Vileja Vya Tambi

Vileja Vya Tambi

 

  

 

Vipimo:

 

 Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko  2

 Siagi - 4 Vijiko vya supu

 Maziwa (condensed) 300Ml

 Lozi zilizokatwakatwa - 1 kikombe

 Zabibu kavu  - 1 Kikombe

 Arki (essence) - 1 Kijiko cha supu

  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Weka karai kwenye moto kiasi
  2. Tia siagi
  3. Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.
  4. Weka lozi na zabibu huku unakoroga
  5. Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.
  6. Tia arki
  7. Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye  kikombe cha kahawa nusu usikijaze.
  8. Kipindue kwenye sahani utoe kileja.
  9. Fanya hivyo mpaka umalize vyote.

 

 

 

Share