027-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuhamana Baina ya Waislamu Wawili Zaidi ya Siku Tatu ila Ikiwa ni Mtu wa Bid'ah au Ufasiki na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم الهجران بين المسلمين فوق ثلاثة أيام

إِلاَّ لبدعة في المهجور ، أَوْ تظاهرٍ بفسقٍ أَوْ نحو ذَلِكَ

027-Mlango Wa Kukatazwa Kuhamana Baina ya Waislamu Wawili Zaidi ya Siku Tatu ila Ikiwa ni Mtu wa Bid'ah au Ufasiki na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. [Al-Hujuraat: 10]

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ  ﴿٢﴾

Na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah: 2]

 

Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تَقَاطَعُوا ، وَلاَ تَدَابَرُوا ، وَلاَ تَبَاغَضُوا ، وَلاَ تَحَاسَدُوا ، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إخْوَاناً ، وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلاَث )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wala msisusiane, wala msipeane nyongo, wala msichukiane, wala msihusudiane, lakini kuweni ndugu enyi waja wa Allaah. Na haifai kwa Muislamu kumhama nduguye zaidi ya siku tatu." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي أيوبَ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( لا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثِ لَيَالٍ : يَلْتَقِيَانِ ، فَيُعْرِضُ هَذَا ، وَيُعْرِضُ هَذَا ، وخَيْرُهُما الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلاَمِ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ayyuwb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si halali kwa Muislamu kumhama nduguye kwa zaidi ya siku tatu kwa jinsi ya kwamba wanakutana huku kila mmoja akimpa nyongo mwenzake. Na mbora kati yao ni yule anayeanza kutoa salamu (kumsalimia mwenziwe)." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( تُعْرَضُ الأَعْمَالُ في كلِّ اثْنَيْنِ وَخَمْيسٍ ، فَيَغْفِرُ اللهُ لِكُلِّ امْرِئٍ لا يُشْرِكُ باللهِ شَيْئاً ، إِلاَّ امْرَءاً كَانَتْ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أخِيهِ شَحْنَاءُ ، فَيقُولُ : اتْرُكُوا هذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Milango ya Pepo hufunguliwa siku ya Jumatatu na Alkhamis, hivyo kusamehewa kila mja asiyemshirikisha Allaah kwa kitu chochote isipokuwa mtu ambaye ana uadui (utesi) baina yake na nduguye. Atasema: 'Waacheni hawa wawili mpaka wafanye mapatano baina yao! Waacheni hawa wawili mpaka wafanye mapatano baina yao!." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن جابر رضي الله عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( إنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ يَئِسَ أنْ يَعْبُدَهُ المُصَلُّونَ فِي جَزِيرَةِ العَرَبِ ، وَلَكِنْ في التَّحْرِيشِ بَيْنَهُمْ )) . رواه مسلم .

Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika shetani amevunjika moyo kabisa kuwa hataabudiwa na Waislamu (wenye kuswali) katika Bara Arabu, hivyo anajaribu kuleta utesi na kuleta ufisadi baina yao na kubadilisha mioyo yao." [Muslim].

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يَهْجُرَ أخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثٍ ، فَمَنْ هَجَرَ فَوْقَ ثَلاَثٍ فَمَاتَ ، دَخَلَ النَّارَ )) . رواه أَبُو داود بإسناد عَلَى شرط البخاري ومسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa Muislamu kumhama nduguye zaidi ya siku tatu. Na yeyote atakaye mhama mwenziwe zaidi ya siku tatu akafa (katika hali hiyo) ataingia motoni." [Abu Daawuwd kwa Isnaad zinazo afikiana na masharti ya Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي خِراشٍ حَدْرَدِ بنِ أَبي حَدْرَدٍ الأسلميِّ . ويقالُ : السُّلمِيّ الصحابي رضي الله عنه : أنَّه سمع النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( مَنْ هَجَرَ أخَاهُ سَنَةً فَهُوَ كَسَفْكِ دَمِهِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Khiraash Hadrad bin Abu Hadrad Al-Aslamiyy na pia anajulikana kama As-Sulamiyy As-Swahabiy (ambaye ni Swahaaba) (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote anayemhama nduguye mwaka mzima ni kama amemwaga damu yake (yaani amemuua). [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh].

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنًّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَحِلُّ لِمُؤْمِنٍ أنْ يَهْجُرَ مُؤْمِناً فَوقَ ثَلاَثٍ ، فإنْ مَرَّتْ بِهِ ثَلاَثٌ ، فَلْيَلْقَهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ ، فَإنْ رَدَّ عَلَيْهِ السَّلامَ فَقَدِ اشْتَرَكَا في الأجْرِ ، وَإنْ لَمْ يَرُدَّ عَلَيْهِ فَقَدْ بَاءَ بِالإثْمِ ، وَخَرَجَ المُسَلِّمُ مِنَ الهِجْرَةِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد حسن . قَالَ أَبُو داود : (( إِذَا كَانَتْ الهِجْرَةُ للهِ تَعَالَى فَليسَ مِنْ هَذَا في شَيْءٍ ))

Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haifai kwa Muumini kumhama nduguye Muumini kwa zaidi ya siku tatu. Baada ya siku tatu, inafaa aende kukutana naye na kumsalimia. Ikiwa atajibu hiyo salamu basi wote wawili wameshirikiana katika thawabu. Na ikiwa hatajibu hiyo salamu basi atakuwa na dhambi, na yule wa kwanza (aliyetoa salamu) atajivua na jukumu la kuhamana (na kukata urafiki)." [Abu Daawuwd, kwa Isnaad iliyo Swahiyh]. Amesema Abu Daawuwd: "Ikiwa kutozungumza ni kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa, hatakuwa na dhambi yoyote."

 

 

Share