039-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Wanaume Kushabihiana na Wanawake na Kinyume Chake Katika Mavazi, Mwendo na Mengineo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم تشبه الرجال بالنساء

وتشبه النساء بالرجال في لباس وحركة وغير ذَلِكَ

039-Mlango Wa Uharamu wa Wanaume Kushabihiana na Wanawake na Kinyume Chake Katika Mavazi, Mwendo na Mengineo

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : لَعَنَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم المُخَنَّثِينَ مِنَ الرِّجَالِ ، وَالمُتَرَجِّلاَتِ مِنَ النِّسَاءِ .

وفي رواية : لَعَنَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم المُتَشَبِّهِينَ مِنَ الرِّجَالِ بالنِّسَاءِ ، والمُتَشَبِّهَاتِ مِنَ النِّسَاءِ بالرِّجَالِ . رواه البخاري .

Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wenye kuwaiga wanawake na wanawake wenye kuwaiga wanaume. 

Na katika riwaayah nyengine: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wenye kujishabahisha na wanawake, na wanawake wenye kujifananisha na wanaume." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : لَعَنَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم الرَّجُلَ يَلْبَسُ لِبْسَةَ المَرْأَةِ ، والمَرْأَةَ تَلْبِسُ لِبْسَةَ الرَّجُلِ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanaume mwenye kuvaa vazi la mwanamke na mwanake anayevaa vazi la mwanaume." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( صِنْفَانِ مِنْ أهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا : قَومٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأذْنَابِ البَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلاَتٌ مَائِلاَتٌ ، رُؤُوسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ البُخْتِ المائِلَةِ لاَ يَدْخُلْنَ الجَنَّةَ ، وَلاَ يَجِدْنَ رِيحَهَا ، وإنَّ رِيحَهَا لَيُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكذَا )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuili wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aina mbili ya watu ni watu wa motoni, bado sijawaona: Watu wenye mijeledi sawa na mikia ya ng'ombe wanayoitumia kupiga watu. Na pia wanawake waliovaa nguo (Kaasiyaat) lakini wapo uchi ('Aariyaat) ambao hugeuza mabega yao kwa maringo na kutembea mwendo wa kimalaya. Vichwa vyao vitakuwa kama nundu ya ngamia (yaani wanazifanya vikubwa kwa kujifunga kilemba au kitambara kichwani au mfano wake). Hawataingia Peponi wala hata kuisikia harufu yake, japokuwa harufu yake itasikika masafa kadhaa na kadhaa." [Muslim]

 

 

Share