038-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukaa Faragha na Mwanamke wa Kando

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم الخلوة بالأجنبية

038-Mlango Wa Kukaa Faragha na Mwanamke wa Kando

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ  ﴿٥٣﴾

Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. [Al-Ahzaab: 53]

 

Hadiyth – 1

وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إيَّاكُمْ وَالدُّخُولَ عَلَى النِّسَاءِ ! )) فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ : أفَرَأيْتَ الحَمْوَ ؟ قَالَ : (( الحَمْوُ المَوْتُ ! )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jiepushenina kuwazuru wanawake (wasio maharimu zenu)." Akauliza mtu miongoni mwa Answaar: "Unaonaje kuhusu Hamwa?" (Ni jamaa wa karibu wa mume kama ndugu, na mtoto wa ndugu yake na mtoto wa ami yake, na kadhalika). Akasema: "Huyu Hamwa ni mauti (ni hatari zaidi)." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( لاَ يَخْلُونَّ أَحَدكُمْ بامْرَأَةٍ إِلاَّ مَعَ ذِي مَحْرَمٍ )) . متفق عَليْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asikae faragha mmoja wenu na mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن بُريدَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( حُرْمَةُ نِسَاءِ المُجَاهِدِينَ عَلَى القَاعِدِينَ كَحُرْمَةِ أُمَّهَاتِهِمْ ، مَا مِنْ رَجُلٍ مِنَ القَاعِدِيْنَ يَخْلُفُ رَجُلاً مِنَ المُجَاهِدِينَ في أهْلِهِ ، فَيَخُونُهُ فِيهِمْ إِلاَّ وَقَفَ لَهُ يَوْمَ القِيَامَةِ ، فَيَأْخُذُ مِنْ حَسَنَاتِهِ مَا شَاءَ حَتَّى يَرْضى )) ثُمَّ التَفَتَ إلَيْنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: (( مَا ظَنُّكُمْ ؟ )). رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Uharamu wa wanawake wa Mujahidina kwa wenye kubakia nyuma ni kama uharamu wa mama zao. Hapana mtu miongoni mwa walio baki nyuma atakaye kuwa mwangalizi wa familia ya mtu miongoni mwa Mujahidina, kisha akamhini isipokuwa atamsimamia Siku ya Qiyaamah na kuchukua thawabu zake anazotaka mpaka aridhike." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitugeukia sisi na kusema: "Je, munadhania nini?" [Muslim]

 

 

Share