043-Asbaabun-Nuzuwl: Az-Zukhruf Aayah 57: وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
043-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zukhruf Aayah 57
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾
Na mwana wa Maryam aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele na kushangilia. [Az-Zukhruf (43:57)]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شَيْبَانَ، عَنْ عَاصِمِ بْنِ أَبِي النَّجُود، عَنْ أَبِي رَزِين، عَنْ أَبِي يَحْيَى -مَوْلَى ابْنِ عُقَيْلٍ الْأَنْصَارِيِّ-قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: لَقَدْ عَلِمْتُ آيَةً مِنَ الْقُرْآنِ مَا سَأَلَنِي عَنْهَا رَجُلٌ قَطُّ، فَمَا أَدْرِي أَعَلِمَهَا النَّاسُ فَلَمْ يَسْأَلُوا عَنْهَا، أَمْ لَمْ يَفْطِنُوا لَهَا فَيَسْأَلُوا عَنْهَا. قَالَ: ثُمَّ طَفِقَ يُحَدِّثُنَا، فَلَمَّا قَامَ تَلَاوَمْنَا أَلَّا نَكُونَ سَأَلْنَاهُ عَنْهَا. فَقُلْتُ: أَنَا لَهَا إِذَا رَاحَ غَدًا. فَلَمَّا رَاحَ الْغَدُ قُلْتُ: يَا ابْنَ عَبَّاسٍ، ذَكَرْتَ أَمْسِ أَنَّ آيَةً مِنَ الْقُرْآنِ لَمْ يَسْأَلْكَ عَنْهَا رَجُلٌ قَطُّ، فَلَا تَدْرِي أَعَلِمَهَا النَّاسُ أَمْ لَمْ يَفْطِنُوا لَهَا؟ فَقُلْتُ: أَخْبِرْنِي عَنْهَا وَعَنِ اللَّاتِي قَرَأْتَ قَبْلَهَا. قَالَ: نَعَمْ، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ لِقُرَيْشٍ: "يَا مَعْشَرَ قُرَيْشٍ، إِنَّهُ لَيْسَ أَحَدٌ يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ فِيهِ خَيْرٌ"، وَقَدْ عَلِمَتْ قُرَيْشٌ أَنَّ النَّصَارَى تَعْبُدُ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ، وَمَا تَقُولُ فِي مُحَمَّدٍ، فَقَالُوا: يَا مُحَمَّدُ، أَلَسْتَ تَزْعُمُ أَنَّ عِيسَى كَانَ نَبِيًّا وَعَبْدًا مِنْ عِبَادِ اللَّهِ صَالِحًا، فَإِنْ كُنْتَ صَادِقًا كَانَ آلِهَتُهُمْ كَمَا تَقُولُونَ؟ قَالَ: فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ)) . قُلْتُ: مَا يَصِدون؟ قَالَ: يَضْحَكُونَ، ((وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِلسَّاعَةِ)) قَالَ: هُوَ خُرُوجُ عِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ قَبْلَ الْقِيَامَةِ.
Ametuhadithia Haashim bin Al-Qaasim, ametuhadithia Shaybaan, toka kwa ‘Aaswim, toka kwa Abu Raziyn, toka kwa Abu Yahyaa Mwachwa huru wa Ibn ‘Aqiyl amesema: Ibn ‘Abbaas alisema: Hakika nimeijua Aayah katika Qur-aan ambayo hakuna mtu yeyote aliyeniuliza kamwe kuhusiana na makusudio yake. Nami sijui kama watu wameifahamu vyema wasiiulizie kujua maana yake, au hawakuitia akilini wakaiulizia. Kisha akaanza kutuelezea (masuala mbalimbali), na alipoondoka tulilaumiana kwa nini tusimuulize Aayah hiyo. Nikasema: Mimi lazima niiulizie kesho, na ilipofika kesho nilimwambia: Ee Ibn ‘Abbaas! Umesema jana kuwa kuna Aayah katika Qur-aan ambayo hakuna mtu aliyewahi kukuuliza kabisa kujua ufafanuzi wake, nawe hujui kama wameielewa vyema wasiiulize au hawakuitia maanani. Nikamwambia: Nielezee pamoja na ile uliyoisoma kabla yake. Akasema vyema. Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaambia Maquraysh: Enyi jamii ya Maquraysh! Hakika hakuna yeyote anayeabudiwa badala ya Allaah ikawepo kheri ndani yake (bali wote wataingizwa motoni; mwabuduji na mwabudiwa). Na Maquraysh wamejua kwamba Manaswara wanamwabudu ‘Iysaa bin Maryam pamoja na yale wanayoyasema kuhusu Muhammad. Wakasema: Ee Muhammad! Si wewe unayedai kuwa ‘Iysaa alikuwa Nabiy na Mja mwema kati ya Waja wa Allaah? Na kama wewe ni mkweli katika maneno yako, basi waabudiwa wao ni kama unavyosema (itaingizwa pamoja nao motoni akiwemo ‘Iysaa). Akasema: Na hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:
وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾
Na mwana wa Maryam aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele na kushangilia.
Nikauliza: Nini maana ya يَصِدُّونَ? Akasema: Wanapiga kelele.
وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ
Na hakika yeye (Nabiy ‘Iysaa) ni alama ya Saa. [Az-Zukhruf (43:61)]
Akasema: Nayo ni kutoka ‘Iysaa bin Maryam kabla ya Siku ya Qiyaamah.”
[Ahmad katika Mujallad wa 1 Uk. wa 317]
At-Twahhaawiy ameikhariji Hadiyth hii katika “Mushkil Al-Aathaar Mujallad wa 1 ukurasa wa 431.