Shurba Ya Nyama Mbuzi - 1

Shurba  Ya Nyama Mbuzi - 1

Vipimo

Nyama ya mbuzi ya mafupa au ya ng'ombe - Kilo moja

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo) - 2

Nyanya (kata ndogo ndogo) - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 1 kijijo cha chai

Gilgilani ya unga (Dania) - ½  kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga - ¼ kijiko cha chai

Kotmiri (iliyokatwa ndogo ndogo) - kiasi

Nanaa (iliyokatwa ndogo ndogo) - kiasi

Chumvi - kiasi

Siki - 3 vijiko vya supu  

Shayiri* /Hariys - 2 vikombe

* Shayiri ni aina ya ngano (oats) ila ni tofauti kidogo na ngano. Baadhi ya maduka inajulikana kama ni 'hariys' .

Kidokezo:

Ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa  muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive.

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Chemsha nyama na chumvi kwa maji kiasi  mpaka iwive.
  2. Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.
  3. Weka bizari zote, pili pili manga, chumvi.
  4. Tia thomu na tangawizi.
  5. Tia nyanya na bila ya kuzikaanga sana tia nyama na supu yake.
  6. Tia kotmiri, nanaa.
  7. Pembeni changanya shayiri  na maji koroga kisha tia katika supu ya shurba.
  8. Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.
  9. Tia siki na tayari kuliwa. 
Share