
Subhaana-Allaahil-’Adhwiym wa bihamdihi
Utakasifu ni wa Allaah Aliye Mtukufu na Himdi ni Zake.
… hupandiwa mtende katika Jannah))[6]
[260]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((يَا عَبْدَ اللَّهِ بْنَ قَيْسٍ، أَلا أَدُلُّكَ عَلَى كَلِمَةٍ مِنْ كَنْزِ الْجَنَّةِ؟)) قَالَ : قُلْتُ: "بَلَى يَا رَسُولُ الله" قَال: (( لا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Ee ’Abdallaahi bin Qays! Hivi nikujulishe hazina miongoni mwa hazina za Jannah?)) Nikamwambia: ”Ndio Ee Rasuli wa Allaah”. Akasema: ((Sema:
لاَ حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ
Laa hawla walaa quwwata illaa BiLLaah
Hakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah[7]
[261]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne:
سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، وَلاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ
Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar,
Utakasifu ni waAllaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.
… si vibaya kuanza kwa lolote katika haya))[8]
[262]
جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى رَسُولِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ عَلِّمْنِي كَلامًا أَقُولُهُ" فَقَالَ: ((قُلْ: لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، وَسُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ)) قَالَ:" هَؤُلاءِ لِرَبِّي فَمَا لِي؟" قَالَ: ((قُلِ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وَارْحَمْنِي، وَاهْدِنِي، وَارْزُقْنِي))
Alikuja mbedui mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akamwambia: ”Nifundishe maneno niyaseme: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akamwambia: ((Sema:
لاَ إِلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبيراَ والْحَمْدُ للهِ كَثيراً، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ العَالَمينَ، لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ العَزيزِ الْحَكِيمِ
Laa ilaaha illa Allaah Wahdau laa shariyka Lah. Allaahu Akbar Kabiyraa, WalhamduliLLaahi kathiyraa, Subhaana-Allaahi Rabbil ’aalamiyn. Laa hawla wa laa quwwata illaa biLLaahil ’Aziyzil-Hakiym
Hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika. Allaah ni Mkubwa tena sana, na Himdi Anastahiki Allaah tena nyingi sana. Utakasiuf ni wa Allaah Rabb wa walimwengu. Hapana uwezo wala nguvu ila ni za Allaah, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima, Mwenye hikmah wa yote daima.
… yule mbedui kisha akasem: ”Haya ni ya Allaah ni yapi yangu?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akamwambia: ((Sema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وارْزُقْنِي
Allaahummagh-fir-liy warhamniy, wahdiniy, warzuqniy
Ee Allaah Nighufurie, na Nirehemu, na Niongoze, na Niruzuku[9]
[263]
كَانَ الرَّجُلُ إِذَا أَسْلَمَ، عَلَّمَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الصَّلَاةَ، ثُمَّ أَمَرَهُ أَنْ يَدْعُوَ بِهَؤُلَاءِ الْكَلِمَاتِ: ((اللهُمَّ اغْفِرْ لِي، وَارْحَمْنِي، وَاهْدِنِي، وَعَافِنِي وَارْزُقْنِي))
Pindi mtu anaposilimu, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akimfundisha kuswali kisha anamuamrisha kuomba kwa matamshi haya:
اللَّهُمَّ اغْفِرِ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وعَافِنِي وارْزُقْنِي
Allaahummagh-fir-liy warhamniy, wahdiniy, wa ’aafiniy, warzuqniy
Ee Allaah Nighufurie, na Nirehemu, na Niongoze, na Nipe afya njema na Niruzuku[10]
[264]
وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((إِنَّ أَفْضَلَ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلَّه، وَأَفْضَلُ الذِّكْرِ: لاَ إلَهَ إِلاَّ الله))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Bora ya du’aa ni mtu kusema:
الْحَمْدُ للهِ
AlhamduliLlaah
Himdi ni za Allaah
na dhikri bora ni:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللهُ
Laa ilaaha illa-Allaah
Hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah[11]
[265]
((الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ: سُبْحَانَ الْلَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا الْلَّهُ، وَالْلَّهُ أَكْبَرُ وَ لاَ حَوٍلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Mema yanayobakia daima ni:
سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ،لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوٍلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ)
Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa-Allaah, wa Allaahu Akbar, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah,
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa a wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa, hapana uwezo wala nguvu isipokuwa ni za Allaah[12]
[1]Hadiyth ya Abu Huraryah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (7/168) [6405], Muslim (4/2071) [2691], na angalia: fadhila zake nyingine ((Atakayesema mara mia asubuhi na jioni…)) katika ‘Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni’ Du’aa Namba 91.
[2]Hadiyth ya Abu Ayyuwb Al-Answaariyy (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (7/67), Muslim (4/2071) kwa tamshi yake na angalia fadhila zake nyingine: “Atakayesema mara mia kwa siku, mara kumi, mara moja” katika ‘Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni’ Du’aa [92, 93]
[3]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (7/168) [3462], Muslim (4/2072) [2694]
[4]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (4/2072) [2695].
[5]Hadiyth ya Sa’iyd bin Abi Waqqaasw (رضي الله عنه) - Muslim (4/2073) [2140]
[6]Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما) At-Tirmidhiy (5/511) [3464, 3465], Al-Haakim (1/501), na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahaby na angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (5/531), na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/160)
[7]Hadiyth ya Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه) (ambaye ndiye ‘Abdullaah bin Qays) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/213) [4205] , Muslim (4/2076) [2704].
[8]Hadiyth ya Samrah bin Jundub (رضي الله عنه) Muslim (3/1685) [[2137]
[9]Hadiyth ya Sa’ad bin Abi Waqqaasw (رضي الله عنه) Muslim (4/2072) [2696] na Abu Daawuwd amezidisha: “Alipogeuka Mbedui, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akasema:
((لَقَدْ مَلأ يَديهِ مِنَ الْخَيْر))
((Hakika mikono yake imejaa kheri)) (1/220) [832].
[10]Hadiyth ya Twaariq bin Ashiym Al-Ashja’iyy (رضي الله عنه) Muslim (4/2073) [2697], na katika riwaayah nyingine:
((فَإنَّ هَؤلآءِ تَجْمَعُ لَكَ دُنْيَاكَ وَآخِرَتك))
((Kwani hayo yanakukusanyia Dunia yako na Akhera yako))
[11]Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) At-Tirmidhiy (5/462) [3383], ibn Maajah (2/1249) [3800], Al-Haakim (1/503) na ameisahihisha na ameiwafiki Adh-Dhahaby na angalia: Swahiyh Al-Jaami (1/362) [1104].
[12]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) Ahmad (3/75) [513] kwa utaratibu wa Ahmad Shaakir na Isnaad yake ni Swahiyh. Na angalia: Majma’ Az-Zawaaid (1/297), na ibn Hajar ameipa nguvu katika Buluwgh Al-Maraam kutoka riwaayah ya Abu Sa’iyd kwa An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm Wal-Layl’ [484] na amesema: Ameisahihisha Al-Haakim (1/512) na Ibn Hibbaan [840].
Tanbihi: Imaam Al-Albaaniy amedhoofisha katika Dhwa’iyf Al-Jaami [828] kwa kuweko tamshi la:
لا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ
Akaisahihisha katika Swahiyh At-Targhiyb [366] yenye kutaja:
لا إلهَ إلَّا اللهُ ، و سُبحانَ اللهِ ، و اللهُ أكبرُ ، و لا حَولَ و لا قُوَّةَ إلَّا بالله
Na pia iliyothibiti nyengineyo ni Hadiyth ifuatayo:
((خُذُوا جُنَّتَكُمْ)) قُلْنَا يَا رَسُولَ اللهِ: مِنْ عَدُوٍّ قَدْ حَضَرَ؟ قَالَ: ((لاَ،جُنَّتَكُمْ مِنَ النَّارِ، قُولُوا : سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، فَإِنَّهَا يَأْتِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مُنْجِيَاتٍ، وَمُقَدَّمَاتٍ ، وَهُنَّ الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jikingeni!)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah; Je adui ameshatufikia? Akasema: ((Hapana bali kinga yenu kutokana na moto. Semeni:
سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ
Subhaana-Allaah, wal-HamduliLLaah, wa laa ilaaha illa-Allaah, wa Allaahu Akbar
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.
Kwani yatakuja zitakuja hizo (Adhkaar) Siku ya Qiyaamah kama ni kinga na kitangulizi, nazo ni Mema yanayobakia daima)) [An-Nasaaiy fiy Sunan Al-Kubraa (10684), Atw-Twabaraniy fiy Al-Mu’jim Al-Awsatw (4027), na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3214), Swahiyh At-Targhiyb (1567), na kwa Riwaayah nyenginezo amesahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (3264), (6/482)]