Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Aashuraa: Mwenye Hedhi Siku Ya 'Aashuraa Inajuzu Alipe Swawm Hiyo?

 

Mwenye Hedhi Siku Ya 'Aashuraa Je Inajuzu Alipe Swawm Hiyo?

Nini Hukmu Ya Kulipa Nawaafil?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Yule ambae imemfikia 'Aashuraa akiwa ni mwenye hedhi, Je,  hulipa Swawm yake? Je kuna Shariy’ah ya kulipa au kutolipa Nawaafil (Swala za khiari au ziada, yaani Sunnah) (Jazaaka-Allaahu khayraa.  

 

 

JIBU:

 

Nawaafil zipo aina mbili; Aina yenye sababu na aina isiyo na sababu.

 

Yenye sababu huondoka kwa kuondoka sababu na hailipwi. Mfano wake: Tahiyyatul-Masjid (Unapoingia tu Msikitini); akija mtu akakaa muda mrefu kisha akataka kuleta Tahiyyatul-Masjid haitokuwa ni Tahiyyatul-Masjid kwani ni Swalaah yenye sababu imeunganishwa na sababu,  ikiondoka basi wajibu wake huondoka.

 

Na mfano wake pia ni kile kinachodhihiri katika siku ya 'Arafah na siku ya 'Aashuraa;  hivyo mtu akichelewesha Swawm ya 'Arafah na 'Aashuraa bila ya udhuru, bila shaka hailipwi na hainufaishi lau akilipa; yaani hainufaishi ya kuwa amefunga 'Arafah au amefunga 'Aashuraa.

 

Ama ikimpita mtu naye akiwa ni mwenye udhuru kwa mfano mwenye hedhi au nifaas (damu ya uzazi) au mgonjwa, basi dhahiri ni kuwa vile vile halipi kwani hii ni makhsusi kwa siku fulani maalum. Huondoka hukumu yake kwa kuondoka siku hii.

 

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Rasaail Ash-Shaykh Muhammad Swaalih Al-‘Uthyamiyn Mjalada 20 Kitaab Asw-Swiyaam]  

 

 

 

Share