064-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusamehewa kwa Kutotekeleza Yamini ya Upuuzi Kuwa Halina Kafara, Nayo ni Kusema kwa Ulimi Bila ya Kukusudia Yamini Kama Kauli Yake ya Ada: Sivyo Wa-Allaahi na Ndio Wa-Allaahi na Mfano wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب العفو عن لغو اليمين

وأنَّه لا كفارة فِيهِ ، وَهُوَ مَا يجري عَلَى اللسان بغير

قصد اليمين كقوله عَلَى العادة : لا والله ، وبلى والله ، ونحو ذَلِكَ

064-Mlango Wa Kusamehewa kwa Kutotekeleza Yamini ya Upuuzi Kuwa Halina Kafara, Nayo ni Kusema kwa Ulimi Bila ya Kukusudia Yamini Kama Kauli Yake ya Ada: Sivyo Wa-Allaahi na Ndio Wa-Allaahi na Mfano wake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ  ﴿٨٩﴾

Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu. [Al-Maaidah: 89]

 

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : أُنْزِلَتْ هذِهِ الآية : [ لاَ يُؤاخِذُكُمُ اللهُ بِاللَّغْوِ في أَيْمَانِكُمْ ] في قَوْلِ الرَّجُلِ : لا واللهِ ، وَبَلَى واللهِ . رواه البخاري .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Ayah hii iliteremshwa: 'Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi' (Aal-'Imraan: 89), kwa mtu anaye kuwa na mazoea ya kusema: 'Sivyo hivyo Wa-Allaahi na ndio Wa-Allaahi'." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share