002-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kusikiliza Kusengenya na Amri kwa Mwenye Kusikia Kumkataza Msemaji na Akishindwa au Asipokubali Kutoka Kwake Basi Aondoke Kwenye kikao

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم سماع الغيبة

وأمر من سمع غيبةً مُحرَّمةً بِرَدِّها والإنكارِ عَلَى قائلها

فإنْ عجز أَوْ لَمْ يقبل منه فارق ذلك المجلس إن أمكنه

002-Mlango Wa Uharamu wa Kusikiliza Kusengenya na Amri kwa Mwenye Kusikia Kumkataza Msemaji na Akishindwa au Asipokubali Kutoka Kwake Basi Aondoke Kwenye kikao

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ  ﴿٥٥﴾

Na wanaposikia maneno ya upuuzi hujitenga nayo [Al-Qaswasw: 55]

وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿٣﴾

Na ambao wanajiepusha na mambo ya upuuzi. [Al-Muuminuwn: 3]

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾

Na wala usifuate usiyo na elimu nayo. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa. [Al-Israa: 36]

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾

Na unapowaona wale wanaoshughulika kuzisakama Aayaat Zetu, jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu. [Al-An'aam: 68]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أخيهِ ، رَدَّ اللهُ عَنْ وَجْهِهِ النَّارَ يَومَ القيَامَةِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwake Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kurudisha cheo na heshima ya nduguye, Allaah Atauepusha uso wake na moto Siku ya Qiyaamah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 2

وعن عِتبَانَ بنِ مَالكٍ رضي اللهُ عنه ، في حديثه الطويل المشهور الَّذِي تقدَّمَ في بابِ الرَّجاء قَالَ : قام النبيّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي فَقَالَ : (( أيْنَ مالِكُ بنُ الدُّخْشُمِ ؟ )) فَقَالَ رَجُلٌ : ذَلِكَ مُنَافِقٌ لا يُحِبُّ اللهَ ولا رَسُولهُ ، فَقَالَ النبيّ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَقُلْ ذَلِكَ ألاَ تَراهُ قَدْ قَالَ : لا إلهَ إِلاَّ اللهُ يُريدُ بِذَلكَ وَجْهَ اللهِ ! وإنَّ الله قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ : لا إلهَ إِلاَّ اللهُ يَبْتَغي بِذَلِكَ وَجْهَ اللهِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Amesema 'Itbaan bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika Hadiyth ndefu mashuhuri ambayo imetangulia kutajwa katika mlango "Kuwa na Matumaini" kwamba: "Alisimama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali akasema: "Yu wapi Maalik bin Ad-Dukhshum?" Akasema mtu mmoja: "Yule ni mnafiki ambaye hampendi Allaah wala Rasuli Wake." Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Usiseme hivyo, je huoni kuwa amesema Laa ilaaha Illa Allaah akitaka ridhaa za Allaah. Hakika Allaah amemharamishia moto yeyote anayesema Laa ilaaha Illa Allaah akitafuta ridhaa ya Allaah kwa hilo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن كعب بن مالك رضي اللهُ عنه في حديثه الطويل في قصةِ تَوْبَتِهِ وَقَدْ سبق في باب التَّوبةِ. قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ جالِسٌ في القَومِ بِتَبُوكَ : (( مَا فَعَلَ كَعبُ بن مالكٍ ؟ )) فَقَالَ رَجلٌ مِنْ بَنِي سَلمَةَ: يَا رسولَ الله ، حَبَسَهُ بُرْدَاهُ والنَّظَرُ في عِطْفَيْهِ . فَقَالَ لَهُ مُعاذُ بنُ جبلٍ رضي اللهُ عنه : بِئْسَ مَا قُلْتَ ، والله يَا رسولَ الله مَا علمنا عَلَيْهِ إِلاَّ خَيْراً ، فَسَكَتَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Ka'ab bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika Hadiyth ndefu kuhusu kusamehewa kwake na tayari Hadiyth hii imetangulia kuelezwa katika mlango wa "Tawbah": Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliuliza alipokuwa amekaa na kaumu huko Tabuwk: "Ka'ab amefanya nini?" Akasema mtu mmoja kutoka kwa Bani Salamah: "Ee Rasuli wa Allaah! Amezuiliwa na burga zake kwa mbili (nguo) na kuangalia mabega yake kwa kibri." Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) akamwambia: "Ni jambo baya ulilosema! Naapa kwa Allaah, ee Rasuli wa Allaah! Hatujui chochote kwake isipokuwa kheri." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinyamaza." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share