129-Hiswnul-Muslim: Kuomba Maghfirah Na Kutubia

Hiswnul-Muslim

129-Kuomba Maghfirah Na Kutubia

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[248]

 

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((وَاللَّهِ إِنِّي لأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً ))

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Naapa kwa Allaa! Hakika mimi ninamuomba maghfirah Allaah na ninatubia Kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini))[1]

 

 

 

[249]

وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((يآيَّها النَّاسُ تُوبُوا إلى اللَّهِ، فَإنِّي أَتُوبُ إِلَيْهِ مائَةَ مَرَّةٍ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Enyi watu!  Tubieni kwa Allaah, kwani mimi ninatubia kwake kwa siku mara mia))[2]

 

 

[250]

 

وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ؛ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema:

 

أَسْتَغْفِرُ اللهَ الْعَظِيمَ الَّذِي لَا إِلَهَ إلَّا هُوَ الحَيُّ القَيّوُمُ وأَتُوبُ إِلَيهِ

Astaghfiru-Allaahal-‘Adhwiyma Alladhiy laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuwmu wa atuwbu Ilayhi

 

Namuomba maghfirah kwa Allaah Mtukufu Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, na ninarejea kutubuia Kwake...

 

Allaah Atamghufuria kama ana makosa hata kama ya kukimbia vitani))[3]

 

 

 

[251]

 

وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَقْرَبَ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ الْعَبْدِ فِي جَوْفَ اللَّيْلِ الآَخِرِ، فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ، فَكُنْ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Wakati ambao mja anakuwa karibu na Rabb wake ni nusu ya mwisho wa usiku. Hivyo ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomdhukuru Allaah kwa wakati huo basi kuwa))[4]

 

 

 

[252]

وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أقْرَبُ ما يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ فأكْثِرُوا الدًّعَاءَ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Sehemu ambayo anakuwa mja yuko karibu mno na Rabb wake ni wakati amesujudu, basi zidisheni du’aa wakati huo))[5]

 

 

[253]

وَقَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((‏إِنَّهُلَيُغَانُعَلَى قَلْبِي وَإِنِّي لَأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ فِي الْيَوْمِ مِائَةَ مَرَّةٍ))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Wakati mwingine hutanabahi kufunikwa moyo wangu (kughafilika kumdhukuru Allaah) huwa namuomba Allaah maghfirah mara mia moja kwa siku))[6]

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Huraryrah (رضي الله عنه)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/101) [6307].

 

[2] Muslim (4/2076)

 

[3]Hadiyth ya ibn Mas-‘uwd (رضي الله عنه)  - Abu Daawuwd (2/85) [1517], At-Tirmidhiy (5/569) [3577], Al-Haakim na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahaby (1/511) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله). Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182), na Jaami’ Al-Uswuwl li-Ahaadiyth Ar-Rasuwl صلى الله عليه وسلم [4/389-390] kwa tahqiyq ya Al-Arnaawuwtw.

 

[4]Hadiyth ya Amruw bin ‘Abasah (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy (1/279), Al-Haakim na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/183) na Jaami’ Al-Uswuwl kwa tahqiyq ya Al-Arnaawuwtw (4/144)

 

[5]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  - Muslim (1/350) [482].

 

[6]Hadiyth ya Al-Agharr Al-Muzaniy (رضي الله عنه) - Muslim (4/2075) [2702] Kadhalika angalia: Jaami’ Al-Uswuwl (4/386)

 

 

Share