040-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi na Kuunga Kizazi (Ujamaa)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب بر الوالدين وصلة الأرحام

040-Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi na Kuunga Kizazi (Ujamaa)

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ  ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. [An-Nisaa: 36]

وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ  ﴿١﴾ 

Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. [An-Nisaa:1]

وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ ﴿٢١﴾

Na ambao wanaunga yale Aliyoamrisha Allaah kuungwa. [Ar-Ra'd: 21]

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ  ﴿٨﴾

Na Tumemuusia insani kuwafanyia wema wazazi wake wawili. [Al-'Ankabuwt: 8]

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾ وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima.Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 23-24]

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ ﴿١٤﴾

Na Tumemuusia insani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; [Luqmaan: 14]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي عبد الرحمان عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : سألت النبي صلى الله عليه وسلم: أيُّ العَمَلِ أحَبُّ إِلَى اللهِ تَعَالَى ؟ قَالَ : (( الصَّلاةُ عَلَى وَقْتِهَا )) ، قُلْتُ : ثُمَّ أي ؟ قَالَ : (( بِرُّ الوَالِدَيْنِ )) ، قُلْتُ : ثُمَّ أيٌّ ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ في سبيلِ الله )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdur-Rahman 'Abdillaah bin bin Mas'uud (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni amali gani inayompendeza zaidi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)? Akajibu: "Swalaah kwa wakati wake." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Wema kwa wazazi wawili." Nikasema: "Kisha ipi?" Akasema: "Jihaad katika Njia ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يَجْزِي وَلَدٌ وَالِداً إلاَّ أنْ يَجِدَهُ مَمْلُوكاً ، فَيَشْتَرِيهُ فَيُعْتِقَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtoto hawezi kumlipa mzazi isipokuwa kama atamkuta amemilikiwa (mtumwa), akamnunua kisha akamuacha huru."  [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَصِلْ  رَحِمَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ ))  مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aunge kizazi. Na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho aseme maneno ya kheri (mazuri) au anyamaze." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ اللهَ تَعَالَى خَلَقَ الخَلْقَ حَتَّى إِذَا فَرَغَ مِنْهُمْ قَامَتِ الرَّحِمُ ، فَقَالَتْ : هَذَا مُقَامُ العَائِذِ بِكَ مِنَ القَطِيعةِ ، قَالَ : نَعَمْ ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ أصِلَ مَنْ وَصَلَكِ ، وَأقْطَعَ مَنْ قَطَعَكِ ؟ قَالَتْ : بَلَى ، قَالَ : فَذَلِكَ لَكِ ، ثُمَّ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( اقْرَؤُوا إنْ شِئْتمْ : ( فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ  ) [ محمد : 22 - 23 ] مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية للبخاري : فَقَالَ الله تَعَالَى : (( مَنْ وَصَلَكِ ، وَصَلْتُهُ ، وَمَنْ  قَطَعَكِ ، قَطَعْتُهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kuumba viumbe vyote, mpaka Alipomaliza (kukamilisha), yalisimama matumbo (kizazi) na kusema: "Hii ni nafasi ya mtu anayetaka ulinzi  na kinga kutoka  Kwako kwa mwemye kukata (kizazi, na kihitaji ulinzi)." Akasema: "Ndio je huridhiki Kwangu kumuunga anayekuunga, na kumkata mwenye kukukata?" Kikasema: "Ndio (naridhika)." Akaambiwa: "Hilo ni lako." Kisha akasema  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Someni mkitaka: "Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao." [Muhammad: 22-23] [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): "Anayekuunga, Nitamuunga na anayekukata Nitamkata."

 

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ: جاء رجل إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: يَا رَسُول الله ، مَنْ أحَقُّ النَّاسِ بِحُسْنِ صَحَابَتِي ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) ، قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ )) ، قَالَ : ثُمَّ مَنْ ؟ قَالَ : (( أبُوكَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : يَا رَسُول الله ، مَنْ أَحَقُّ بحُسْنِ الصُّحْبَةِ ؟ قَالَ : (( أُمُّكَ ، ثُمَّ  أُمُّكَ ، ثُمَّ أُمُّكَ ، ثُمَّ أَبَاكَ ، ثُمَّ أدْنَاكَ أدْنَاكَ )) .

Na kutoka kwake Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Ee Rasli wa Allaah! Nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu wa kuwa naye na ushirikiano mzuri (na mwema)?" na Akasema: "Mama yako." Akauliza tena: "Kisha nani?" Akasema: "Mama yako." Akauliza: "Kisha nani?" Akasema: "Mama yako." Akauliza tena: "Kisha nani?" Akasema: "Baba yako." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyengine: "Ee Rasuli wa Allaah! Nani mwenye haki zaidi ya kusuhubiana naye kwa mema?" Akasema: "Mamako, kisha mamako, kisha mamako, kisha babako, kisha wale alio chini yao."

 

 

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( رغِم أنفُ ، ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ ، ثُمَّ رَغِمَ أنْفُ مَنْ أدْرَكَ أبَويهِ عِنْدَ الكِبَرِ ، أَحَدهُما أَوْ كِليهمَا فَلَمْ يَدْخُلِ الجَنَّةَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Raghima anf, kisha raghima anf, kisha raghima anf (kudhalilishwa), mtu aliyewakuta wazazi wake katika uzee; mmoja wao au wote wawili na asiingie Peponi." [Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رجلاً قَالَ : يَا رَسُول الله ، إنّ لِي قَرابةً أصِلُهُمْ وَيَقْطَعُوني ، وَأُحْسِنُ إلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إلَيَّ ، وَأحْلَمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ ، فَقَالَ :(( لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ ، فَكأنَّمَا تُسِفُّهُمْ الْمَلَّ ، وَلاَ يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذلِكَ )) رواه مسلم .

Na kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Kuna mtu alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nina jamaa zangu, ninaowaunga, nao wananikata. Nawafanyia wema wananifanyia mabaya; nawasamehe wananitukana." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): " Ikiwa uko kama unavyosema, itakuwa ni kama unawalisha jivu la moto; na muda huachi kuwa hivyo ila Allaah atakusaidia dhidi yao." [Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن أنسٍ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( من أحَبَّ أنْ يُبْسَطَ لَهُ في رِزْقِهِ ، ويُنْسأَ لَهُ في أثَرِهِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayependa akunjuliwe riziki yake, na arefushiwe maisha yake basi aunge kizazi chake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]  

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن أنسٍ رضي الله عنه، قَالَ : كَانَ أَبُو طَلْحَةَ أكْثَرَ الأنْصَارِ بالمَدينَةِ مَالاً مِنْ نَخل ، وَكَانَ أحَبُّ أمْوَاله إِلَيْهِ بَيْرَحاء ، وَكَانَتْ مسْتَقْبَلَةَ المَسْجِدِ ، وَكَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَدْخُلُهَا ، وَيَشْرَبُ مِنْ مَاءٍ فِيهَا طَيِّب ، فَلَمَّا نَزَلَتْ هذِهِ الآيةُ : ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) [ آل عمران : 92 ] قَامَ أَبُو طَلْحَةَ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، إنَّ الله تبارك وتَعَالَى ، يقول : ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) وَإنَّ أَحَبَّ مَالِي إِلَيَّ بَيْرَحَاءُ ، وَإنَّهَا صَدَقَةٌ للهِ تَعَالَى ، أرْجُو بِرَّهَا وَذُخْرَهَا عِنْدَ الله تَعَالَى ، فَضَعْهَا يَا رَسُول الله ، حَيْثُ أرَاكَ الله . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( بَخ ! ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ، ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ! وقَدْ سَمِعْتُ مَا قُلْتَ ، وَإنِّي أرَى أنْ تَجْعَلَهَا في الأقْرَبينَ )) ، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ : أفْعَلُ يَا رَسُول الله ، فَقَسَّمَهَا أَبُو طَلْحَةَ في أقَارِبِهِ وبَنِي عَمِّهِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Toka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: 'Abu Twalhah alikuwa na mitende mingi kuliko Answariwote. Mali iliyompendeza zaidi ni shamba lililokuwa Bayrahaa', lililokuwa limeelekeana na Msikiti wa Nabiy. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiingia humo na kunywa maji yake tamu. Amesema Anas: Ilipoteremka ayah hii (Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda) [Aal-'Imraan: 92] Abu Twalhah alimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Allaah ( Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekuteremshia: '(Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda)'. Kwa hakika mali niipendayo sana ni shamba la Bayrahaa', nimelitoa sadaka kwa ajili ya Allaah nikitaraji kheri na ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Ee Rasuli wa Allaah, nakuomba uliweke Atakavyokuonyesha Allaah. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Bakhin, Hiyo ni mali yenye faida, hiyo ni mali yenye faida. Bila shaka nimesikia uliyosema. Mimi naona uwape jamaa zako wa karibu." Abu Twalhah akasema: "Nitafanya, Ee Rasuli wa Allaah! Abu Twalhah akaligawa kwa jamaa zake na binamu zake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 10

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : أقبلَ رَجُلٌ إِلَى نَبيِّ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : أُبَايِعُكَ عَلَى الهِجْرَةِ وَالجِهَادِ أَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى . قَالَ : (( فَهَلْ لَكَ مِنْ وَالِدَيْكَ أحَدٌ حَيٌّ ؟ )) قَالَ : نَعَمْ ، بَلْ كِلاهُمَا . قَالَ : (( فَتَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى ؟ )) قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( فارْجِعْ إِلَى وَالِدَيْكَ ، فَأحْسِنْ صُحْبَتَهُمَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، وهذا لَفْظُ مسلِم .

وفي رواية لَهُمَا : جَاءَ رَجُلٌ فَاسْتَأذَنَهُ في الجِهَادِ ، فقَالَ : (( أحَيٌّ وَالِداكَ ؟ ))
قَالَ : نَعَمْ ، قَالَ : (( فَفيهِمَا فَجَاهِدْ )) .

Na amesema 'Abdillaahi bin 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa):  Mtu mmoja alimkabili Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Nitakubai juu ya Hijra na Jihaad nikitafuta ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)." Akasema: "Je, katika wazazi wako yuko aliye hai?" Akajibu: "Ndio, bali wote wawili." Akamuuliza: "je, unataka ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)?" Akasema: "Ndio." Akamwambia: "Rudi kwa wazazi wako na usuhubiane nao kwa wema (wafanyie wema)." [Al-Bukhaariy na Muslim], na hii ni lafdhi ya Muslim. pia imenukuliwa na Abu Daawuud na An-Nasaa'iy.

Riwaayah ya wao wawili: Alikuja mtu akataka ruhusa ya Jihaad. Akaulizwa: "Je wazazi wako wako hai?" Akasema: "Ndio." Akaambiwa: "Kwao wao, pigana Jihaad."

 

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَيْسَ الوَاصِلُ بِالمُكَافِىء ، وَلكِنَّ الوَاصِلَ الَّذِي إِذَا قَطَعَتْ رَحِمُهُ وَصَلَهَا )) رواه البخاري .

Na kutoka kwake Ibn 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa):  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayeunga si yule anayetoa anapopewa, lakini anayeunga jamaa ni ambaye jamaa zake wanapomkata, yeye huwaunga." [Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

Hadiyth – 12

وعن عائشة ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالعَرْشِ تَقُولُ : مَنْ وَصَلَنِي ، وَصَلَهُ اللهُ ، وَمَنْ قَطَعَنِي ، قَطَعَهُ اللهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kizazi kimetundikwa katika 'Arshi, kinasema: "Anayeniunga, Allaah atamuunga, na anayenikata, Allaah Atamkata." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 13

وعن أم المؤمنين ميمونة بنتِ الحارث رضي الله عنها : أنَّهَا أعْتَقَتْ وَليدَةً وَلَمْ تَستَأذِنِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُهَا الَّذِي يَدُورُ عَلَيْهَا فِيهِ ، قَالَتْ : أشَعَرْتَ يَا رَسُول الله ، أنِّي أعتَقْتُ وَليدَتِي ؟ قَالَ : (( أَوَ فَعَلْتِ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . قَالَ : (( أما إنَّكِ لَوْ أعْطَيْتِهَا أخْوَالَكِ كَانَ أعْظَمَ لأجْرِكِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Maymuunah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'Anhaa) kuwa alimwacha huru kijakazi bila kumuomba idhini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alipomtembelea (Maymuunah) siku yake, alimuuliza: "Je umejua, Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa nimemwacha huru kijakazi wangu?" Akamuuliza: "Je, umefanya hivyo?" Akajibu: "Ndio." Akasema: "Lau ungewapatia (kijakazi huyo) wajomba zako ungepata ujira mkubwa zaidi."  [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]

 

 

 

 

Hadiyth – 14

وعن أسماءَ بنتِ أَبي بكر الصديق رضي الله عنهما ، قَالَتْ : قَدِمَتْ عَلَيَّ أُمِّي وَهِيَ مُشركةٌ في عَهْدِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فاسْتَفْتَيْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قُلْتُ : قَدِمَتْ عَلَيَّ أُمِّي وَهِيَ رَاغِبَةٌ ، أفَأصِلُ أُمِّي ؟ قَالَ : (( نَعَمْ ، صِلِي أُمَّكِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Na amesema Asmaa' bint Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Alikuja kwangu mamangu, akiwa ni mushrik katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitaka usaidizi kutoka kwangu. Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mamangu amekuja kwangu akitaka usaidizi, je nimuunge mamngu (kwa kumfanyia wema) mamako."  [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]

 

 

 

 

Hadiyth – 15

وعن زينب الثقفيةِ امرأةِ عبدِ الله بن مسعود رضي الله عَنْهُ وعنها ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( تَصَدَّقْنَ يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ وَلَوْ مِنْ حُلِيِّكُنَّ ))، قَالَتْ : فَرَجَعْتُ إِلَى عبد الله بنِ مسعود ، فقلتُ لَهُ : إنَّكَ رَجُلٌ خَفِيفُ ذَاتِ اليَدِ ، وَإنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ أمَرَنَا بِالصَّدَقَةِ فَأْتِهِ ، فَاسألهُ ، فإنْ كَانَ ذلِكَ يْجُزِىءُ عَنِّي وَإلاَّ صَرَفْتُهَا إِلَى غَيْرِكُمْ . فَقَالَ عبدُ اللهِ : بَلِ ائْتِيهِ أنتِ ، فانْطَلَقتُ ، فَإذا امْرأةٌ مِنَ الأنْصارِ بِبَابِ رسولِ الله  صلى الله عليه وسلم حَاجَتي حَاجَتُها ، وَكَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ أُلْقِيَتْ عَلَيهِ المَهَابَةُ ، فَخَرجَ عَلَيْنَا بِلاَلٌ ، فَقُلْنَا لَهُ : ائْتِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَأخْبرْهُ أنَّ امْرَأتَيْنِ بالبَابِ تَسألانِكَ : أُتُجْزِىءُ الصَّدَقَةُ عَنْهُمَا عَلَى أزْواجِهمَا وَعَلَى أيْتَامٍ في    حُجُورِهِما ؟ ، وَلاَ تُخْبِرْهُ مَنْ نَحْنُ ، فَدَخلَ بِلاَلٌ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فسأله ، فَقَالَ لَهُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ هُمَا ؟ )) قَالَ : امْرَأةٌ مِنَ الأنْصَارِ وَزَيْنَبُ . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( أيُّ الزَّيَانِبِ هِيَ ؟ )) ، قَالَ : امْرَأةُ عبدِ الله ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَهُمَا أجْرَانِ : أجْرُ القَرَابَةِ وَأجْرُ الصَّدَقَةِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kwa Zaynab Ath-Thaqafiyyah (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) mke wa 'Abdillaahi bin Mas'uud kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Enyi kongamano la wanawake, toeni sadaqah japokuwa ni mapambo ya vito." Akasema: Nilirudi kwa 'Abdillaahi bin Mas'uud nikamwambia: "Hakika wewe ni mtu mwenye mali kidogo na  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru tutoe sadaqah, nenda ukamuulize ikiwa inanitosheleza kukupa wewe, ikiwa si hinyo nimpatie mwengine." Akasema 'Abdillaahi: "Bali nenda mwenyewe." Nikatoka kuelekea (kwa Rasuli), hapo nikakutana na mwanamke miongoni mwa Answaar mlangoni mwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), haja yake ni kama yangu. Na tulikuwa tunamstahi sana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, pindi alipotutokea Bilaal (Radhwiyah Allaahu 'anhu) tulimwambia: "Nenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) umpashe habari kuwa wapo wanawake wawili mlangoni wanakuuliza: "Je, inatosha kwa wao wanawake kuwapatia waume zao swadaqah (zakaah) na pia mayatima majumbani mwao wala usimwambie sisi ni nani." Bilaal akaingia kumuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: "Wao ni nani?" Akajibu: "Mwanamke wa Ki-Answaar na Zaynab." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Zaynab gani huyo?" Akajibu: "Ni mkewe 'Abdillaahi." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Watapata thawabu mara mbili: Ujira wa ujamaa na ujira wa swadaqah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 16

وعن أَبي سفيان صخر بنِ حرب رضي الله عَنْهُ في حديثِهِ الطويل في قِصَّةِ هِرَقْلَ : أنَّ هرقْلَ قَالَ لأبي سُفْيَانَ : فَمَاذَا يَأمُرُكُمْ بِهِ ؟ يَعْنِي النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : قُلْتُ : يقول : (( اعْبُدُوا اللهَ وَحْدَهُ ، وَلاَ تُشْرِكُوا بِهِ شَيئاً ، واتْرُكُوا مَا يَقُولُ آبَاؤُكُمْ ، وَيَأمُرُنَا بِالصَّلاةِ ، وَالصّدْقِ ، والعَفَافِ ، والصِّلَةِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Sufyaan Swakhr bin Harb (Radhwiyah Allaahu 'anhu) katika hadiyth yake ndefu kuhusiana na kisa cha Hiraql. Hiraqal alimuuliza Abu Sufyaan: "Je, anawaamuru nini, Yani: Nabiy?" Akasema: Nikamwambia kuwa anasema: Muabuduni Allaah Peke Yake wala usimshirikishe Yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, anatuamuru kuswali, kusema ukweli, kuwa safi (kutozini) na kuunga uzazi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 17

وعن أَبي ذرّ رضي الله عَنْهُ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّكُمْ سَتَفْتَحُونَ أرْضاً يُذْكَرُ فِيهَا القِيرَاطُ )) . وفي رواية : (( سَتَفْتَحونَ مِصْرَ وَهِيَ أرْضٌ يُسَمَّى فِيهَا القِيراطُ ، فَاسْتَوْصُوا بأهْلِهَا خَيْراً ؛ فَإنَّ لَهُمْ ذِمَّةً وَرَحِماً )) وفي رواية : (( فإذا افتتحتموها ، فأحسنوا إلى أهلها ؛ فإن لهم ذمة ورحماً )) ، أَوْ قَالَ : (( ذِمَّةً وصِهْراً )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika nyinyi mtaifungua ardhi inayoitwa Qiyraatw." Na katika riwaayah nyengine: Mtaifungua Misri na hiyo ni ardhi inayoitwa Qiyraatw, wafanyieni wema watu wake; kwani wana uhusiano nanyi, katika haki ya ulinzi na kizazi", Katika riwaayah : Mapoifungua, wafanyieni wema watu wake; kwani tuna uhusiano naowa ulinzi na kizazi" au amesema: "haki na ukwe." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 18

وعن أَبي هريرة رضي الله عَنْهُ، قَالَ : لما نزلت هذِهِ الآية : ( وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ ) [ الشعراء : 214] دَعَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قُرَيْشاً ، فَاجْتَمَعُوا فَعَمَّ وَخَصَّ ، وَقالَ : (( يَا بَنِي عَبْدِ شَمْسٍ ، يا بَنِي كَعْبِ بْنِ لُؤيٍّ ، أنقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي مُرَّةَ بن كَعْبٍ ، أنْقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي عَبْدِ مَنَاف ، أنْقِذُوا أنْفُسَكُمْ مِنَ النَّارِ ، يَا بَنِي هاشم ، أنقذوا أنفسكم من النار ، يَا بني عبد المطلب ، انقذوا أنفسكم من النار ، يَا فَاطِمَةُ ، أنْقِذي نَفْسَكِ مِنَ النَّارِ . فَإنِّي لا أمْلِكُ لَكُمْ مِنَ اللهِ شَيئاً ، غَيْرَ أنَّ لَكُمْ رَحِماً سَأبُلُّهَا بِبِلالِهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Ilipoteremka aayah hii: "Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu." [Ash-Shu'araa: 214]. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Maquraysh katika makundi yao na watu binafsi, akasema: "Enyi Bani 'Abdi Shams, enyi Bani Ka'b bin Lu'ayy, ziokoeni nafsi zenu na Moto. Enyi Bani Murrah bin Ka'b, ziokoeni nafsi zenu na Moto; enyi Bani 'Abdi Manaaf, ziokoeni nafsi zenu na Moto, enyi Bani Haashim, ziokoeni nafsi zenu na Moto; enyi Bani 'Abdil Mutwtwalib, ziokoeni nafsi zenu na Moto; Ee Faatwimah, okoa nafsi yako na Moto, kwani siwezi kuwafanyia lolote mbele ya Allaah. Hata hivyo, baina yetu kuna unasaba, nami nitaulinda. (na kuuhifadhi)." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 19

وعن أَبي عبد الله عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم جِهَاراً غَيْرَ سِرٍّ ، يَقُولُ : (( إنَّ آل بَني فُلاَن لَيْسُوا بِأولِيَائِي ، إِنَّمَاوَلِيِّيَ اللهُ وَصَالِحُ المُؤْمِنينَ ، وَلَكِنْ لَهُمْ رَحِمٌ أبُلُّهَا بِبلاَلِهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، واللفظ للبخاري .

Kutoka kwa Abu Abdillaahi 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema waziwazi bila kuficha: "Hakika jamaa wa Bani fulani si rafiki zangu. Hakika rafiki yangu ni Allaah na walio wema katika Waumini, lakini wana ujamaa, nitauunga." [Al-Bukhaariy na Muslim, na lafdhi ni ya Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 20

وعن أَبي أيوب خالد بن زيد الأنصاري رضي الله عَنْهُ: أنَّ رجلاً قَالَ : يَا رَسُول الله ، أخْبِرْني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجَنَّةَ ، وَيُبَاعِدُني مِنَ النَّارِ . فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: (( تَعْبُدُ الله ، وَلاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً ، وَتُقِيمُ الصَّلاةَ ، وتُؤتِي الزَّكَاةَ ، وتَصِلُ الرَّحمَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Ayyuub Khaalid bin Zayd Al-Answaariy (Radhwiyah Allaahu 'anhumma) kuwa mtu mmoja alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nipe habari ya amali itakayo niingiza Peponi na kuniepusha na Moto?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Muabuduni Allaah wala usimshirikishe kwa chochote, usimamishe Swalaah, utoe Zakaah na uunge kizazi (ujamaa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 21

وعن سلمان بن عامر رضي الله عَنْهُ ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أفْطَرَ أحَدُكُمْ ، فَلْيُفْطرْ عَلَى تَمْرٍ ؛ فَإنَّهُ بَرَكةٌ ، فَإنْ لَمْ يَجِدْ تَمْراً ، فالمَاءُ ؛ فَإنَّهُ  طَهُورٌ )) ، وَقالَ : (( الصَّدَقَةُ عَلَى المِسكينِ صَدَقةٌ ، وعَلَى ذِي الرَّحِمِ ثِنْتَانِ : صَدَقَةٌ وَصِلَةٌ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofuturu mmoja wenu afuturu kwa tende, kwani ina baraka. Asiopata tende, basi afungue kwa maji; kwani yanatwahirisha." Na akasema: "Sadaqah kwa maskini ni sadaqah na kumpa jamaa ina ujira mara mbili: ni sadaqah na kuunga ujamaa." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 22

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَتْ تَحْتِي امْرَأةٌ ، وَكُنْتُ أحِبُّهَا ، وَكَانَ عُمَرُ يَكْرَهُهَا ، فَقَالَ لي : طَلِّقْهَا ، فَأبَيْتُ ، فَأتَى عُمَرُ رضي الله عَنْهُ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَذَكَرَ ذلِكَ لَهُ ، فَقَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( طَلِّقْهَا )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nilimuoa mke niliyekuwa nampenda; lakini 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alikuwa anamchukia. Akaniambia: "Mpatie talaka", Nikakataa. 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumtajia jambo hilo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mtaliki." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, naye akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 23

وعن أَبي الدرداءِ رضي الله عَنْهُ: أن رجلاً أتاه ، قَالَ : إنّ لي امرأةً وإنّ أُمِّي تَأمُرُنِي بِطَلاقِهَا ؟ فَقَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( الوَالِدُ أوْسَطُ أبْوَابِ الجَنَّةِ ، فَإنْ شِئْتَ ، فَأضِعْ ذلِكَ البَابَ ، أَو احْفَظْهُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa mtu mmoja alikuja kwake, akamuuliza: "Hakika mimi nina mke, ambaye mamangu anataka nimuache?" Akamwambia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mzazi ndiye mlango bora miongoni mwa milango ya Peponi, ukitaka upoteze huo mlango au uhifadhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

Hadiyth – 24

وعن البراءِ بن عازب رضي اللهُ عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الخَالةُ بِمَنْزِلَةِ الأُمِّ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhiwyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Halati (mama mdogo) yu katika daraja ya mama."  [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

 

 

 

 

Share