065-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kula Yamini katika Biashara Hata Akiwa Mkweli

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب كراهة الحلف في البيع وإنْ كان صادقاً

065-Mlango Wa Ukaraha wa Kula Yamini katika Biashara Hata Akiwa Mkweli

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه قال : سَمِعتُ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( الحَلِفُ مَنْفَقَةٌ لِلسِّلْعَةِ ، مَمْحَقَةٌ لِلْكَسْبِ )) . متفق عليه .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kuapa sana katika biashara huenda kukaongeza mauzo lakini inafuta faida yote uliyopata." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 2

وعن أبي قتادة رضي الله عنه : أنَّه سمعَ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إيَّاكُمْ وَكَثْرَةَ الحَلِفِ فِي البَيْعِ ، فَإنَّهُ يُنَفِّقُ ثُمَّ يَمْحَقُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Jiepusheni na kuapa yamini sana katika kuuza (bidhaa zenu), kwani hilo mwanzo huboresha biashara na kisha huleta hasara." [Muslim]

 

 

Share