079-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Mtu Kusema: Ee Mola Wangu Nisamehe Ukipenda Bali Aazimie katika Maombi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة قول الإنسان : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي إنْ شِئْتَ

بل يجزم بالطلب

079-Mlango Wa Ukaraha wa Mtu Kusema: Ee Mola Wangu Nisamehe Ukipenda Bali Aazimie katika Maombi

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَ يَقُولَنَّ أَحَدُكُمْ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي إنْ شِئْتَ : اللَّهُمَّ ارْحَمْنِي إنْ شِئْتَ ، لِيَعْزِم المَسْأَلَةَ ، فَإنَّهُ لاَ مُكْرِهَ لَهُ )) . متفق عليه .

وفي رواية لمسلم : (( وَلكِنْ لِيَعْزِمْ وَلْيُعَظمِ الرَّغْبَةَ فَإنَّ اللهَ تَعَالَى لاَ يَتَعَاظَمُهُ شَيْءٌ أَعْطَاهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asiseme mmoja wenu: 'Ee Mola wangu nisamehe ukitaka. Ee Mola wangu nirehemu Ukitaka.' Bali aazimie katika kumuomba Allaah kwa sababu hakuna wa kumlazimisha Yeye (Allaah)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

Na riwaayah ya Muslim: "Lakini aazimie na awe na matumaini makubwa, kwani hakuna kitu chochote ambacho ni kikubwa kwa Allaah Ta'aalaa kutoa."

 

Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إذا دَعَا أحَدُكُمْ فَلْيَعْزِم المَسْأَلَةَ ، وَلاَ يَقُولَنَّ : اللَّهُمَّ إنْ شِئْتَ ، فَأَعْطِنِي ، فَإنَّهُ لاَ مُسْتَكْرِهَ لَهُ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoomba mmoja wenu aazimie kwa dhati na asiseme: 'Ee Mola wangu! Ukitaka nipe'. Kwa sababu hakuna wa Kumkalifisha kitu dhidi ya Utashi Wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share