019-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuwa na Dhana Mbaya kwa Waislamu Bila ya Dharura

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن سوء الظنّ بالمسلمين من غير ضرورة

019-Mlango Wa Kukatazwa Kuwa na Dhana Mbaya kwa Waislamu Bila ya Dharura

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ ﴿١٢﴾

Enyi walioamini!  Jiepusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. [Al-Hujuraat: 12]

 

 

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إيَّاكُمْ والظَّنَّ ، فإنَّ الظَّنَّ أكْذَبُ الحَدِيثِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tahadharini na dhana, kwani dhana ni uwongo mkubwa katika mazungumzo." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Share