14-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Manabii Na Rusuli Wote Walifungamana Ahadi Naye Kumwamini
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
14-Manabii Na Rusuli Wote Walifungamana Ahadi Naye Kumwamini
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾
Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah): Akasema Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu? Wakasema: Tumekiri. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia. [Aal-‘Imraan: 81]
Na katika Hadiyth:
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكِتَابٍ أَصَابَهُ مِنْ بَعْضِ أَهْلِ الْكُتُبِ، فَقَرَأَهُ على النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَغَضِبَ وَقَالَ: ((أَمُتَهَوِّكُونَ فِيهَا يَا ابْنَ الْخَطَّابِ؟ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَقَدْ جِئْتُكُمْ بِهَا بَيْضَاءَ نَقِيَّةً، لَا تَسْأَلُوهُمْ عَنْ شَيْءٍ فَيُخْبِرُوكُمْ بِحَقٍّ فَتُكَذِّبُوا بِهِ، أَوْ بِبَاطِلٍ فَتُصَدِّقُوا بِهِ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَوْ أَنَّ مُوسَى كَانَ حَيًّا، مَا وَسِعَهُ إِلَّا أَنْ يَتْبَعَنِي)) رواه أحمد، وحسنه الألباني في إرواء الغليل
Kutoka kwa Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba ‘Umar Ibn Al-Khatw-twaab (رضي الله عنهما) alimwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Maandishi aliyoyapata kutoka kwa Ahlul-Kitaab. Akamsomea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaghadhibika akasema: ((Je unachanganyikiwa (Dini yako) ee ibn Al-Khatw-twaab? Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, nimekujieni na (Risala ya Uislaam) ikiwa ni angavu na safi kabisa. Usiwaulize lolote wasije wakakuambia jambo la kweli nawe ukalikanusha, au wasije kukuambia jambo la uongo nawe ukaliamini. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikoni Mwake, angeliuwa Muwsaa yuko hai, basi asingelikuwa na chaguo isipokuwa kunifuata mimi)) [Imaam Ahmad [14736] na ameipa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaani katika Irwaa Al-Ghaliyl (6/34)]
Pia imethibitika kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) atateremka duniani kabla ya Qiyaamah na atahukumu kwa Dini ya Kiislamu:
عن أبي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمُ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا عَدْلاً، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الْخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الْجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ الْمَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ، حَتَّى تَكُونَ السَّجْدَةُ الْوَاحِدَةُ خَيْرًا مِنَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((وَإِنْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلاَّ لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا))
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu na atavunja misalaba, na kuua nguruwe, na ataondosha jizyah (ushuru kutoka kwa wasio Waislamu ambao wamo katika himaya ya serikali ya Waislamu). Kisha kutakuwa na mali nyingi hadi itafikia kuwa hakuna mtu wa kupokea swadaqh. Wakati huu sijdah moja itakuwa ni bora kwao kuliko maisha haya na yote yaliyomo (katika dunia).” Kisha Abuu Huraryah akasema: Someni mkipenda:
وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾
Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao. (4: 159)[Al-Bukhaariy]
Na pia:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، وَالأَنْبِيَاءُ إِخْوَةٌ لِعَلاَّتٍ، أُمَّهَاتُهُمْ شَتَّى، وَدِينُهُمْ وَاحِدٌ))
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mimi ni awlaa (bora na karibu zaidi) kwa ‘Iysaa mwana wa Maryam dunina na Aakhirah na Manabii wote ni ndugu, mama zao wanatofautiana lakini Dini yao ni moja)) [Al-Bukhaariy]