15-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kitabu Chake (Qur-aan) Kimejumuisha Vitabu Vyote Vya Mbinguni
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
15- Kitabu Chake (Qur-aan) Kimejumuisha Vitabu Vyote Vya Mbinguni
Qur-aan imejumuisha na kusadikisha yote yaliyoteremshwa katika Tawraat, Injiyl na Zaabuwr kama Anavyosema Allaah :(سبحانه وتعالى)
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ
Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake na chenye kudhibiti, kushuhudia na kuhukumu juu yake (hivyo Vitabu). Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah. [Al-Maaidah: 48]
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu:
وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ
Yaani: Kinadhibiti Vitabu viliyo kabla yake.
Na Imaam As-Sa’dy amesema kuhusu
وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ
Yaani: Kinajumuisha yaliyojumuishwa katika Vitabu vya awali.
Na katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ: كَيْفَ تَسْأَلُونَ أَهْلَ الْكِتَابِ عَنْ شَىْءٍ، وَكِتَابُكُمُ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْدَثُ، تَقْرَءُونَهُ مَحْضًا لَمْ يُشَبْ وَقَدْ حَدَّثَكُمْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ بَدَّلُوا كِتَابَ اللَّهِ وَغَيَّرُوهُ وَكَتَبُوا بِأَيْدِيهِمُ الْكِتَابَ وَقَالُوا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً، أَلاَ يَنْهَاكُمْ مَا جَاءَكُمْ مِنَ الْعِلْمِ عَنْ مَسْأَلَتِهِمْ، لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا مِنْهُمْ رَجُلاً يَسْأَلُكُمْ عَنِ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَيْكُمْ.
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kwanini mnawauliza Ahlul-Kitaab jambo lolote ilhali Kitabu chenu ambacho kimeteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kipya (na cha karibuni)? Mnakisoma kikiwa ni kisafi, hakikupotoshwa wala kubadilishwa. Na mmeshajulishwa (na Allaah) kwamba Ahlul-Kitaab wamebadilisha Vitabu vya Allaah na wakavigeuza na wakaandika kwa mikono yao Kitabu wakasema “Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo.’” Je haikuwafikia ilmu kuwakataza msiwaulize lolote? Hapana, wa-Allaahi hatujapata kuona mtu yeyote kutoka kwao anayewauliza nyinyi yale yaliyoteremshwa kwenu.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-I’tiswaam Bil-Kitaabi Was-Sunnah]