042-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kunyoa na Kubakishia Vijisehemu Visivyo Nyolewa (Denge) na Kukubaliwa Kunyoa Zote kwa Wanaume na Wala si kwa Wanawake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن القَزَع وَهُوَ حلق بعض الرأس

دون بعض ، وإباحة حَلْقِهِ كُلّهِ للرجل دون المرأة

042-Mlango Wa Kukatazwa Kunyoa na Kubakishia Vijisehemu Visivyo Nyolewa (Denge) na Kukubaliwa Kunyoa Zote kwa Wanaume na Wala si kwa Wanawake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : نهَى رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم عن القَزَعِ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunyoa na kubakisha vijisehemu bila ya kuvinyoa. [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : رأَى رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم صَبِيّاً قَدْ حُلِقَ بَعْضُ شَعْرِ رَأسِهِ وَتُرِكَ بَعْضُهُ ، فَنَهَاهُمْ عَنْ ذَلِكَ ، وقال : (( احْلِقُوهُ كُلَّهُ ، أَوِ اتْرُكُوهُ كُلَّهُ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح عَلَى شرط البخاري ومسلم .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona mtoto ambaye amekatwa nywele sehemu moja ya kichwa chake na kuachwa sehemu nyengine, akawakataza jambo hilo. Na akasema: "Mnyoweni zote (nywele) au mwacheni zote." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh kulingana na sharti ya Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن جعفر رضي الله عنهما : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، أمْهَلَ آلَ جَعْفَر ثَلاَثاً ثُمَّ أتَاهُمْ فَقَالَ : (( لاَ تَبْكُوا عَلَى أخِي بَعْدَ اليَوْمِ )) ثُمَّ قَالَ : (( ادْعُوا لِي بَنِي أَخِي )) فَجِيءَ بِنَا كَأنَّنَا أفْرُخٌ فَقَالَ : (( ادْعُوا لِي الحَلاَّقَ )) فَأمرَهُ ، فَحَلَقَ رُؤُوسَنَا . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح عَلَى شرط البخاري ومسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Ja'far (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaruhusu watoto wa Ja'far kuwa na huzuni kwa ajili yake kwa muda wa siku tatu. Kisha akaja kwao na kuwaambia: "Musilie kwa ajili ya ndugu yangu baada ya leo." Kisha akasema: "Niitieni watoto wa ndugu yangu." Kwa ajili ya huzuni tuliyokuwa nayo hali yetu ilikuwa kama vifaranga. Akasema: "Niitieni kinyozi." (Alipofika) alimuamuru atunyoe, naye (kinyozi) akafanya hivyo." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh kulingana na sharti ya Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 4

وعن عليٍّ رضي الله عنه قَالَ : نَهَى رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنْ تَحْلِقَ المَرْأةُ رَأسَهَا . رواه النسائي .

Amesema 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza wanawake kunyoa nywele za vichwa vyao. [An-Nasaaiy]

 

 

 

Share