041-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Mwanaume na Mwanamke Kutia Rangi Nyeusi katika Nywele zao

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب نهي الرجل والمرأة عن خضاب شعرهما بسواد

041-Mlango Wa Kukatazwa Mwanaume na Mwanamke Kutia Rangi Nyeusi katika Nywele zao

 

Alhidaaya.com

 

عن جابر رضي الله عنه قَالَ : أُتِيَ بِأَبِي قُحَافَةَ والِدِ أَبي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ رضي الله عنهما ، يَومَ فَتْحِ مَكَّةَ وَرَأسُهُ وَلِحْيَتُهُ كَالثَّغَامَةِ  بَيَاضاً . فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( غَيِّرُوا هَذَا وَاجْتَنِبُوا السَّوَادَ )) . رواه مسلم .

Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliletwa Abu Quhaafah, babake Abu Bakar As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) siku iliyofunguliwa Makkah na ilhali kichwa chake na ndevu zake zilikuwa nyeupe pepepe mfano wa Thaghaamah (ni mti unaotoa maua na matunda meupe). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Mbadilisheni hii (rangi yake ya nywele) na jiepusheni na rangi nyeusi." [Muslim]

 

 

Share