023-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kughushi na Kuhadaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن الغش والخداع

023-Mlango Wa Kukatazwa Kughushi na Kuhadaa

 

Alhidaaya.com

 

 

قال الله تَعَالَى :

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا السِّلاَحَ فَلَيْسَ مِنَّا ، وَمَنْ غَشَّنَا فَلَيْسَ مِنَّا )) . رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، مَرَّ عَلَى صُبْرَةِ طَعَامٍ فَأدْخَلَ يَدَهُ فِيهَا فَنَالَتْ أصابِعُهُ بَلَلاً ، فَقَالَ : (( مَا هذَا يَا صَاحِبَ الطَّعَامِ ؟ )) قَالَ : أصَابَتهُ السَّمَاءُ يَا رسول الله . قَالَ : (( أفَلاَ جَعَلْتَهُ فَوقَ الطَّعَامِ حَتَّى يرَاهُ النَّاسُ ! مَنْ غشَّنَا فَلَيْسَ مِنَّا )) .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kubeba silaha kupigana dhidi yetu, si katika sisi. Na mwenye kutughushi, si katika sisi." [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyengine, kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita mbele ya chakula kilichokuwa kimewekwa, akaingiza mkono wake, hivyo vidole vyake kupata umande. Akasema: "Hii ni nini, ee mwenye chakula hiki?" Akajibu: "Kimenyeshwa na mvua, ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Kwa nini hukukiweka juu ya chakula ili kipate kuonekana na watu? Mwenye kutughushi, si katika sisi." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( لاَ تَنَاجَشُوا )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wala msiongezeane bei (pasina kuwa na haja ya kununua)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، نَهى عن النَّجْشِ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kuongezeana bei." [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : ذَكَرَ رَجُلٌ لِرَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : أنَّهُ يُخْدَعُ في البُيُوعِ ؟ فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ بَايَعْتَ ، فَقُلْ : لاَ خِلاَبَةَ )) . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alielezwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kuwa kuna mtu mmoja ambaye anadanganywa sana katika biashara. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Unapoingia katika biashara (kununua) na mtu yeyote mwambie, 'Hakuna udanganyifu'." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ خَبَّبَ زَوْجَةَ امْرِئٍ ، أَوْ مَمْلُوكَهُ ، فَلَيْسَ مِنَّا )) . رواهُ أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumharibu na kumhadaa mke wa mtu au kijakazi, basi si miongoni mwetu." [Abuu Daawuwd].

 

 

Share