036-Asbaabun-Nuzuwl: Yaasiyn Aayah 12: إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
036-Asbaabun-Nuzuwl: Yaasiyn Aayah 12
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ ﴿١٢﴾
Hakika Sisi Tunahuisha wafu, na Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao na kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari bayana. [Yaasiyn (36:12)]
Sababun-Nuzuwl:
قال الْحَافِظ أَبُو بَكْر الْبَزَّار حَدَّثَنَا عَبَّاد بْن زِيَاد السَّاجِيّ حَدَّثَنَا عُثْمَان بْن عُمَر حَدَّثَنَا شُعْبَة عَنْ سَعِيد الْجُرَيْرِيّ عَنْ أَبِي نَضْرَة عَنْ أَبِي سَعِيد رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : إِنَّ بَنِي سَلَمَة شَكَوْا إِلَى رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بُعْد مَنَازِلهمْ مِنْ الْمَسْجِد فَنَزَلَ: (( وَنَكْتُب مَا قَدَّمُوا وَآثَارهمْ ))
Al-Haafidh Abu Bakr Al-Bazzaar amesema: Ametuhadithia ‘Abbaad bin Ziyaad As-Saajiyy, ametuhadithia ‘Uthmaan bin ‘Umar, ametuhadithia Shu‘ubah toka kwa Al-Jariyriy toka kwa Abu Nadhwrah (naye ni Al-Mundhir bin Maalik) toka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: Banu Salamah walimlalamikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa nyumba zao ziko mbali na Msikiti. Na hapo ikateremka:
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao. [Yaasiyn (36:12)]”
[Ibn Kathiyr katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 556]
Na pia,
حَدَّثَنَا مُحَمَّد بْن الْمُثَنَّى حَدَّثَنَا عَبْد الْأَعْلَى حَدَّثَنَا الْجُرَيْرِيّ عَنْ أَبِي نَضْرَة عَنْ أَبِي سَعِيد رَضِيَ اللَّه عَنْهُ عَنْ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِنَحْوِهِ وَفِيهِ غَرَابَة مِنْ حَيْثُ ذِكْر نُزُول هَذِهِ الْآيَة وَالسُّورَة بِكَمَالِهَا مَكِّيَّة
Ametuhadithia Muhammad bin Al-Muthannaa, ametuhadithia ‘Abdul A’alaa, ametuhadithia Al-Jariyriy toka kwa Abu Nadhwrah toka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaah ‘anhu) toka kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mfano wa Hadiyth hii. Katika Hadiyth hii, kuna utatanishi pale ilipoelezwa kuwa Aayah hii pamoja na Suwrah kamili viliteremka Makkah.
Wapokezi wa Hadiyth ni wapokezi wa Swahiyh isipokuwa ‘Abbaad bin Ziyaad ambaye kuna maneno dhidi yake kama ilivyoandikwa katika Tahdhiyb At-Tahdhiyb, lakini amepata ushirika “Mutaaba’ah” na Muhammad bin Al-Muthannaa wa kuihadithia Hadiyth moja kama unavyoona. At-Tirmidhiy ameikhariji katika Mujallad wa 4 ukurasa wa 171, na amesema ni Hasan. Pia Al-Haakim ameikhariji katika Mujallad wa 2 ukurasa wa 428 na amesema ni Swahiyh. Adh-Dhahabiy ameikubali kwa upokezi wa Abu Sa’iyd Al-Khudriyy. Lakini kwa upande wao, yupo Twariyf bin Shihaab ambaye ni dhaifu mno [wa kumbukumbu] kama ilivyoandikwa katika Al-Miyzaan. Naye kwa Al-Haakim ni Sa’iyd bin Twariyf, na huenda baadhi ya wapokezi wamemkosea.
Wakati huo huo, Hadiyth ina mwenza wake kwa
اِبْن جَرِير عَنْ اِبْن عَبَّاس رَضِيَ اللَّه عَنْهُمَا قَالَ كَانَتْ مَنَازِل الْأَنْصَار مُتَبَاعِدَة مِنْ الْمَسْجِد فَأَرَادُوا أَنْ يَنْتَقِلُوا إِلَى الْمَسْجِد فَنَزَلَتْ " وَنَكْتُب مَا قَدَّمُوا وَآثَارهمْ "
Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) aliyesema: “Nyumba za Answaar zilikuwa mbali na Msikiti, na wao wakataka wahamie Msikitini, ikateremka:
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao. [Yaasiyn (36:12)]”
Na Sanad yake ni Swahiyh.
Ama kauli ya Al-Haafidh Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) aliposema kuwa kuna utatanishi kwa kuwa Suwrah yote kamili imeteremka Makkah, basi mimi (Muqbil Al-Waadi’iyy) kwa upande wangu sijauona mwelekeo wake na uzito wa pingamizi. Na ikiwa itathibiti kuwa Aayah hii imeteremka Makkah, basi hakuna kizuizi cha uwezekano wa kuwa imeshuka mara mbili. Na kama haikuthibiti kuteremka Makkah, basi inawezekana Suwrah ikawa imeshuka Makkah isipokuwa Aayah hii moja [ya 12] kama inavyojulikana. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.