039-Asbaabun-Nuzuwl: Az-Zumar Aayah 67: وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
039-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zumar Aayah 67
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾
Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itatekwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39:67)]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الأعمش، عَنْ إِبْرَاهِيمَ عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم مَنْ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَقَالَ: يَا أَبَا الْقَاسِمِ، أُبَلِّغَكَ أَنَّ اللَّهَ [تَعَالَى] يَحْمِلُ الْخَلَائِقَ عَلَى إِصْبَعٍ، والسموات عَلَى إِصْبَعٍ، وَالْأَرْضِينَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالشَّجَرَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالثَّرَى عَلَى إِصْبَعٍ؟ قَالَ: فَضَحِكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى بَدَتْ نَوَاجِذُهُ. قَالَ: وَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ((وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ)) إِلَى آخِرِ الْآيَةِ.
Ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, ametuhadithia Al-A’amash toka kwa Ibraahiym, toka kwa ‘Al-Qamah, toka kwa ‘Abdullaah amesema: Mtu katika Ahlul Kitaab (ambaye ni Myahudi) alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Abal Qaasim! Je umepata kujua kwamba Allaah (عز وجل) Atavibeba Viumbe juu ya Kidole (Chake Siku ya Qiyaamah), na mbingu juu ya Kidole, na ardhi juu ya Kidole, na miti juu ya Kidole. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akacheka mpaka magego yake ya mbele yakaonekana (kusadikisha na kufurahishwa na maneno hayo). Na hapo Allaa (عز وجل) Akateremsha:
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾
Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itakamatwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa! Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39:67)]
[Ahmad katika Mujallad wa 1 ukurasa wa 378]
Wapokezi wa Hadiyth hii ni Wapokezi wa Swahiyh. Walioikhariji ni Ibn Khuzaymah katika “Kitaabu At-Tawhiyd” ukurasa wa 36, Ibn Jariyr katika Mujallad wa 24 ukurasa wa 27, Al-Bayhaqiy katika “Al-Asmaa was Swifaat” ukurasa wa 333, At-Tirmidhiy ambaye amesema ni Swahiyh katika Mujallad wa 4 ukurasa wa 177, Ibn Khuzaymah katika “At-Tawhiyd” ukurasa wa 78, na At-Twabariy katika Mujallad wa 18 ukurasa wa 26 toka Hadiyth inayofanana ya Ibn ‘Abbaas. Na kwa ‘Atwaa yupo Ibn As-Saaib ambaye kumbukumbu yake ilidhoofika.
Zindusho:
Al-Haafidh As-Suyuwtwiy amesema katika “Al-Itqaan” Mujallad wa 1 ukurasa wa 34: “Hadiyth katika As-Swahiyh imekuja kwa tamshi lisemalo: “Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma”, na hii ndio sawa zaidi, kwa kuwa Aayah iliteremka Makkah.
Nami (Muqbil Al-Waadi’iyy) nasema, tamshi la “akasoma” lililopo kwenye As-Swahiyh halipingani na uwezekano wa kuwa Aayaah iliteremka [hapo hapo] kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaisoma. Ama kuwa kwake iliteremka Makkah, ikiwa imethibiti – nikimaanisha Aayah hii - kuwa ilishuka Makkah, basi hakuna kizuizi cha kuweza kushuka mara mbili. Na kama haikuthibiti kuteremka Makkah kwa Sanad Swahiyh, basi Suwrah itakuwa imeteremka Makkah isipokuwa Aayah moja. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Hadiyth iko katika “Kashf Al-Mastuwr” Mujallad wa 1 ukurasa wa 302. Ametajwa ndani yake Swadaqah bin Saabiq ambaye uadilifu wake wa kindani haujulikani, na hakumthibitisha isipokuwa Ibn Hibaan. Lakini ‘Abdullaah bin Idriys ameshirikiana naye kama ilivyo kwa Al-Haakim.