001-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Kusengenya na Amri ya Kuhifadhi Ulimi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم الغيبة والأمر بحفظ اللسان

001-Mlango Wa Kuharamishwa Kusengenya na Amri ya Kuhifadhi Ulimi

 

 

Alhidaaya.com

 

 

قال الله تَعَالَى :

وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾

Na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. [Al-Hujuraat: 12]

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾

Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa. [Al-Israa: 36]

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]

 

 

Hadiyth – 1

 

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho na aseme jambo zuri au anyamaze." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

 

وعن أَبي موسى رضي اللهُ عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسولَ اللهِ أَيُّ المُسْلمِينَ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( مَنْ سَلِمَ المُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ )) متفق عَلَيْهِ .

Amesema Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! ni Waislamu gani walio bora?" Akasema: "Muislamu ni yule ambaye Waislamu wenzake wamesalimika kutokana na shari za ulimi na mikono yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

 

وعن سهل بن سعد رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ أَضْمَنْ لَهُ الجَنَّةَ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kunidhaminia (kulinda) kilichoko baina ya taya zake (yaani ulimi) na kile kilicho baina ya miguu yake (utupu wake), basi nitamdhaminia Peponi." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 4

 

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّه سمع النبيَّ صلى الله عليه وسلم يقول : (( إنَّ العَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بالكَلِمَةِ مَا يَتَبَيَّنُ فِيهَا يَزِلُّ بِهَا إِلَى النَّارِ أبْعَدَ مِمَّا بَيْنَ المَشْرِقِ والمَغْرِبِ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika mja huendelea kuzungumza maneno ambayo ni ya kutaka kheri na kuyatafakari, basi anaepushwa na Moto kwa umbali ulio baina ya mashariki na magharibi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 5

 

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إنَّ العَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ الله تَعَالَى مَا يُلْقِي لَهَا بَالاً يَرْفَعُهُ اللهُ بِهَا دَرَجاتٍ ، وإنَّ العَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلَمَةِ مِنْ سَخَطِ اللهِ تَعَالَى لا يُلْقِي لَهَا بَالاً يَهْوِي بِهَا في جَهَنَّمَ )) . رواه البخاري .

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mja huzungumza maneno yenye kumridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) bila kuyapa umuhimu wowote, na Allaah Akamnyanyulia kwayo daraja nyingi Na hakika mja huzungumza maneno yenye kumkasirisha Allaah (سبحانه وتعالى) bila kuyapa umuhimu wowote, yakaja kumporomosha ndani ya Jahannam.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 6

 

 

وعن أَبي عبد الرحمن بِلالِ بن الحارِثِ المُزَنِيِّ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : ((إنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ اللهِ تَعَالَى مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ اللهُ لَهُ بِهَا رِضْوَانَهُ إِلَى يَومِ يَلْقَاهُ ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ سَخَطِ اللهِ مَا كَانَ يَظُنُّ أنْ تَبْلُغَ مَا بَلَغَتْ يَكْتُبُ الله لَهُ بِهَا سَخَطَهُ إِلَى يَوْمِ يَلْقَاهُ )). رواه مالك في المُوَطَّأ ، والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Abuu 'Abdir-Rahmaan Bilaal bin Al-Haarith Al-Muzniy (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Kwa hakika mja atazungumza neno linalomridhisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo Radhi Zake hadi Siku ya Qiyaamah. Na Kwa hakika mja atazungumza neno linalomkasirisha Allaah, wala asidhani kuwa litafikia lilipofikia, Allaah Amuandikie kwa neno hilo hasira Zake hadi Siku ya Qiyaamah)) [Maalik katika Muwattwa na At-Tirmidhiy ambaye amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 7

 

وعن سفيان بن عبد الله رضي اللهُ عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسولَ الله حدِّثني بأَمْرٍ أَعْتَصِمُ بِهِ قَالَ : (( قلْ : رَبِّيَ اللهُ ثُمَّ اسْتَقِمْ )) قُلْتُ : يَا رسولَ اللهِ ، مَا أخْوَفُ مَا تَخَافُ عَلَيَّ ؟ فَأَخَذَ بِلِسانِ نَفْسِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( هَذَا )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Sufyaan bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Niambie mimi jambo ambalo nitashikana nalo imara." Akasema: "Sema: Rabb Wangu ni Allaah, kisha kuwa na msimamo." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Ni kitu gani ambacho unanihofia sana?" Akashika ulimi wake, kisha akasema: "Huu." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 8

 

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تُكْثِرُوا الكَلاَمَ بِغَيْرِ ذِكْرِ اللهِ؛ فَإنَّ كَثْرَةَ الكَلاَمِ بِغَيْرِ ذِكْرِ اللهِ تَعَالَى قَسْوَةٌ لِلقَلْبِ ! وإنَّ أبْعَدَ النَّاسِ مِنَ اللهِ القَلْبُ القَاسِي )) . رواه الترمذي .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usizungumze sana bila kumdhukuru Allaah, kwani maneno mengi bila ya kumtaja Allaah Ta'aalaa yanaufanya moyo uwe mgumu. Na hakika mtu aliye mbali zaidi na Allaah ni yule mwenye moyo ngumu." [At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 9

 

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ وَقَاهُ اللهُ شَرَّ مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ ، وَشَرَّ مَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ دَخَلَ الجَنَّةَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuokolewa na Allaah na ouvu wa kilicho baina ya taya zake mbili (ulimi) na ubaya wa kilichoko baina ya miguu yake (utupu), ataingia Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 10

 

وعن عقبة بن عامرٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسولَ اللهِ مَا النَّجَاةُ ؟ قَالَ : (( أَمْسِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ ، وابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini kuokoka (kufuzu)?" Akasema: "Uzuilie ulimi wako, na kaa ndani ya nyumba yako na ulie kwa madhambi yako uliyo yafanya." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 11

 

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إِذَا أصْبَحَ ابْنُ آدَمَ ، فَإنَّ الأعْضَاءَ كُلَّهَا تَكْفُرُ اللِّسانَ ، تَقُولُ : اتَّقِ اللهَ فِينَا ، فَإنَّما نَحنُ بِكَ ؛ فَإنِ اسْتَقَمْتَ اسْتَقَمْنَا ، وإنِ اعْوَجَجْتَ اعْوَجَجْنَا )) . رواه الترمذي .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoamka mwanadamu asubuhi viungo vyake vyote vinauomba ulimi vikisema: 'Mche Allaah kwa ajili yetu, kwani sisi tunakufuata wewe, ukinyooka na kusimama wima nasi pia tutasimama wima na ukienda kombo, nasi pia tutakwenda kombo." [At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 12

 

وعن مُعَاذٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رَسُولَ اللهِ ، أَخْبِرْني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجَنَّةَ وَيُبَاعِدُني مِنَ النَّارِ ؟ قَالَ : (( لَقَدْ سَألتَ عَنْ عَظيمٍ ، وإنَّهُ لَيَسيرٌ عَلَى مَنْ يَسَّرَهُ اللهُ تَعَالَى عَلَيْهِ: تَعْبُدُ الله لا تُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً ، وَتُقِيمُ الصَّلاَةَ ، وتُؤتِي الزَّكَاةَ ، وتَصُومُ رَمَضَانَ ، وتَحُجُّ البَيْتَ )) ثُمَّ قَالَ : (( ألاَ أدُلُّكَ عَلَى أبْوابِ الخَيْرِ ؟ الصَّوْمُ جُنَّةٌ ، وَالصَّدَقَةُ تُطْفِئُ الخَطِيئَةَ كَما يُطْفِئُ المَاءُ النَّارَ ، وَصَلاَةُ الرَّجُلِ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ )) ثُمَّ تَلا : [ تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ المَضَاجِعِ ] حَتَّى بَلَغَ [ يَعْمَلُونَ ] ثُمَّ قَالَ : (( ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأَمْرِ ، وَعَمُودِهِ ، وَذِرْوَةِ سِنَامِهِ )) قُلْتُ : بَلَى يَا رسولَ اللهِ ، قَالَ : (( رَأسُ الأمْر الإسْلامُ ، وَعَمُودُهُ الصَّلاَةُ ، وَذِرْوَةِ سِنَامِهِ الجِهادُ )) ثُمَّ قَالَ : (( ألاَ أُخْبِرُكَ بِمِلاكِ ذَلِكَ كُلِّهِ ! )) قُلْتُ : بلَى يَا رَسولَ اللهِ ، فَأخَذَ بِلِسانِهِ وقال : (( كُفَّ عَلَيْكَ هَذَا )) قُلْتُ : يَا رسولَ الله وإنَّا لَمُؤاخَذُونَ بما نَتَكَلَّمُ بِهِ ؟ فقالَ : (( ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ ! وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ فِي النَّارِ عَلَى وُجُوهِهِمْ إِلاَّ حَصَائِدُ أَلْسِنَتِهِمْ ؟ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح ))

Imepokewa kutoka kwake Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nipe habari ya amali itakayonitia mimi Peponi, na kuniepusha na moto." Akasema: "Umeuliza jambo kubwa, nalo ni sahali kwa aliyemsahilishia Allaah Ta'aalaa: Ni kumuabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kufunga Ramadhwaan, na kwenda kuhiji katika nyumba (yaani Ak-Ka'abah)." Kisha akasema: "Nikujulishe wewe milango ya kheri? Saumu ni kinga, na swadaqah hufuta madhambi kama maji yanavyozima moto; pia Swalaah ya mtu katikati ya usiku." Kisha akasoma: "Mbavu zao zinatengana na vitanda"...Hadi akafikia: "Wakiyatenda" [As-Sajdah: 16-17]. Kisha akasema: "Je, nikujulishe kichwa cha jambo, na nguzo zake na kilele chake?" Nikamwambia: "Kwa nini ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Kichwa cha jambo hili ni Uislamu, na nguzo yake ni Swalaah, na kilele cha juu kabisa ni Jihadi." Kisha akasema: "Nikupe habari ya kutamalaki yote hayo?" Nikamwambia: "Kwa nini ee Rasuli wa Allaah, kwani sisi tutapatilizwa kwa tuyasemayo?" Akasema: "Uwe ni mwenye kukoswa na mamako ee Mu'aadh! Jua, kuwa watu watatoswa motoni kwa nyuso zao isipokuwa ni kwa mavuno ya ndimi zao!" [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh] 

 

 

Hadiyth – 13

 

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ ؟ )) قالوا : اللهُ وَرَسُولُهُ أعْلَمُ ، قَالَ : (( ذِكْرُكَ أخَاكَ بِما يَكْرَهُ )) قِيلَ : أفَرَأيْتَ إنْ كَانَ في أخِي مَا أقُولُ ؟ قَالَ : (( إنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ ، فقد اغْتَبْتَهُ ، وإنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدْ بَهَتَّهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza: "Je, munajua maana ya Ghiybah (useng'enyaji)?" Wakasema: "Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi." Akasema: "Ni kumtaja (kuzungumza) ndugu yako kwa anayo chukia." Pakasemwa: "Unaonaje ikiwa ndugu yangu anayo ninayosema?" Akasema: "Ikiwa analo unalosema, basi hakika umemseng'enya na ikiwa hana unalosema itakuwa umemkashifu." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 14

 

وعن أَبي بَكْرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ في خُطْبَتِهِ يَوْمَ النَّحْرِ بِمِنًى في حَجَّةِ الوَدَاعِ : (( إنَّ دِماءكُمْ ، وَأمْوَالَكُمْ ، وأعْرَاضَكُمْ ، حَرَامٌ عَلَيْكُمْ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، في شَهْرِكُمْ هَذَا، في بَلَدِكُمْ هَذَا، ألا هَلْ بَلَّغْتُ )) متفق عَلَيْهِ.

Imepokewa kutoka kwake Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika Khutbah yake siku ya kuchinja hapo Minaa katika Hijjah ya Kuaga: "Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni tukufu (hivyo ni haramu juu yenu) kama utukufu wa siku yenu ya leo, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu Ehee je sikufikisha." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 15

 

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : قُلْتُ للنبيّ صلى الله عليه وسلم : حَسْبُكَ مِنْ صَفِيَّةَ كذَا وكَذَا . قَالَ بعضُ الرواةِ : تَعْنِي قَصيرَةً ، فقالَ : (( لَقَدْ قُلْتِ كَلِمَةً لَوْ مُزِجَتْ بِمَاءِ البَحْرِ لَمَزَجَتْهُ ! )) قالت : وَحَكَيْتُ لَهُ إنْسَاناً فَقَالَ : (( مَا أُحِبُّ أنِّي حَكَيْتُ إنْساناً وإنَّ لِي كَذَا وَكَذَا )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Inatosha kwako kujua ya kwamba Swafiyyah ni kadha na kadha." Wamesema baadhi ya wapokezi: "Akimaanisha kuwa ni mfupi." Akasema: "Hakika umesema neno lau lingetiwa katika bahari, lingebadilisha tamu au harufu ya maji hayo." Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Nilimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati mmoja mambo yasiyo mazuri kuhusu mtu." Akasema: "Sipendi kabisa kusikia jambo lolote lisilokuwa zuri kuhusu mtu yoyote, hata kama nitapatiwa kitu kadha na kadha." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh] 

 

 

Hadiyth – 16

 

وعن أنسٍ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَمَّا عُرِجَ بي مَرَرْتُ بِقَومٍ لَهُمْ أظْفَارٌ مِنْ نُحَاسٍ يَخْمِشُونَ وُجُوهَهُمْ وَصُدُورَهُمْ فَقُلْتُ : مَنْ هؤُلاءِ يَا جِبرِيلُ ؟ قَالَ : هؤُلاءِ الَّذِينَ يَأكُلُونَ لُحُومَ النَّاسِ ، وَيَقَعُونَ في أعْرَاضِهِمْ ! )) . رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilipopandishwa mbinguni (katika usiku wa Miraji) nilipita kwa kaumu waliokuwa na makucha ya shaba waliyokuwa wakikwaruza nyuso zao na vifua vyao." Nikauliza: "Hawa ni kina nani, ee Jibriyl?" Akasema: "Hawa ni wale ambao kwamba walikuwa wakila nyama za watu na kuwatweza (kuwataharisha)." [Abuu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 17

 

وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( كُلُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِمِ حَرَامٌ : دَمُهُ وَعِرْضُهُ وَمَالُهُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila Muislamu ni haramu kwa Muislamu mwenzake: Damu yake, cheo chake, na mali yake." [Muslim]

 

 

Share