018-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupeleleza na Kusikiliza Mazungumzo kwa Wasiotaka Usikiliza

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النَّهي عن التجسُّس

والتَّسَمُّع لكلام من يكره استماعه

018-Mlango Wa Kupeleleza na Kusikiliza Mazungumzo kwa Wasiotaka Usikiliza

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَلَا تَجَسَّسُوا ﴿١٢﴾

Na wala msichunguzane [Al-Hujuraat: 12]

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إيَّاكُمْ وَالظَّنَّ ، فَإنَّ الظَّنَّ أَكْذَبُ الحَدِيثِ ، ولا تحسَّسوا وَلاَ تَجَسَّسُوا وَلاَ تَنَافَسُوا ، وَلاَ تَحَاسَدُوا ، وَلاَ تَبَاغَضُوا ، وَلاَ تَدَابَرُوا ، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إخْوَاناً كَمَا أَمَرَكُمْ .المُسْلِمُ أَخُو المُسْلِمِ ، لاَ يَظْلِمُهُ ، وَلاَ يَخْذُلُهُ وَلاَ يَحْقِرُهُ ، التَّقْوَى هاهُنَا التَّقْوَى هاهُنَا )) وَيُشِيرُ إِلَى صَدْرِهِ (( بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أنْ يَحْقِرَ أخَاهُ المُسْلِمَ ، كُلُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِمِ حَرَامٌ : دَمُهُ ، وَعِرْضُهُ ، وَمَالُهُ . إنَّ اللهَ لاَ يَنْظُرُ إِلَى أجْسَادِكُمْ ، وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ ، وَلكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وأعْمَالِكُمْ )) .

وَفِي رواية : (( لاَ تَحَاسَدُوا، وَلاَ تَبَاغَضُوا ، وَلاَ تَجَسَّسُوا ، وَلاَ تَحَسَّسُوا ، وَلاَ تَنَاجَشُوا وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إخْواناً )) .

وفي رواية : (( لاَ تَقَاطَعُوا ، وَلاَ تَدَابَرُوا ، وَلاَ تَبَاغَضُوا ، وَلاَ تَحَاسَدُوا ، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إخْواناً )) وَفِي رِواية : (( وَلاَ تَهَاجَرُوا وَلاَ يَبِعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ )) . رواه مسلم بكلّ هذِهِ الروايات ، وروى البخاريُّ أكْثَرَهَا .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tahadharini na dhana, kwani dhana ni uwongo mkubwa katika mazungumzo. Wala msiulizie ulizie kuhusu makosa ya watu wala msipeleleze wala msishindane katika kupata kitu cha mtu mwengine wala msihusudiane wala msichukiane wala msiwakane nyongo, lakini kuweni enyi waja wa Allaah ndugu kama Alivyo waamuru. Muislamu ni ndugu wa Muislamu: hamdhulumu, wala haachi kumsaidia, wala hamdhuru. Uchamungu uko hapa - akaashiria kwenye kifua chake. Yamtosha mtu kuwa ni miongoni mwa shari kumdharau ndugu yake Muislamu. Kila Muislamu ni haramu kwa Muislamu mwenzake: damu yake, cheo chake na mali yake. Hakika Allaah Hatizami miili yenu wala sura zenu, lakini Anaangalia mioyo yenu na amali zenu." 

Na katika riwaayah nyengine: "Msihusudiane, wala msichukiane, wala msipelelezane, wala msiulizie ulizie kuhusu makosa ya watu wengine, wala msiongezeane bei (pasina kuwa na haja ya kununua), lakini kuweni enyi waja wa Allaah ndugu." 

Na katika riwaayah nyengine: "Wala msisusiane, wala msipeane nyongo, wala msichukiane, wala msihusudiane, lakini kuweni ndugu enyi waja wa Allaah." 

Na katika riwaayah nyengine: "Wala msitengane, wala wasinunue baadhi yenu kilichokwisha kuuziwa wenzenu." [Muslim kwa riwaayah zote hizo, na Al-Bukhaariy amepokea nyingi miongoni mwa hizo riwaayah]

 

 

Hadiyth – 2

وعن معاوية رضي الله عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقول : (( إنَّكَ إنِ اتَّبَعْتَ عَوْرَاتِ المُسْلِمينَ أفْسَدْتَهُمْ ، أَوْ كِدْتَ أنْ تُفْسِدَهُمْ )) . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Amesema Mu'awiyah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika ukifuata katika kuangazia makosa ya Waislamu utawafisidi (utawaharibu) au utaelekea katika kuwafisidi." [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawud kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن مسعود رضي الله عنه : أنَّهُ أُتِيَ بِرَجُلٍ فَقِيلَ لَهُ : هَذَا فُلاَنٌ تَقْطُرُ لِحْيَتُهُ خَمْراً ، فَقَالَ : إنَّا قَدْ نُهِيْنَا عَنِ التَّجَسُّسِ، ولكِنْ إنْ يَظْهَرْ لَنَا شَيْءٌ، نَأخُذ بِهِ . حديث حسن صحيح ، رواه أَبُو داود بإسنادٍ عَلَى شَرْطِ البخاري ومسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliletwa mtu kwake na kuambiwa: "Huyu ni fulani, ambaye ndevu zake zinanuka pombe." Akasema: "Hakika tumekatazwa jambo tunalichukua kama lilivyo." [Hadiyth Hasan Swahiyh, Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri kulingana na sharti zilizowekwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share