Keki Ya Jibini Ya Nanasi (Pineapple Cheese Cake)

Keki Ya Jibini  Ya Nanasi  (Pineapple Cheese Cake)

Vipimo 

Malai ya Jibini (Cream Cheese) - 450g Pakiti 2

Sukari  -   1/2 Kikombe

Mayai  -   2

Unga wa ngano  -   1 Kijiko cha chai

Mtindi (yogurt)  -    1/2 Kikombe cha chai

Ukoko wa tayari  (ready crust) -   2

Mananasi ya kopo -   1

Kastadi ya unga -  1 Kijiko cha chai

 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Washa oveni 350°F.
  2. Kwenye bakuli la mashine, changanya malai ya jibini, sukari, mtindi na unga upige hadi ichanganyikane vizuri.
  3. Kisha tia mayai na upige kidogo.
  4. Ikisha changanyika vizuri mimina juu ya ule ukoko (crust)  na utandaze kila kipembe.
  5. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 15, kisha weka moto wa 300°F na uchome kwa muda wa saa moja.
  6. Ikishaiva iache ipoe na huku uitayarishie sosi yake.
  7. Katika kisufuria, tia ile juisi ya mananasi utakayoitoa kwenye kopo, pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga hadi iwe nzito.
  8. Mimina juu ya Keki Ya Jibini na upange mananasi. Ukipenda weka cheri au jelly katikati ya duara ya mananasi.
  9. Iweke kwenye friji ipate baridi na itakuwa tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

Unaweza ukagawanya vipimo mara mbili ukatoa keki moja.

 

 

 

Share