040-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kujifananisha na Shetani na Makafiri

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن التشبه بالشيطان والكفار

040-Mlango Wa Kukatazwa Kujifananisha na Shetani na Makafiri

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن جابر رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَأكُلُوا بِالشِّمَالِ ، فَإنَّ الشَّيْطَانَ يَأكُلُ ويَشربُ بِالشِّمَالِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Usile kwa mkono wa kushoto, kwani shetani anakula na kunywa kwa mkono wa kushoto." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَأكُلَنَّ أَحَدُكُمْ بِشِمَالِهِ ، وَلاَ يَشْرَبَنَّ بِهَا ، فَإنَّ الشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ وَيَشْرَبُ بِهَا )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asile mmoja wenu kwa mkono wa kushoto wala ainywe nao, kwani shetani anakula kwa mkono wa kushoto na kunywa nao." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ اليَهُودَ وَالنَّصَارى لاَ يَصْبغُونَ ، فَخَالِفُوهُمْ )) . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Mayahudi na Manaswara (wakiristo) hawatii rangi nywele zao, hivyo fanyeni kinyume na wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share