Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Unyeyekevu Wake Wa Kutokulalamika Chakula Nyumbani
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hakuwa mwenye makuu katika chakula, akila chochote alichopikiwa bila ya kulalamika:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: مَا رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَابَ طَعَامًا قَطُّ كَانَ إِذَا اشْتَهَاهُ أَكَلَهُ وَإِنْ لَمْ يَشْتَهِهِ سَكَتَ . مسلم
Abuu Huraryrah amesema: “Sijapatapo kamwe kumuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitia dosari chakula. Alikuwa anapokipenda anakila, na asipokipenda ananyamaza.” [Muslim]
Na Riwaayah nyenginezo
“Asipokipenda alikiacha.” [Al-Bukhaariy na wengineo]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
02-Unyeyekevu Wake Alikiri Kuwa Manabii Wengineo Ni Bora Kuliko Yeye
Juu ya kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabiy wa mwisho na ndiye ambaye Allaah (عزّ وجلّ) Amejaalia fadhila nyingi kulikoni Manabii na Rusuli wengineo; mfano yeye ndiye aliyewasalisha Manabii wote alipofika Masjid Al-Aqswaa katika safari ya Al-Israa wal Mi’raaj, lakini hakujiona kuwa yeye ni mbora kuliko wengineo, kwa sababu ya unyenyekevu wake aliwafadhilisha Manabii wengineo kama ilivyokuja katika Hadiyth:
عنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَدْ لُطِمَ وَجْهُهُ وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ إِنَّ رَجُلاً مِنْ أَصْحَابِكَ مِنَ الأَنْصَارِ لَطَمَ وَجْهِي. قَالَ: ((ادْعُوهُ)) فَدَعَوْهُ قَالَ: ((لِمَ لَطَمْتَ وَجْهَهُ)) قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي مَرَرْتُ بِالْيَهُودِ فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ وَالَّذِي اصْطَفَى مُوسَى عَلَى الْبَشَرِ. فَقُلْتُ: وَعَلَى مُحَمَّدٍ، وَأَخَذَتْنِي غَضْبَةٌ فَلَطَمْتُهُ. قَالَ: ((لاَ تُخَيِّرُونِي مِنْ بَيْنِ الأَنْبِيَاءِ، فَإِنَّ النَّاسَ يَصْعَقُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَكُونُ أَوَّلَ مَنْ يُفِيقُ، فَإِذَا أَنَا بِمُوسَى آخِذٌ بِقَائِمَةٍ مِنْ قَوَائِمِ الْعَرْشِ، فَلاَ أَدْرِي أَفَاقَ قَبْلِي أَمْ جُزِيَ بِصَعْقَةِ الطُّورِ))
Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia: Alikuja Myahudi mmoja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alipigwa kibao usoni akasema: “Ee Muhammad! Mmoja kati ya Maswahaba zako wa ki-Answaariy amenipiga kibao!” Akasema: ((Mwiteni!)). Akaitwa akamuuliza: (Kwanini umempiga kibao usoni?)) Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, mimi nilipita kwa Myahudi nikamsikia Anasema: Naapa kwa Ambaye Amechagua Muwsaa kuliko walimwengu wote.” Nikamwambia: “Bali Muhammad (kuliko wote).” Basi nikaghadhibika nikampiga kibao usoni.” Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Msinifadhilishe juu ya Manabii wengineo, kwani hakika Siku ya Qiyaamah watu watazimia na nitakuwa mimi ni wa kwanza kupata fahamu. Kisha nitamuona Muwsaa akikamata nguzo moja ya ‘Arsh. Sitojua kama kama alipata fahamu kabla yangu au ni mshtuko ulimtosheleza alioupata katika Mlima (alipomuomba Allaah amtazame alipokuwa hai)) [Al-Bukhaari]
Na akamfadhilisha Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) katika Hadiyth:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا خَيْرَ الْبَرِيَّةِ! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ذَاكَ إِبْرَاهِيمُ عَلَيْهِ السَّلَام)) مسلم
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Ee kiumbe bora kabisa!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: “Huyo ni Ibraahiym ((عليه السلام [Muslim]
Na akamfadhilisha Nabiy Yuwnus (عليه السلام) katika Hadiyth:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((؟مَا يَنْبَغِى لِعَبْدٍ أَنْ يَقُولَ أَنَا خَيْرٌ مِنْ يُونُسَ بْنِ مَتَّى عَلَيْهِ السَّلاَمُ))
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Haipasi mja yeyote aseme kuwa mimi ni mbora kuliko Yuwnus ibn Mattaaعليه السلام (( [Al-Bukhaariy]
Na akamfadhilisha Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) :
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قِيلَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم: مَنْ أَكْرَمُ النَّاسِ قَالَ: ((أَكْرَمُهُمْ أَتْقَاهُمْ)) قَالُوا يَا نَبِيَّ اللَّهِ، لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ. قَالَ: ((فَأَكْرَمُ النَّاسِ يُوسُفُ نَبِيُّ اللَّهِ ابْنُ نَبِيِّ اللَّهِ ابْنِ نَبِيِّ اللَّهِ ابْنِ خَلِيلِ اللَّهِ)) قَالُوا لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ. قَالَ: ((فَعَنْ مَعَادِنِ الْعَرَبِ تَسْأَلُونِي)) قَالُوا نَعَمْ. قَالَ: ((فَخِيَارُكُمْ فِي الْجَاهِلِيَّةِ خِيَارُكُمْ فِي الإِسْلاَمِ إِذَا فَقِهُوا)) البخاري
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia: Watu walimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Nani aliye mtukufu zaidi kati ya watu?” Akasema: ((Aliye mtukufu zaidi ni ambaye mwenye taqwa zaidi)). Wakasema: “Ee Nabiy wa Allaah, hatukuulizi kuhusu hivyo!” Akasema: ((Basi aliye mtukufu zaidi kati ya watu ni Yuwsuf ambaye ni Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Khaliyl wa Allaah)). Wakasema: “Hatukuulizi kuhusu hivyo!” Akasema: ((Basi hivyo mnataka kuniuliza kuhusu majadi wa Kiarabu?)) Wakasema: “Naam.” Akasema: ((Wale waliokuwa wabora kabisa katika Ujaahiliyyah (kabla ya Uislaam) ndio wabora kabisa katika Uislaam, ikiwa watakuwa na ufahamu wa kina (wa Dini yao)) [Al-Bukhaariy]
Faida: Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) ni mwana wa Nabiy Ya’quwb (عليه السلام) mwana wa Nabiy Is-haaq (عليه السلام) mwana wa Nabiy Ibraahiym (عليه السلام).
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
03-Unyenyekevu Wake: Akifanya Kazi Za Nyumbani Kwake Na Kuwahudumia Ahli Wake
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisaidia kazi za nyumba kama kufagia na usafi mwingine wa nyumba na akijihudumia mwenyewe na kuwahudumia ahli wake, kwa dalili zifuatazo:
عَنِ الأَسْوَدِ، قَالَ سَأَلْتُ عَائِشَةَ مَا كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ فِي بَيْتِهِ قَالَتْ كَانَ يَكُونُ فِي مِهْنَةِ أَهْلِهِ ـ تَعْنِي خِدْمَةَ أَهْلِهِ ـ فَإِذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ خَرَجَ إِلَى الصَّلاَةِ.
Kutoka kwa Al-Aswad ambaye amesema: Nilimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها): Je, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya nini nyumbani kwake? Akajibu: “Alikuwa akijishughulisha kuwahudumia ahli wake, na inaponadiwa Swalaah hutoka kwenda kuswali.” [Al-Bukhaariy na wengineo]
Pia:
عن عائشةَ قالت : سأَلها رجُلٌ : هل كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يعمَلُ في بيتِه ؟ قالت : نَعم كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يخصِفُ نعلَه ويَخيطُ ثوبَه ويعمَلُ في بيتِه كما يعمَلُ أحَدُكم في بيتِه
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Mtu mmoja alimuuliza: Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kazi nyumbani kwake? Akajibu: “Naam. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitengeneza viatu vyake na akishona viraka vya nguo zake na akifanya kazi kama afanyavyo kazi mmoja wenu nyumbani mwake.” [Ahmad, Adab Al-Mufrad, Ibn Hibban na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Takhriyj Mishkaat Al-Maswaabiyh [5759]
Pia:
وقد سئلت عَائِشَة رضي الله عنها : " مَا كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعْمَلُ فِي بَيْتِهِ؟ فقَالَتْ: كَانَ بَشَرًا مِنَ الْبَشَرِ يَفْلِي ثَوْبَهُ ، وَيَحْلُبُ شَاتَهُ، وَيَخْدُمُ نَفْسَهُ .
رواه أحمد (26194) ، وصححه الألباني في "الصحيحة(671) .
Aliulizwa ‘Aaishah (رضي الله عنها): Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kazi nyumbani kwake? Akajibu: Yeye ni bin Aadam kama walivyo wana Aadam, wengineo; alikuwa akisafisha nguo zake, akikamua maziwa mbuzi wake, na akijihudumia mwenyewe.” [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah [671]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
04-Unyenyekevu Wake Akiwasalimia Watoto Na Kuwapapasa Vichwa Vyao
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mwenye mapenzi na huruma mpaka kwa watoto wake na wasio wake:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ مَا رَأَيْتُ أَحَدًا كَانَ أَرْحَمَ بِالْعِيَالِ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ كَانَ إِبْرَاهِيمُ مُسْتَرْضِعًا لَهُ فِي عَوَالِي الْمَدِينَةِ فَكَانَ يَنْطَلِقُ وَنَحْنُ مَعَهُ فَيَدْخُلُ الْبَيْتَ وَإِنَّهُ لَيُدَّخَنُ وَكَانَ ظِئْرُهُ قَيْنًا فَيَأْخُذُهُ فَيُقَبِّلُهُ ثُمَّ يَرْجِعُ .
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Sijapatapo kuona mtu mwenye huruma zaidi na familia yake kama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema: Ibrahiym (mwanawe Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam( alikuwa akinyonyeshwa na familia moja ya Madiynah. Alipokuwa anapowatembelea nasi tulikuwa pamoja naye, huingia katika nyumba iliyojaa moshi kwa vile baba yake (Ibraahiym) wa kambo alikuwa ni mhunzi wa chuma. Basi alimbeba Ibraahiym akambusu kisha akimrudisha. [Muslim]
Pia,
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضى الله عنه أَنَّهُ مَرَّ عَلَى صِبْيَانٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ وَقَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَفْعَلُهُ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliwapitia Watoto akawasalimia kisha akasema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo: [Al-Bukhaari]
Pia,
عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : " كَانَ يَزُورُ الأَنْصَارَ وَيُسَلِّمُ عَلَى صِبْيَانِهِمْ ، وَيَمْسَحُ بِرُءُوسِهِمْ "
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwatembelea kina Answaariy na akiwasalimia watoto wao na akiwapapasa vichwa vyao. [Ibn Maajah, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (459), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/149)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
05-Unyeyekevu Wake: Akikaa Na Maswahaba Kuongea Nao
عن أنس بن مالك رضي الله عنه يَقُولُ إِنْ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لَيُخَالِطُنَا حَتَّى يَقُولَ لأَخٍ لِي صَغِيرٍ" يَا أَبَا عُمَيْرٍ مَا فَعَلَ النُّغَيْرُ ".
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akichanganyika na sisi mno hadi kwamba alikuwa akimwambia mmoja kati ya aliye mdogo kwetu: ((Ee Abaa ‘Umayr, An-Nu’ayr (aina ya ndege mdogo) amefanya nini?)) [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عَنْ أَبِي ذَرٍّ، وَأَبِي، هُرَيْرَةَ قَالاَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَجْلِسُ بَيْنَ ظَهْرَىْ أَصْحَابِهِ فَيَجِيءُ الْغَرِيبُ فَلاَ يَدْرِي أَيُّهُمْ هُوَ حَتَّى يَسْأَلَ فَطَلَبْنَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ نَجْعَلَ لَهُ مَجْلِسًا يَعْرِفُهُ الْغَرِيبُ إِذَا أَتَاهُ - قَالَ - فَبَنَيْنَا لَهُ دُكَّانًا مِنْ طِينٍ فَجَلَسَ عَلَيْهِ وَكُنَّا نَجْلِسُ بِجَنْبَتَيْهِ وَذَكَرَ نَحْوَ هَذَا الْخَبَرِ فَأَقْبَلَ رَجُلٌ فَذَكَرَ هَيْئَتَهُ حَتَّى سَلَّمَ مِنْ طَرْفِ السِّمَاطِ فَقَالَ السَّلاَمُ عَلَيْكَ يَا مُحَمَّدُ. قَالَ فَرَدَّ عَلَيْهِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم.
Abuu Dharr na Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiketi pamoja na Maswahaba wake. Basi pindi anapokua mtu mgeni huwa hamtambui mpaka pindi anapomuulizia. Kisha tukamuomba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tumfanyie kibaraza cha kukalia ili pindi anapokuja mtu mgeni aweze kumtambua. Tukamjengea kibaraza cha udongo ili akikalie, nasi huwa tunaketi pembeni yake. Akataja maelezo kama haya kwamba mtu mmoja, na akataja muonekano wake; (Huyo mtu mgeni) alimkabili (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamsalimia pembeni mwa ukumbi akasema:
“Assalaamu ‘alayka Yaa Muhammad.” Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu (maamkizi yake).” [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (4698)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
06-Unyenyekevu Wake: Hakujiona Yeye Ni Bora Kuliko Maswahaba Wake
عن أنس بن مالك رضي الله عنه أنَّ رجلًا قال: يا محمدُ: أيا سيَّدَنا وابنَ سيِّدِنا! وخيرَنا وابنَ خيرِنا! فقال رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ: ((يا أيها الناسُ عليكم بتقواكم، ولا يستهوينَّكم الشيطانُ، أنا محمدُ بنُ عبدِ اللهِ، أنا عبدُ اللهِ ورسولِه، ما أحبُّ أن ترفعوني فوقَ منزلَتي التي أنزلَنيها اللهُ))
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja aliita: “Ee Muhammad! Ee Bwana wetu, mwana wa Bwana wetu! Mbora wetu, mwana wa mbora wetu!” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Enyi watu! Shikameni na taqwa yenu! Msimwache shaytwaan akuchezeeni! Mimi ni Muhammad bin ‘Abdillaah, mja wa Allaah na Rasuli Wake. Sipendi mnipandishe zaidi ya daraja ambayo Ameniteremshia Allaah)) [Ahmad, An-Nasaaiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/101)]
Na pia:
عنْ أَبِي مَسْعُودٍ، قَالَ أَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ـ رَجُلٌ فَكَلَّمَهُ فَجَعَلَ تُرْعَدُ فَرَائِصُهُ فَقَالَ لَهُ: ((هَوِّنْ عَلَيْكَ فَإِنِّي لَسْتُ بِمَلِكٍ إِنَّمَا أَنَا ابْنُ امْرَأَةٍ تَأْكُلُ الْقَدِيدَ))
Kutoka kwa Abuu Mas‘uwd amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamsemesha basi akawa anatetemeka kwa sababu ya kumwogopa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Jitulize, kwani mimi si mfalme, hakika mimi ni mwana ambaye mama yake alikula nyama kavu)) [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (2693)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
07-Unyenyekevu Wake: Aliitikia Mwaliko Na Kupokea Zawadi Hata Kama Ni Duni
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَوْ دُعِيتُ إِلَى ذِرَاعٍ أَوْ كُرَاعٍ لأَجَبْتُ، وَلَوْ أُهْدِيَ إِلَىَّ ذِرَاعٌ أَوْ كُرَاعٌ لَقَبِلْتُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kama nitaalikwa mwaliko wa makongoro ya kondoo nitaitikia na nitapokea zawadi hata kama ni mkono au makongoro ya kondoo)) [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
08-Alikataa Kutukuzwa Mno Kama Walivyotukuzwa Manabii Wa Awali
Mojawapo wa sifa ya unyenyekevu wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwamba hakupenda atukuzuwe kama walivyotukuzwa Manabii wa awali, na juu ya hivyo kumtukuza mno kupindukia mipaka ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), naye alikhofia hilo:
عن ابنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما سَمِعَ عُمَرَ رضي الله عنه يَقُولُ عَلَى المِنْبَرِ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ
Kutoka kwa ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kamsikia ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika minbari akisema: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
09-Unyenyekevu Wake Akipanda Punda Na Akiitikia Mwaliko Wa Mtumwa
عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنْتُ رَدِيفَ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى حِمَارٍ فَقَالَ لِي: ((يَا مُعَاذُ؟ أَتَدْرِي مَا حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ، وَمَا حَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ؟)) قُلْتُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: ((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اَللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ اَلنَّاسَ؟ قَالَ: ((لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا)) أَخْرَجَاهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ
Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya punda akasema: ((Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah juu ya waja Wake, na nini haki ya waja juu ya Allaah?)) Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: ((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niwabashirie watu? Akasema: ((Usiwabashirie wasije kuitegemea)) [wakaacha kufanya juhudi katika ‘ibaadah])) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia:
عن أنس بن مالك ان النبي صلى الله عليه وسلم كان يُرْدِفُ خلْفَهُ ، ويضعُ طعامَهُ على الأرضِ ، ويُجِيبُ دعوةَ المملوكِ ، ويركَبُ الحمارَ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimpandisha nyuma yake (kwenye kipando) na akiweka chakula chake ardhini na akiitikia mwaliko wa mtumwa na akipanda punda. [Swahiyh Al-Jaami’ (4945)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
10-Unyenyekevu Wake Aliwabashiria Masikini Jannah
عَنْ حَارِثَةَ بْنِ وَهْبٍ الْخُزَاعِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ الْجَنَّةِ، كُلُّ ضَعِيفٍ مُتَضَاعِفٍ، لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اللَّهِ لأَبَرَّهُ، أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ النَّارِ كُلُّ عُتُلٍّ جَوَّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ".
Kutoka kwa Haarithah bin Wahbi Al-Khuzaa’iyy kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, nikujulisheni watu wa Jannah? Ni kila aliye dhaifu na duni na anapochukua kiapo kwa Allaah kuwa atafanya jambo, Allaah Humtimiza kiapo chake. Je, nikujulisheni watu wa Motoni? Ni kila jeuri muonevu, mwenye kujinata na kutakabari. [Al-Bukhaariy]
Na pia:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((احْتَجَّتْ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَقَالَتْ النَّارُ: فِيَّ الْجَبَّارُونَ وَالْمُتَكَبِّرُونَ. وَقَالَتْ الْجَنَّةُ: فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ: فَقَضَى الله بَيْنَهُمَا: إِنَّكِ الْجَنَّةُ رَحْمَتِي أَرْحَمُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ. وَإِنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ. وَلِكِلَاكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jannah na moto zilihojiana. Moto ukasema: Kwangu kunapatikana watu majabari na wenye kiburi. Jannah ikasema: Kwangu kunapatikana watu madhaifu na masikini wao. Allaah Akahukumu baina yao (Akisema): Wewe Jannah ni Rahma Yangu, Nitamrehemu kwa sababu yako Nimtakaye. Na wewe moto ni adhabu Yangu, Nitamwadhibu Nimtakaye kwa sababu yako, na nyote Nitawajaza)). [Muslim]
Na pia,
(Wataingia Jannah Waislamu masikini kabla ya matajiri wao kwa nusu siku ambayo ni miaka 500)). [Swahiyh At-Tirmidhiy, Al-Albaaniy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
11-Unyenyekevu Wake Alikuwa Akitembelea Masikini
Akizuru Wagonjwa Wao Na Akihudhuria Maziko Yao
عن سهل بن حنيف ان النبي صلى الله عليه سلم كان يأتي ضُعفاءَ المسلِمينَ، ويزورُهمْ، ويعودُ مرضاهمْ، ويشهَدُ جنائزَهم
Kutoka kwa Sahl bin Haniyf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akienda kwa Waislamu walio duni na akiwatembelea na akitembelea wagonjwa wao na akihudhuria maziko yao.” [Al-Haakim na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (4877)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
12-Unyenyekevu Wake Akiwahudumia Wajakazi Na Kuwatimizia Haja Zao
www.alhidaaya.com [16]
عن انس بن مالك قَالَ : كَانَتِ الأَمَةُ مِنْ إِمَاءِ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَتَأْخُذُ بِيَدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَتَنْطَلِقُ بِهِ حَيْثُ شَاءَتْ.
Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mjakazi katika wakaazi wa Madiynah alikuwa akikamata mkono Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha humpeleka atakako.” [Al-Bukhaariy]
Riwaayah ya Ibn Maajah imesema kuwa mpaka amtimizie haja zake:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ إِنْ كَانَتِ الأَمَةُ مِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَتَأْخُذُ بِيَدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَمَا يَنْزِعُ يَدَهُ مِنْ يَدِهَا حَتَّى تَذْهَبَ بِهِ حَيْثُ شَاءَتْ مِنَ الْمَدِينَةِ فِي حَاجَتِهَا .
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba pindi Mjakazi katika wakaazi wa Madiynah akitaka kukamata mkono Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi hakuwa akikataa kuondosha mkono wake, mpaka ampeleke atakapo Madiynah ili amtimizie haja zake.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3386)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
13-Akiomba Kuishi Umasikini Na Kufishwa Pamoja Na Masikini
Na Akinasihi Kuwa Karibu Nao
عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مِسْكِينًا وَأَمِتْنِي مِسْكِينًا وَاحْشُرْنِي فِي زُمْرَةِ الْمَسَاكِينِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ " . فَقَالَتْ عَائِشَةُ لِمَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ " إِنَّهُمْ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ قَبْلَ أَغْنِيَائِهِمْ بِأَرْبَعِينَ خَرِيفًا يَا عَائِشَةُ لاَ تَرُدِّي الْمِسْكِينَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ يَا عَائِشَةُ أَحِبِّي الْمَسَاكِينَ وَقَرِّبِيهِمْ فَإِنَّ اللَّهَ يُقَرِّبُكِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ "
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameomba: ((Ee Allaah Nijaalia uhai wa umaskini na nifishe nikiwa maskini na nifufue pamoja na kundi la masaakini Siku ya Qiyaamah)). ‘Aaishah akasema: “Kwa nini ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: ((Hakika wao wataingia Jannah kabla ya matajiri kwa miaka arubaini. Ee ‘Aaishah usimrudishe maskini (bila kumpa kitu, umpe) hata kipande cha tende. Ee ‘Aaishah kurubiana nao kwani Allaah Atakukurubisha Siku ya Qiyaamah)) [At-Tirmidhiy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
14-Unyenyekevu Wake: Hakukataa Kuhudumiwa Na Watumwa
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا صَلَّى الْغَدَاةَ جَاءَ خَدَمُ الْمَدِينَةِ بِآنِيَتِهِمْ فِيهَا الْمَاءُ فَمَا يُؤْتَى بِإِنَاءٍ إِلاَّ غَمَسَ يَدَهُ فِيهَا فَرُبَّمَا جَاءُوهُ فِي الْغَدَاةِ الْبَارِدَةِ فَيَغْمِسُ يَدَهُ فِيهَا .
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza kuswali Alfajiri, watumwa wa Madiynah walikuja na vyombo vyao vya maji, basi hakimfikii chombo (cha maji) ila alitumbukiza mikono yake. Na mara nyengine huja asubuhi ya ubaridi mno (hata hivyo hakukataa kwa kupuuza ombi lao ila) alitumbukiza mkono wake.” [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
15-Unyenyekevu Wake Aliwafunza Maswahaba Wawe Unyenyekevu
Ili Wasifanyiane Ufidhuli Au Kujifakharisha
وَعَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ رضى الله عنه - قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِنَّ اَللَّهَ أَوْحَى إِلَيَّ أَنْ تَوَاضَعُوا, حَتَّى لَا يَبْغِيَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ, وَلَا يَفْخَرَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ .
‘Iyaadhw bin Himaar amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameniteremshia Wahyi kwamba (Nyinyi) muwe wanyenyekevu ili msifanyianeni ufidhuli, wala msijifakharishe baina yenu)). [Muslim na wengineo]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
16-Unyenyekevu Wake:
Akiwafundisha Maswahaba Fadhila Za Unyenyekevu Kuwa Unapandisha Daraja
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إلاَّ عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kutoa sadaka hakupunguzi mali, Allaah Humzidishia mja ‘izzah (hadhi) kwa ajili ya kusamehe kwake. Na yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah Aliyetukuka Atampandisha Daraja [Atamtukuza]. [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
17-Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Maswahaba
Kama Kuwamiminia Maji Ya Kunywa
Hadiyth ndefu ya Abuu Qataadah kuhusu kisa cha kupitiwa kwao na usingizi Alfajiri …..
قَالَ: فَانْتَهَيْنَا إِلَى النَّاسِ حِينَ امْتَدَّ النَّهَارُ وَحَمِيَ كُلُّ شَىْءٍ وَهُمْ يَقُولُونَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ: هَلَكْنَا عَطِشْنَا . فَقَالَ: "لاَ هُلْكَ عَلَيْكُمْ" . ثُمَّ قَالَ: "أَطْلِقُوا لِي غُمَرِي" . قَالَ: وَدَعَا بِالْمِيضَأَةِ فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَبُو قَتَادَةَ يَسْقِيهِمْ فَلَمْ يَعْدُ أَنْ رَأَى النَّاسُ مَاءً فِي الْمِيضَأَةِ تَكَابُّوا عَلَيْهَا . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: "أَحْسِنُوا الْمَلأَ كُلُّكُمْ سَيَرْوَى". قَالَ: فَفَعَلُوا فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَسْقِيهِمْ حَتَّى مَا بَقِيَ غَيْرِي وَغَيْرُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم – قَالَ: ثُمَّ صَبَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي: "اشْرَبْ ". فَقُلْتُ: لاَ أَشْرَبُ حَتَّى تَشْرَبَ يَا رَسُولَ اللَّهِ: قَالَ: "إِنَّ سَاقِيَ الْقَوْمِ آخِرُهُمْ شُرْبًا" . قَالَ: فَشَرِبْتُ وَشَرِبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: فَأَتَى النَّاسُ الْمَاءَ جَامِّينَ رِوَاءً
…(Abuu Qaatadah) akasema: “Basi tukaendelea mpaka tukawafikia watu (tulioawaacha nyuma), na mchana ukawa umetanda na kila kitu kilishika joto nao (Maswahaba) wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tumeangamia! Tumebanwa na kiu!” Akasema: ((Hamtaangamia)) Kisha akasema: ((Nipeni kikombe kodogo changu)). Kisha akaomba aletewe jagi la maji. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kumimina maji (katika kikombe kidogo) na Abuu Qaatadah akawa anawanyeshwa maji. Watu walipoona kuwa kuna maji (kidogo) katika jagi, wakalielemea. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Tulieni! Maji yatakutosheni!)). Kisha (Maswahaba) wakaanza kupata (mgao wao) wa maji kwa utulivu (bila ya kudhihirisha kutapatapa) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kujaza (kifuniko) nami nikaanza kuwamiminia (maji) mpaka ikawa hakuna aliyebakia isipokuwa mimi na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha akajaza (kikombe) maji na akaniambia: ((Kunywa!)) Nikamwambia: “Sitokunywa mpaka unywe wewe Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Anayewamiminia watu hanywi mpaka wa mwisho wao amalize kunywa)). Nikanywa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanywa pia na watu wakafikia mahali pa maji wakiwa wanafuraha na kuridhika... [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
18-Unyeyekevu Wake Hakuwa Mwenye Kiburi Bali Amekataza Kutakabari
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ كَانَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ كِبْر)) قَالَ رَجُلٌ: إِنَّ الرَّجُلَ يُحِبُّ أَنْ يَكُونَ ثَوْبُهُ حَسَنًا وَنَعْلُهُ حَسَنَةً. قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ جَمِيلٌ يُحِبُّ الْجَمَالَ، الْكِبْرُ بَطَرُ الْحَقِّ وَغَمْطُ النَّاسِ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoingia Jannah ambaye moyoni mwake mna kiburi uzito wa chembe (au sisimizi)). Mtu mmoja akauliza: “Mtu hupenda nguo yake iwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri [itakuwaje?]” Akasema: ((Hakika Allaah ni Mzuri Anapenda Uzuri. Kiburi ni kukataa haki na kudharau watu)). [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
19-Unyenyekevu Wake Akinyenyekea Kwa Ahli Zake
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَ " خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِي " رواه الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
20-Unyenyekevu Wake Akimhudumia Yeyote Aliyemuomba Njiani
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ أَنَّ امْرَأَةً لَقِيَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ لِي إِلَيْكَ حَاجَةً؟ قَالَ: يَا أُمَّ فُلَانٍ اجْلِسِي فِي أَيِّ نَوَاحِي السِّكَكِ شِئْتِ أَجْلِسْ إِلَيْكِ، قَالَ: فَقَعَدَتْ فَقَعَدَ إِلَيْهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى قَضَتْ حَاجَتَهَا
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kwamba mwanamke mmoja alikutana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika njia mojawapo ya Madiynah akasema: Ee Rasuli wa Allaah, hakika mimi nnakuhitaji jambo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akasema: “Ee Ummu fulani, kaa kitako upande wowote ule wa njia nami nitakaa pamoja nawe.” Anas akasema: Akakaa kitakao, naye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akakaa kitako (akamsikiliza) hadi akamtimizia haja yake.” [Abuu Daawuwd, ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Abiy Daawuwd (4818), Swahiyh Al-Jaami’ (7857)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
21-Unyenyekevu Wake Akila Na Kuketi Kama Wanavyokula Na Kuketi Maswahaba
عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ
Kutoka kwa Yahya bin Abi Kathiyr kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi nakula kama anavyokula mja na nakaa kitako kama anavyokaa mja, kwani hakika mim ni mja.” [Al-Bayhaqiy na ameisahihisha Al-Albaaniy As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]
Katika Riwaayah nyengine:
حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ، يَقُولُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُؤْتَى بِطَعَامٍ، فَيَأْمُرُ بِهِ فَيُوضَعُ عَلَى الْأَرْضِ، ثُمَّ يَقُولُ: "إِنِّي إِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ، آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ" ، وَأَحْسَبُهُ قَالَ: وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُز" رواه البيهقي
Jariyr ibn Haazim amehadithia kwamba: Nilimsikia Al-Hasan akisema: Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa analetewa chakula huamrisha kiwekwe huwekwa chini kisha husema: “Hakika mimi ni mja, nakula kama mnavyokula.” Na nadhani pia amesema: “Na nakaa kitako kama mnavyokaa kitako.”
[Al-Bayhaqiy, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
22-Unyenyekevu Wake Akimpandisha Kwanza Swahaba Wake Kabla Yake Katika Kipando
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جَعْفَرٍ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ تُلُقِّيَ بِصِبْيَانِ أَهْلِ بَيْتِهِ قَالَ: وَإِنَّهُ قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ فَسُبِقَ بِي إِلَيْهِ فَحَمَلَنِي بَيْنَ يَدَيْهِ ثُمَّ جِيءَ بِأَحَدِ ابْنَيْ فَاطِمَةَ فَأَرْدَفَهُ خَلْفَهُ قَالَ: فَأُدْخِلْنَا الْمَدِينَةَ ثَلَاثَةً عَلَى دَابَّةٍ
‘Abdullaah bin Ja’far (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pindi anaporudi safarini, watoto katika ahli yake walikuwa wakija kumpokea na kumkaribisha. Safari moja ikawa katika hali kama hii, pindi aliporudi safarini ikawa nimemwendea mimi kwanza kabla ya mtu mwengine. Akanipandisha (katika mnyama) mimi kabla yake. Kisha akaja mmojawapo wa watoto wawili wa Faatwimah akampandisha nyuma yake ikawa hivi ndivyo sisi watatu tulivyoingia Madiynah huku tumepanda mnayma.” [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
23-Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Swahaba Zake
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakujiona kuwa ni mtu bora kuliko Swahaba juu ya kuwa yeye ni Rasuli wa Allaah, hivyo alikuwa haamui jambo peke yake bila ya kuchukua ushauri kwa Swahaba zake. Ameitikia amri ya Rabb Wake pindi Alipomuamrisha afanye hivyo kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]
Hivyo alipokea ushauri kadhaa kutoka kwa Swahaba zake kama ifuatavyo:
عَنِ الْمِسْوَرِ بْنِ مَخْرَمَةَ، وَمَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، يَزِيدُ أَحَدُهُمَا عَلَى صَاحِبِهِ قَالاَ خَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَامَ الْحُدَيْبِيَةِ فِي بِضْعَ عَشْرَةَ مِائَةً مِنْ أَصْحَابِهِ، فَلَمَّا أَتَى ذَا الْحُلَيْفَةِ قَلَّدَ الْهَدْىَ، وَأَشْعَرَهُ، وَأَحْرَمَ مِنْهَا بِعُمْرَةٍ، وَبَعَثَ عَيْنًا لَهُ مِنْ خُزَاعَةَ، وَسَارَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى كَانَ بِغَدِيرِ الأَشْطَاطِ، أَتَاهُ عَيْنُهُ قَالَ إِنَّ قُرَيْشًا جَمَعُوا لَكَ جُمُوعًا، وَقَدْ جَمَعُوا لَكَ الأَحَابِيشَ، وَهُمْ مُقَاتِلُوكَ وَصَادُّوكَ عَنِ الْبَيْتِ وَمَانِعُوكَ. فَقَالَ " أَشِيرُوا أَيُّهَا النَّاسُ عَلَىَّ، أَتَرَوْنَ أَنْ أَمِيلَ إِلَى عِيَالِهِمْ وَذَرَارِيِّ هَؤُلاَءِ الَّذِينَ يُرِيدُونَ أَنْ يَصُدُّونَا عَنِ الْبَيْتِ، فَإِنْ يَأْتُونَا كَانَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ قَدْ قَطَعَ عَيْنًا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَإِلاَّ تَرَكْنَاهُمْ مَحْرُوبِينَ ". قَالَ أَبُو بَكْرٍ يَا رَسُولَ اللَّهِ، خَرَجْتَ عَامِدًا لِهَذَا الْبَيْتِ، لاَ تُرِيدُ قَتْلَ أَحَدٍ وَلاَ حَرْبَ أَحَدٍ، فَتَوَجَّهْ لَهُ، فَمَنْ صَدَّنَا عَنْهُ قَاتَلْنَاهُ. قَالَ " امْضُوا عَلَى اسْمِ اللَّهِ ".
Al-Miswaar bin Makhramah na Marwaan bin Hakam (رضي الله عنهما) Wamesema, (mmoja wao kasema zaidi kulikoni swahibu yake) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mwaka wa Al-Hudaybiyah pamoja na Swahaba wapatao elfu moja. Walipofika Dhul-Hulayfah akamtia kigwe[1] Hady wake (mnyama wa kuchinja kwa ajili ya Hajj), akaingia hapo Ihraam kwa ajili ya ‘Umrah kisha akamtuma mpelelezi kutoka kabila la Khuzaa’ah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea mpaka akafika (kijiji cha) Ghaadiyr Al-Ashtwaatw. Akamjia mpelelezi wake akasema: “Hakika Maquraysh wamejumuika mjumuiko mkubwa dhidi yako na wamekusanya Wahabashia wawe dhidi yako na watapigana nawe na watakuzuia kuingia Al-Ka’bah.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akasema: “Nishaurini enyi watu! Je, mnanishauri niangamize ahli zao na vizazi vyao hao watu wanaotaka kutuzia kuingia Al-Ka’bah? Kwani wakitujia kwa (amani) basi Allaah (عزّ وجلّ) Ataangamiza jasusi wa makafiri, laa sivyo tutawaacha katika hali mbaya wakiwa wamesulibiwa.” Abuu Bakr akasema? “Ee Rasuli wa Allaah, umetoka ukiwa na niyyah ya kuzuru Nyumba (Ka’bah) na hutaki kuua mtu wala kupigana vita na mtu. Basi endelea kuiendea (Ka’bah) na yeyote atakayetuzuia kuingia humo tutapigana nao.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Endeleeni kwa Jina la Allaah.” [Al-Bukhaariy]
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَشِيرُوا عَلَىَّ فِي الْكَعْبَةِ أَنْقُضُهَا ثُمَّ أَبْنِي بِنَاءَهَا أَوْ أُصْلِحُ مَا وَهَى مِنْهَا؟ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فَإِنِّي قَدْ فُرِقَ لِي رَأْىٌ فِيهَا أَرَى أَنْ تُصْلِحَ مَا وَهَى مِنْهَا وَتَدَعَ بَيْتًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهِ وَأَحْجَارًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهَا وَبُعِثَ عَلَيْهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم
“Enyi watu! Nishaurini kuhusu Nyumba (Ka’bah). Je, niivunje kisha kuijenga upya kuanzia msingi wake au nitengeneze kilichoharibiwa?” Ibn ‘Abbaas akasema: “Imenijia rai kwamba nnavyoona sawa, ni utengeneze tu (sehemu) ziloharibika na uiache Nyumba (Ka’bah) katika hali yake ile ile pindi watu walipoingia Uislamu (na uache) mawe (katika hali yake ile ile) pindi watu walipoingia Uislamu na katika hali ile ile ulipotumwa (na Allaah) kuja kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). [Hadiyth ya ‘Atwaa ameirekodi Imaam Muslim]
[1] Kama kidani cha chuma kwa ajili ya alama kujulikana kuwa ni mnyama wa Hady yaani kuchinjwa katika Hajj.
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
24-Unyenyekevu Wake Akichukia Kusimamiwa
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ، قَالَ لَمْ يَكُنْ شَخْصٌ أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ وَكَانُوا إِذَا رَأَوْهُ لَمْ يَقُومُوا لِمَا يَعْلَمُونَ مِنْ كَرَاهِيَتِهِ لِذَلِكَ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: “Hakuweko mtu aliyekuwa kipenzi zaidi kwao kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Akasema: Lakini hawakuwa wakimsimamia pindi wanapomuona kwa sababu walijua jinsi gani alivyokuwa akichukia hivyo (kusimamiwa). [Adab Al-Mufrad, At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy – Swahiyh At-Tirmidhiy (2754),
Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah (حمه الله) amesema: “Maswahaba (رضي الله عنهم) hawakuwa wakimsimamia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa vile walijua kuchukiwa kwake hivyo, wala hawakuwa wakisimamiana wao kwa wao.” [Mukhtaswar Al-Fataawaa Al-Miswriyyah (2/26-27)]
Imaam Ibn Baaz (حمه الله) amesema: “Maswaahaba walikuwa wanapokutana naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walikuwa wakimwamkia kwa kumpa mikono na hawakuwa wakibusu mkono wake…” [Fataawaa Nuwr Alad-Darb ukanda 488)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
25-Unyenyekevu Wake Katika ‘Ibaadah Akivaa Nguo Duni
www.alhidaaya.com [16]
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنِ الرَّبِيعِ بْنِ صَبِيحٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبَانَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ حَجَّ النَّبِيُّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ عَلَى رَحْلٍ رَثٍّ وَقَطِيفَةٍ تُسَاوِي أَرْبَعَةَ دَرَاهِمَ أَوْ لاَ تُسَاوِي ثُمَّ قَالَ " اللَّهُمَّ حِجَّةٌ لاَ رِيَاءَ فِيهَا وَلاَ سُمْعَةَ " .
Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitekeleza Hajj akiwa katika kipando chake cha mnyama, alivaa joho lilokuwa na thamani ya dhirham nne au chini yake. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Allaah, (nakuomba iwe) Hajj isiyokuwa na riyaa-a (kujionyesha) wala umaarufu.” [Ibn Maajah, ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (2355), Swahiyh At-Targhiyb (1122)]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
26-Unyenyekevu Wake Akitembelea Wagonjwa Hata Wasio Waislamu
عَنْ ثَابِتٍ عَنْ أَنَسٍ رَضِي اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعُودُهُ فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ، فَقَالَ لَهُ: أَسْلِمْ فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ فَقَالَ لَهُ: أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَسْلَمَ فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ: الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنَ النَّارِ ((البخاري
Kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) amesema: Alikuweko mtoto wa ki-Yahudi akimhudumia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa anaumwa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea. Akaketi karibu ya kichwa chake na akamtaka asilimu. Yule mtoto akamtazama baba yake ambaye alikuwa ameketi karibu yake. Basi baba huyo akamwambia (mwanawe) amtii Abdul-Qaasim, na mtoto akatii na kusilimu. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka nje akisema: ((AlhamduliLLaah Ambaye Amemkinga na moto)) [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
27-Unyenyekevu Wake Katika Ibaadah Hakujitukuza Kwa Kujitanguliza Yeye
Katika Jamaraat (Kurusha Vijiwe Minaa)
Ingawa kawaida ya viongozi hutangulia kutekeleza jambo, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ni kiongozi wa Swahaba katika kutekeleza taratibu za Hajj, lakini hakujipa umbele kama kiongozi, bali alifanya nao pamoja bila ya kujitukuza.
عَنْ قُدَامَةَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْمِي جَمْرَةَ الْعَقَبَةِ يَوْمَ النَّحْرِ عَلَى نَاقَةٍ لَهُ صَهْبَاءَ لاَ ضَرْبَ وَلاَ طَرْدَ وَلاَ إِلَيْكَ إِلَيْكَ .
Amehadithia Qudaamah bin ‘Abdillaah kwamba: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa juu ya ngamia aliyechanganyika rangi nyekundu na kahawia, akirusha vijiwe katika Jamarah ya Al-‘Aqabah (Minaa) Siku ya An-Nahr (Siku ya Iydul-Adhw-haa), bila kumpiga mtu yeyote au kumfukuza." [At-Tirmidhiy na amesema Abuu ‘Iysaa Hadiyth Hasan Swahiyh. Imekusanywa pia na An-Nasaaiy na Ibn Maajah]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
28-Unyenyekevu Wake Anapokutana Na Mtu Na Kusalimiana Naye
Na Anapoketi Na Mtu
Miongoni mwa khulqa zake njema (صلى الله عليه وآله وسلم) na unyenyekevu wake, hakuwa akimgeuzia mtu uso wake mpaka yule mtu ageuke kwanza, na pindi mtu anapompa mkono kumsalimia, hakuwa akiondosha mkono wake hadi yule mtu aondoshe mkono wake, na pia hakuwa akiketi kwa magoti mbele ya mtu aliyeketi kwa magoti:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا لَقِيَ الرَّجُلَ فَكَلَّمَهُ لَمْ يَصْرِفْ وَجْهَهُ عَنْهُ حَتَّى يَكُونَ هُوَ الَّذِي يَنْصَرِفُ، وَإِذَا صَافَحَهُ لَمْ يَنْزِعْ يَدَهُ مِنْ يَدِهِ حَتَّى يَكُونَ هُوَ الَّذِي يَنْزِعُهَا، وَلَمْ يُرَ مُتَقَدِّمًا بِرُكْبَتَيْهِ جَلِيسًا لَهُ قَطُّ - ابن ماجه
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: “Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anapokkutana na mtu, huwa hamgeuzii uso wake hadi yule mtu awe ndiye mwenye kugeuza uso wake. Na pindi anapompa mtu mkono, alikuwa hauondoshi hadi yule mtu auondoshe mwenyewe. Na hakuwa akionekana kamwe ameketi kwa magoti yake mbele ya magoti ya yule aliyekuwa amekaa kando yake. [Ibn Maajah
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
29-Aliposhauri Jambo Katika Mas-ala Ya Kidunia Kwa Kutumia Rai Yake Ya Kibinafsi
Alikiri Kuwa Yeye Ni Bin Aadam
Alhidaaya.com [4]
Swahaba (رضي الله عنهم) waliheshimu ushauri wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mas-ala ya Dini yao na dunia yao. Basi pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowashauri jambo kwa fikra yake ya ki binafsi kuhusu jambo katika mambo ya kidunia, walifuata ushauri wake. Lakini ilipokuja kutambulika kuwa ushauri ule haukuwa wenye kunufasiha jambo hilo la ki dunia, basi alikiri kuwa yeye ni mwana Aadam huenda ukawa ushauri wake si wa kuwanufaisha jambo hilo, kwa hiyo akawanasihi anapowashauri au kuwaamrisha jambo katika mas-ala ya Dini wafuate, lakini katika mas-ala ya ushauri kutokana na fikra zake za kibinafsi, basi wafuate jambo ambalo wana ujuzi nalo zaidi wenyewe. Mfano ni kama huu uliosimuliwa katika Hadiyth kuhusu namna ya upandikizaji na uzalishajia wa mitende.
رَافِعُ بْنُ خَدِيجٍ، قَالَ قَدِمَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْمَدِينَةَ وَهُمْ يَأْبُرُونَ النَّخْلَ يَقُولُونَ يُلَقِّحُونَ النَّخْلَ فَقَالَ " مَا تَصْنَعُونَ " . قَالُوا كُنَّا نَصْنَعُهُ قَالَ " لَعَلَّكُمْ لَوْ لَمْ تَفْعَلُوا كَانَ خَيْرًا " . فَتَرَكُوهُ فَنَفَضَتْ أَوْ فَنَقَصَتْ - قَالَ - فَذَكَرُوا ذَلِكَ لَهُ فَقَالَ " إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ إِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ مِنْ دِينِكُمْ فَخُذُوا بِهِ وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ مِنْ رَأْىٍ فَإِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ " . قَالَ عِكْرِمَةُ أَوْ نَحْوَ هَذَا . قَالَ الْمَعْقِرِيُّ فَنَفَضَتْ . وَلَمْ يَشُكَّ .
Raafi’ bin Khadiyj (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja Madiyna na watu walikuwa wakipandikiza na kuzalisha mitende. Akasema: “Je, mnafanya nini?” Wakajibu: “Tunaipandikiza.” Akasema: “Labda msingelifanya hivyo hiyvo ingelikuwa bora.” Wakaacha (kupandikiza na kuchipuza au kuzalisha mitende kwa njia zao), lakini matokeo yake yakawa ni kupatikana uchache wa mazao. Wakamtajia hilo, hapo akasema: “Mimi ni mwana Aadam, nnapokuamrisheni jambo la kuhus Dini yenu basi lipokeeni na fuateni, lakini nnapokuamrisheni jambo la rai yangu, basi hakika mimi ni mwana Aadam.” Ikirmah amesema: “Alisema jambo kama hivyo.” [Muslim]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/285
[2] http://alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10310&title=Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10343&title=01-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Kutokulalamika%20Chakula%20Nyumbani%20Kwake
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10345&title=02-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Alikiri%20Kuwa%20Manabii%20Wengineo%20Ni%20Bora%20Kuliko%20Yeye
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10346&title=03-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Akifanya%20Kazi%20Za%20Nyumbani%20Kwake%20Na%20Kuwahudumia%20Ahli%20Wake
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10347&title=04-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Akiwasalimia%20Watoto%20Na%20Kuwapapasa%20Vichwa%20Vyao%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10348&title=05-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Akikaa%20Na%20Maswahaba%20Kuongea%20Nao
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10349&title=06-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Hakujiona%20Yeye%20Ni%20Bora%20Kuliko%20Maswahaba%20Wake
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10350&title=07-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Aliitikia%20Mwaliko%20Na%20Kupokea%20Zawadi%20%20Hata%20Kama%20Ni%20Duni
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10351&title=08-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Alikataa%20Kutukuzwa%20Mno%20Kama%20Walivyotukuzwa%20Manabii%20Wa%20Awali%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10352&title=09-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Akipanda%20Punda%20Na%20Akiitikia%20Mwaliko%20wa%20Mtumwa
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10353&title=10-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Aliwabashiria%20Masikini%20Jannah
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10354&title=11-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Alikuwa%20Akitembelea%20Masikini%20Akizuru%20Wagonjwa%20Wao%20Na%20Akihudhuria%20Maziko%20Yao
[16] http://www.alhidaaya.com
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10355&title=12-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akiwahudumia%20Wajakazi%20Na%20Kuwatimizia%20Haja%20Zao%20
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10356&title=13-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akiomba%20Kuishi%20Umasikini%20Na%20Kufishwa%20Pamoja%20Na%20Masikini%20Na%20Akinasihi%20Kuwa%20Karibu%20Nao%20
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10357&title=14-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Hakukataa%20Kuhudumiwa%20Na%20Watumwa%20
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10358&title=15-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Aliwafunza%20Maswahaba%20Wawe%20Unyenyekevu%20Ili%20Wasifanyiane%20Ufidhuli%20Au%20Kujifakharisha
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10359&title=16-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3AUnyenyekevu%20Wake%3A%20Akiwafundisha%20Maswahaba%20Fadhila%20Za%20Unyenyekevu%20Kuwa%20Unapandisha%20Daraja%20
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10360&title=17-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akiwahudumia%20Maswahaba%20Kama%20Kuwamiminia%20Maji%20Ya%20Kunywa%20
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10361&title=18-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyeyekevu%20Wake%3A%20Hakuwa%20Mwenye%20Kiburi%20Bali%20Amekataza%20Kutakabari
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10362&title=19-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Akinyenyekea%20Kwa%20Ahli%20Zake%20
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10363&title=20-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akimhudumia%20Yeyote%20Aliyemuomba%20Njiani
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10364&title=21-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3AUnyenyekevu%20Wake%3A%20Akila%20Na%20Kuketi%20Kama%20Wanavyokula%20Na%20Kuketi%20Maswahaba
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10365&title=22-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akimpandisha%20Kwanza%20Swahaba%20Wake%20Kabla%20Yake%20Katika%20Kipando
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10366&title=23-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akichukuwa%20Ushauri%20Kwa%20Swahaba%20Zake
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10367&title=24-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akichukia%20Kusimamiwa
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10368&title=25-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Katika%20%E2%80%98Ibaadah%20Akivaa%20Nguo%20Duni
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10369&title=26-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Akitembelea%20Wagonjwa%20Hata%20Wasio%20Waislamu
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10370&title=27-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%20Katika%20Ibaadah%3A%20Hakujitukuza%20Kwa%20Kujitanguliza%20Yeye%20Katika%20Jamaraat%20%28Kurusha%20Vijiwe%20Minaa%29%20
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10371&title=28-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%20%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Anapokutana%20Na%20Mtu%20Na%20Kusalimiana%20Naye%20Na%20Anapoketi%20Na%20Mtu%20
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10306&title=29-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Unyenyekevu%20Wake%3A%20Aliposhauri%20Jambo%20Katika%20Mas-ala%20Ya%20Kidunia%20Kwa%20Kutumia%20Rai%20Yake%20Alikiri%20Kuwa%20Yeye%20Ni%20Bin%20Aadam%20%20