Keki Ya Nazi Na Semolina Kwa Shira Ya Mdalasini

Keki Ya Nazi Na Semolina Kwa Shira Ya Mdalasini

 

Vipimo 

Nazi ya chenga kikombe 1

Unga wa sembe wa chenga (Semolina) 1

Vijiko 10 vya kulia

Sukari  kikombe 1

Baking powder kijiko cha chai

Mtindi 1 kikombe

Maziwa mazito ¼   kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Andaa shira yake kwanza:
  2. Washa oven moto wa kiasi baina ya 300 – 350 Deg F
  3. Katika bakuli changanya sukari na mtindi mpaka ilainike.
  4. Tia unga wa sembe wa chenga (semolina), maziwa na baking powder.
  5. Pole pole tia siagi uliyoyayuka changanya vizuri.
  6. Funika uache mchanganyiko kidogo utulie.
  7. Mimina kwenye treya ya oven uliyopakaza siagi.
  8. Pika (bake) kiasi kwa muda dakika 40 takriban mpaka juu igeuke rangi ya hudhurungi na uhakikishe imewiva.
  9. Epua umwagie shira yake>

 

Shira

 

Sukari kikombe 1 ½

Maji kikombe 1 ¾

Mdalasini ½ kijiko cha chai

Ndimuu ½ kijiko cha chai

 

Changanya vizuri uchemshe hadi iwe nzito kisha acha ipoe ndio umwagi juu ya keki  iyayuke ndani yake

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

Share