024-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuvunja Ahadi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم الغدر

024-Mlango Wa Kukatazwa Kuvunja Ahadi

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ  ﴿١﴾

Enyi walioamini! Timizeni mikataba. [Al-Maaidah: 1]

وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾

Na timizeni ahadi, hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa. [Al-Israa: 34]

 

Hadiyth – 1

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنافِقاً خَالِصاً ، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَها : إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa, na kama atakuwa na moja katika hayo manne atakuwa na sifa moja ya unafiki mpaka aliache; kama akiaminiwa anaongopa; na anapotoa ahadi huvunja  na anapogombana anaicha haki na kuwa jeuri." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعودٍ ، وابن عمر ، وأنس رضي الله عنهم قالوا : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم : (( لِكُلِّ غادِرٍ لِواءٌ يَوْمَ القِيَامَةِ ، يُقَالُ : هذِهِ غَدْرَةُ فلانٍ )) . متفق عَلَيْهِ .

Wamesema Ibn Mas'uwd, na Ibn 'Umar na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhum) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kwa kila mwenye kuvunja ahadi atakuwa na bendera (kama ishara na alama) Siku ya Qiyaamah na patatangazwa: 'Huyu ni yule aliyevunja ahadi na fulani." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيدٍ الخدريّ رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ عِنْدَ اسْتِهِ يومَ القِيَامَةِ يُرْفَعُ لَهُ بِقَدَرِ غَدْرِهِ ، ألاَ وَلاَ غَادِرَ أعْظَمُ غَدْراً مِنْ أمِيرِ عَامَّةٍ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kwa kila mwenye kuvunja ahadi atakuwa na bendera watu wengine wakiwa nyuma yake Siku ya Qiyaamah ambayo atanyanyuliwa kiasi cha uvunjaji wake na ahadi. Sikilizeni na tanabahini! Hapana mvunjaji mkubwa wa ahadi kama amiri (kiongozi mabaye si mkweli kwa watu wake)." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( قَالَ الله تَعَالَى : ثَلاَثَةٌ أنا خَصْمُهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ : رَجُلٌ أعْطَى بي ثُمَّ غَدَرَ ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرَّاً فَأَكَلَ ثَمَنَهُ ، وَرَجُلٌ اسْتَأجَرَ أجيراً ، فَاسْتَوْفَى مِنْهُ ، وَلَمْ يُعْطِهِ أجْرَهُ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa Amesema: 'Watu aina tatu Nitapigana nao Siku ya Qiyaamah; mtu anayeweka miadi kwa kuapa kwa jina Langu kisha akavunja ahadi hiyo; na mtu aliyemuuza mtu aliye huru kisha akala thamani yake; na mtu aliyemwajiri mtu mwengine ambaye alifanya kazi kamili lakini akakosa kumlipa ujira wake." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share