030-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Kuadhibu Mnyama Yoyote Hata Chungu na Mfano Wake Kutumia Moto

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم التعذيب بالنار

في كل حيوان حَتَّى النملة ونحوها

030-Mlango Wa Kuharamishwa Kuadhibu Mnyama Yoyote Hata Chungu na Mfano Wake Kutumia Moto

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرةَ رضي الله عنه قَالَ : بعثنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في بَعْثٍ، فَقَالَ : (( إنْ وَجَدْتُمْ فُلاَناً وَفُلاناً )) لِرَجُلَيْنِ مِنْ قُرَيْشٍ سَمَّاهُمَا (( فَأَحْرِقُوهُمَا بالنَّارِ )) ثُمَّ قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِيْنَ أرَدْنَا الخرُوجَ: (( إنِّي كُنْتُ أَمَرْتُكُمْ أنْ تُحْرِقُوا فُلاناً وفُلاناً ، وإنَّ النَّارَ لا يُعَذِّبُ بِهَا إِلاَّ الله ، فإنْ وَجَدْتُمُوهُما فاقْتُلُوهُما )) . رواه البخاري.

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma kikosi kwa ajili ya Jihadi, na akawaambia: "Mukimpata fulani na fulani (akawataja watu wawili wa Ki-Quraysha) wachomeni kwa moto." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia tulipokuwa tayari kuondoka: "Hakika nilikuwa nimewaamuru muwachome fulani na fulani, lakini ni Allaah tu Anayeadhibu kwa moto. Hivyo mukiwapata wauweni." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ : كنَّا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ ، فانْطَلَقَ لحَاجَتِهِ ، فَرَأيْنَا حُمَّرَةً مَعَهَا فَرْخَانِ ، فَأَخَذْنَا فَرْخَيْهَا ، فَجَاءتِ الحُمَّرَةُ فَجَعَلَتْ تَعْرِشُ فَجَاءَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : (( مَنْ فَجَعَ هذِهِ بِوَلَدِهَا ؟ ، رُدُّوا وَلَدَهَا إِلَيْها )) . ورأَى قَرْيَةَ نَمْلٍ قَدْ حَرَّقْنَاهَا ، فَقَالَ : (( مَنْ حَرَّقَ هذِهِ ؟ )) قُلْنَا : نَحْنُ قَالَ : (( إنَّهُ لا يَنْبَغِي أنْ يُعَذِّبَ بالنَّارِ إِلاَّ رَبُّ النَّارِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح

Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari na tuliposimama sehemu kwa mapumziko, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliondoka kwenda kutekeleza haja yake. Tulimuona ndege mwekundu pamoja na watoto wake wawili. Tulivichukua vitoto vyake, yule mama alifadhaika sana kuona hayo na akaanza kupiga ardhi kwa mbawa zake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alirudi na kuuliza: "Ni nani aliyemtatiza ndege huyu kwa kuchukua watoto wake? Warudisheni vitoto vyake." Na baada ya hapo akaona kichuguu (kijiji cha chungu) kimechomwa, akasema: "Kwa hakika haifai yeyote kuadhibu kwa moto isipokuwa Rabb wa moto." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

 

Share