036-Asbaabun-Nuzuwl: Yaasiyn Aayah 77-83: أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
036-Asbaabun-Nuzuwl Yaasiyn 77 - 83
Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):
أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾ وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾ الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ ﴿٨٠﴾ أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ ﴿٨١﴾ إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾ فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾
Je, binaadamu haoni kwamba Sisi Tumemuumba kutokana na tone la manii, mara yeye ni mpinzani bayana? Na akatupigia mfano, akasahau kuumbwa kwake; akasema: Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshaoza na kusagika na kuwa kama vumbi. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ataihuisha Yule Aliyeianzisha mara ya kwanza; Naye ni Mjuzi wa kila kiumbe. Ambaye Amekujaalieni moto kutokana na miti ya kijani, kisha nyinyi mnauwasha. Je, kwani Yule Aliyeumba mbingu na ardhi (mnadhani) Hana uwezo wa kuumba mfano wao? Naam bila shaka (Anaweza)! Naye ni Mwingi wa kuumba Atakavyo, Mjuzi wa yote. Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: Kun! (Kuwa), nacho huwa. Basi Subhaanah! Utakasifu ni wa Ambaye Mkononi Mwake kuna ufalme wa kila kitu, na Kwake mtarejeshwa. [Yaasiyn (36): 77 – 83]
Sababun-Nuzuwl:
قَالَ اِبْن أَبِي حَاتِم حَدَّثَنَا حَدَّثَنَا عَلِيّ بْن الْحُسَيْن بْن الْجُنَيْد حَدَّثَنَا مُحَمَّد بْن الْعَلَاء حَدَّثَنَا عُثْمَان بْن سَعِيد الزَّيَّات عَنْ هُشَيْم عَنْ أَبِي بِشْر عَنْ سَعِيد بْن جُبَيْر عَنْ اِبْن عَبَّاس رَضِيَ اللَّه عَنْهُمَا قَالَ : إِنَّ الْعَاص بْن وَائِل أَخَذَ عَظْمًا مِنْ الْبَطْحَاء فَفَتَّهُ بِيَدِهِ ثُمَّ قَالَ لِرَسُولِ اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَيُحْيِي اللَّه هَذَا بَعْد مَا أَرَى ؟ فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ " نَعَمْ يُمِيتك اللَّه ثُمَّ يُحْيِيك ثُمَّ يُدْخِلك جَهَنَّم " قَالَ فَنَزَلَتْ الْآيَات مِنْ آخِر يس
Ibnu Abiy Haatim amesema: Ametuhadithia ‘Aliy bin Al-Husayn bin Al-Junayd, ametuhadithia Muhammad bin Al-‘Ulaa, ametuhadithia ‘Uthmaan bin Sa’iyd Az-Zayyaat, toka kwa Hashiym, toka kwa Abu Bishr, toka kwa Sa’iyd bin Jubayr, toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema: Al-‘Aaswiy bin Waail aliokota fupa toka Al-Batwhaa akalimeng’enya na kulipukutisha kwa mkono wake. Kisha akamwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Je, kweli Allaah Atalihuisha hili baada ya kuwa limebungulika hivi? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Na’am, Allaah Atakufisha wewe, kisha Atakufufua, halafu Atakuingiza Jahannam)). Akasema: Aayaat zikateremka mwisho wa Yaasiyn”.
[Ibnu Abiy Haatim kama ilivyo kwa Ibn Kathiyr katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 581
Hadiyth imekharijiwa na Al-Haakim katika Al-Mustadrak Mujallad wa 2 ukurasa wa 429 kupitia kwa ‘Amri bin ‘Awn toka kwa Hashiym, na kasema ni Swahiyh juu ya sharti ya Mashekih Wawili ambao hawakuikhariji.