025-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumsimanga Mtu kwa Ulichompa na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن المنِّ بالعطية ونحوها

025-Mlango Wa Kukatazwa Kumsimanga Mtu kwa Ulichompa na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ  ﴿٢٦٤﴾

Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia [Al-Baqarah: 264]

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ ﴿٢٦٢﴾

Wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia [Al-Baqarah: 262]

 

 

 

وعن أَبي ذَر رضي الله عنه ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( ثَلاَثَةٌ لاَ يُكَلِّمُهُمُ اللهُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، وَلاَ يَنْظُرُ إلَيْهِمْ ، وَلاَ يُزَكِّيِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَليمٌ )) قَالَ : فَقَرَأَهَا رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ثلاثَ مِرارٍ : قَالَ أَبُو ذرٍ : خَابُوا وخَسِرُوا مَنْ هُمْ يَا رسول الله ؟ قَالَ : (( المُسْبِلُ ، والمَنَّانُ ، وَالمُنْفِقُ سِلْعَتَهُ بالحَلِفِ الكَاذِبِ )) . رواه مسلم .

وفي روايةٍ لَهُ : (( المُسْبِلُ إزَارَهُ )) يَعْنِي : المُسْبِلَ إزَارَهُ وَثَوْبَهُ أسْفَلَ مِنَ الكَعْبَيْنِ لِلخُيَلاَءِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Hatazungumza na watu aina tatu Siku ya Qiyaamah wala Hatawaangalia na wala Hatawatakasa na watakuwa na adhabu iumizayo." Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliikariri kauli hii mara tatu." Akasema Abu Dharr: "Watu hao wamehasirika, ni kina nani ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Mwenye kuburuza nguo kwa kiburi; na mwenye kujionyesha kwa fadhila aliyomfanyia mtu mwengine; na mwenye kuuza mali duni kwa kiapo cha uongo." [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyengine: "Mwenye kuburuza kikoi chake." Yaani: "Mwenye kuburuza kikoi chake na nguo yake chini ya kongo mbili kwa kiburi."

 

Share