078-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kuusifu Uzuri wa Mwanamke Mbele ya Mwanaume ila Anapohitajia Hilo kwa Haja Inayokubaliwa na Sheria Kama Kumuoa na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن وصف محاسن المرأة لرجل

إلاَّ أن يحتاج إلى ذلك لغرض شرعي كنكاحها ونحوه

078-Mlango Wa Kukatazwa Kuusifu Uzuri wa Mwanamke Mbele ya Mwanaume ila Anapohitajia Hilo kwa Haja Inayokubaliwa na Sheria Kama Kumuoa na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com

 

عن ابن مسعودٍ رضي الله عنه ، قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تُبَاشِرِ المَرْأَةُ المَرْأَةَ ، فَتَصِفَهَا لِزَوْجِهَا كَأَنَّهُ يَنْظُرُ إلَيْهَا )) . متفق عليه .

imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke asimguse mwanamke mwenziwe sehemu zake za siri kisha amsifie mumewe uzuri wake wa kimaumbile kama kwamba anamuona." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share