026-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kujifakhiri na Ujeuri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن الافتخار والبغي

026-Mlango Wa Kukatazwa Kujifakhiri na Ujeuri

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm: 32]

إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٢﴾

Hakika sababu (ya kulaumiwa) ni juu ya wale wanaodhulumu watu na wanakandamiza katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iumizayo. [Ash-Shuwraa: 42]

 

Hadiyth – 1

وعن عياضِ بن حمارٍ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ تَعَالَى أوْحَى إلَيَّ أنْ تَوَاضَعُوا حَتَّى لا يَبْغِيَ أَحَدٌ عَلَى أحَدٍ ، وَلاَ يَفْخَرَ أَحَدٌ عَلَى أحَدٍ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Iyaadh bin Himaar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa Amenifunulia mimi kuwa niwe mnyenyekevu mpaka mtu mmoja asiwe mjeuri kwa mwengine wala asijifakhiri mtujuu ya mtu mwengine." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا قَالَ الرجُلُ : هَلَكَ النَّاسُ ، فَهُوَ أهْلَكُهُمْ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindi anaposema mtu: Watu wameangamia (wamekufa), basi ni yeye ndiye aliyeangamia." [Muslim]

 

 

Share